Umemalizia kwa Mh Mbowe apumzike kwa lipi? Mbona umemalizia kirahisi sana kuliko ulivyoanza!! Ebu rudi tena utueleze apumzike kivipi, na awe mshahuri kivipi.
Pili ujue Chadema ni chama cha siasa, chenye lengo la kushika dola.
Kwahiyo hakijafikia hilo lengo bado, sasa unapokuwa na mwenyekiti ambae amekitoa chama kikiwa na wabunge wanne, mpaka kufika 70 hii leo, halafu unasema apumzike ili iweje?
Hauoni ni kurudisha chama nyuma?
Na kama chama tawala chenyewe, mwenyekiti wake ni yule anaekuwa Rais, hauoni hapo kuwa bado kinaogopa kumpa uenyekiti mtu tofauti ili asije mvuruga Rais?
Mh msomi mimi nakupinga kwa hoja zako, uongozi ni kalama na sio kila mtu anafaa kuongoza. Wengine lazima waandaliwe ili waongoze, kwa chama chetu Chadema mimi nasema tunamuhitaji Mh Mbowe kuliko yeye anavyokihitaji chama chetu.
Naunga mkono hoja ya Mh Mbowe kugombea tena uenyekiti wa chama, mpaka pale Tanzania itakapo pata Rais sahihi wa kuongoza nchi.