Si Cecil Mwambe wala John Heche wanaotosha uenyekiti CHADEMA Taifa, Uenyekiti una mambo mengi

Cecil Mwambe mwenyewe sidhani, jamaa ana busara ila sema ndio kahamia tu mwaka 2015 kutokana na kukatwa CCM , japo nampongeza kwa kutorudi CCM tena ambako angeshind tena uchaguzi wa marudio na kuwa na maisha rahisi kuliko upinzani
Naona anayefaa zaidi ni John Heche, Heche aliwahi kuwa mwenyekiti wa vijana na yupo dedicated kwa chama sana na pia ni mtu tough, jambi ambalo linalohitajika kwenye siasa hizi za kibabe
Akina Selasini na Mnyika watawapa CCM sababu ya kueneza zile propaganda za kikabila kuwa ni Chama cha kanda ya Kaskazini, japo Mnyika sijui ni mtu wa wapi
John Heche is the best option baada ya Mbowe
 
Mnyika na Selasini watakoleza zile propaganda ya chama cha kaskazini sijui cha wachaga, Heche anafaa sana
 
Ahahhaa
 
Tundu Lisu haruhusiwi kugombea? Naaamn yule ana msimamo thabithi / Tuondoke Kaskasini tuwekeze na maeneo mengine
 
Umemalizia kwa Mh Mbowe apumzike kwa lipi? Mbona umemalizia kirahisi sana kuliko ulivyoanza!! Ebu rudi tena utueleze apumzike kivipi, na awe mshahuri kivipi.
Pili ujue Chadema ni chama cha siasa, chenye lengo la kushika dola.
Kwahiyo hakijafikia hilo lengo bado, sasa unapokuwa na mwenyekiti ambae amekitoa chama kikiwa na wabunge wanne, mpaka kufika 70 hii leo, halafu unasema apumzike ili iweje?
Hauoni ni kurudisha chama nyuma?
Na kama chama tawala chenyewe, mwenyekiti wake ni yule anaekuwa Rais, hauoni hapo kuwa bado kinaogopa kumpa uenyekiti mtu tofauti ili asije mvuruga Rais?
Mh msomi mimi nakupinga kwa hoja zako, uongozi ni kalama na sio kila mtu anafaa kuongoza. Wengine lazima waandaliwe ili waongoze, kwa chama chetu Chadema mimi nasema tunamuhitaji Mh Mbowe kuliko yeye anavyokihitaji chama chetu.
Naunga mkono hoja ya Mh Mbowe kugombea tena uenyekiti wa chama, mpaka pale Tanzania itakapo pata Rais sahihi wa kuongoza nchi.
Sifa za niliyowataja ni hizo ambazo akina Heche hawana kwa sasa.
 
Lengo lenu iendelee kuwa chama cha kaskazini tu
Kinachotakiwa ni kiongozi Mkuu.
Uongozi ni Hekima awe wa kusini,kaskazini,mashariki au magharibi ili mradi atekeleze majukumu yake ipasavyo.
 
100% true
 
mi binafs na muunga mkono John Heche kuwa Mwenyekiti chadema
 
Nilitegemea utatuwekea sifa za watu uliowataja, kama ni kutaja majina tu hata mimi nilishapendekeza Membe anafaa sana uenyekiti wa CCM ila sijui kwanini hawanisikii.
Umemaliza kazi, uumemjibu vizuri sana!
 
Hayo mambo ya kuchagua ukanda eti fulani ni wa Kaskazini, mmeanguka kwenye mtego wa CCM huku mkijua kabisa.... matokeo yake ndio mnaleta kina Mashinji ambao hawana impact yoyote kisiasa.

You are doomed.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…