KabisaHayo mambo ya kuchagua ukanda eti fulani ni wa Kaskazini, mmeanguka kwenye mtego wa CCM huku mkijua kabisa.... matokeo yake ndio mnaleta kina Mashinji ambao hawana impact yoyote kisiasa.
You are doomed.
Mshawishini atangaze nia, au ni dhambi?mi binafs na muunga mkono John Heche kuwa Mwenyekiti chadema
Heche ni mtiifu kwa Mbowe atajitoa hawezi kuingia naye kwenye uchaguzi....Cecil Mwambe mwenyewe sidhani, jamaa ana busara ila sema ndio kahamia tu mwaka 2015 kutokana na kukatwa CCM , japo nampongeza kwa kutorudi CCM tena ambako angeshind tena uchaguzi wa marudio na kuwa na maisha rahisi kuliko upinzani
Naona anayefaa zaidi ni John Heche, Heche aliwahi kuwa mwenyekiti wa vijana na yupo dedicated kwa chama sana na pia ni mtu tough, jambi ambalo linalohitajika kwenye siasa hizi za kibabe
Akina Selasini na Mnyika watawapa CCM sababu ya kueneza zile propaganda za kikabila kuwa ni Chama cha kanda ya Kaskazini, japo Mnyika sijui ni mtu wa wapi
John Heche is the best option baada ya Mbowe
Ya katiMnyika ni wa kanda gani?
Mnyika wa kaskazini mkoa gani?Mnyika na 30 Wote wa kaskazini hatukubali
Kilimanjaro ya Upareni
Mnyika wa kaskazini mkoa gani?
Mimi ni mtu wa Mbeya nawachukia sana wanaohangaika na ukanda ni mawazo ya hovyo sana, tuangalie uwezo wa mtu kura za wajumbe ndio zitazoamua.Hayo mambo ya kuchagua ukanda eti fulani ni wa Kaskazini, mmeanguka kwenye mtego wa CCM huku mkijua kabisa.... matokeo yake ndio mnaleta kina Mashinji ambao hawana impact yoyote kisiasa.
You are doomed.
mkuu msomi, umenichanganya kidogo......inakuwaje kama huna maslahi ndani ya hiki chama utake Mbowe aondoke kwenye uenyekiti kwa mfano? vipi wenye chama chao wakimhitaji tena, wewe unaona si sawa?Mwanzo mwanzoni niseme wazi kuwa mimi si na sijawahi kuwa mwanachama wa CHADEMA au chama kingine chochote cha siasa hapa Tanzania au kwingineko duniani. Hilo linatosha kutoa maoni yangu huru kuhusu siasa za nchi yangu kwakuwa nazifuatilia.
CHADEMA wanapaswa kufanya uchaguzi mkuu wa kichama kitaifa mwaka huu(kwa mujibu wa Msajili wa Vyama vya Siasa wameshachelewa/ na wao CHADEMA wanadai waliusogeza uchaguzi wao mbele kwa kikao hadi Disemba mwaka huu.
Katika uchaguzi huo, nafasi mbalimbali zitagombewa. Lakini, nafasi ya juu kabisa ya kichama ni ya Mwenyekiti wa Taifa. Nafasi hii ni nyeti kwenye chama chochote-isipokuwa ACT Wazalendo yenye Kiongozi Mkuu wa Chama. Sababu ni kuwa Mwenyekiti ni nembo na kielelezo cha chama.
Mwenyekiti anapaswa kujaa busara, hekima, utulivu, ubunifu, uimara, ukali na upole ambavyo vitatumika kwa nyakati tofauti kulingana na matakwa yaliyo mezani. Si kila wakati huhitajika moja au lingine, hutegemea na mazingira. Mwenyekiti ndiye mtu wa mbele.
Chama ni itikadi na imani. Chama ni nidhamu na utii kwa sheria,taratibu na kanuni zinazokiongoza. Chama ni kukubali au kukataa vikaoni; kupongeza au kukosoa vikaoni. Mwenyekiti hapaswi kuwa mkurupukaji au mfuata upepo au mpendasifa.
Kwa maoni yangu, na kwa sifa nilizozianisha hapo juu, si Cecil Mwambe wa Ndanda wala John Heche wa Tarime wanaofaa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa. Wanapaswa kuwa darasani kiuongozi kwa muda kidogo kabla ya kukabidhiwa chama hicho.
Mapendekezo yangu yangekuwa John John Mnyika wa Kibamba au Joseph Selasini wa Rombo. Lakini, Mbowe anapaswa kupumzika na kuketi benchi la washauri wa chama.