The Boss
JF-Expert Member
- Aug 18, 2009
- 49,282
- 117,244
Huu wimbo wa kila Rais kuambiwa anauza nchi ulianza kwa Rais Mwinyi, unajua sababu ilikuwaje?
Baada ya Nyerere kwenda China mwaka 1966 akasema akakuta kule China kila kitu kinafanywa na serikali kuanzia maduka ya mchele na sigara hadi magari ya taxi na bakery za kuuza mikate.U communist ulikuwa umepamba Moto sana sana, ingawa leo wachina washaufuta kabisa huo ucommunits. Lakini kipindi Nyerere anaenda huko hadi Suti zile tunaita Kaunda Suit Nyerere alitoa huko kwa wachina. Waziri mkuu wao anaitwa Choun Enlai kama sikosei, Kaunda nae alizitoa huko huko kwa wachina.
Nyerere aliporudi mwaka 1967 akapitisha Azimio la Arusha na kuanza rasmi "siasa za Ujama na kujitegemea" na kutaiifisha biashara zote za watu binafsi na majumba yao na kampuni za Serikali za kuuza mchele na sigara zikaanzishwa kukaja RTC ikaja Co Cabs kampuni ya taxi ya serikali. RTC na maduka ya kijiji na mtaa na shirika la kusaga na kukoboa unga na Makampuni Tele Tele ya serikali.
Ikawa marufuku kwa mwananchi kumiliki taxi yako binafsi hata kununua gari tu Kwa kibali maalum kwanza. Ikawa marufuku kuwa hata na kiduka cha kuuza mchele na unga na sigara, ukifanya hivyo wewe ni mhujumu wa uchumi na bepari na mkabaila. Siasa hizo pia zilifanya kila shirika kuwe na ofisi ya CCM wananchi wanafundishwa utii na itikadi za siasa ya Ujamaa na kujitegemea.
Pamoja na mazuri mengi sana ya Nyerere na siasa ya Ujamaa na kujitegemea lakini ukweli usemwe ku copy kila kitu Kwa wachina bila kuangalia mazingira yetu alikosea sana hasa pale alipojaribu kuanzisha vijiji vya ujamaa. Watu wakaondolewa kwa nguvu kwenye mashamba yao wakalazimishwa kulima shamba la kijiji.
Wengine waliogoma wakachomewa nyumba zao moto waende wahamie kwenye vijiji vya ujamaa, wapo walioliwa na Simba na wengi walipohamia huko wakawa masikini zaidi. Hadi zoezi la vijiji vya ujamaa likapigwa stop, nchi ikaingia na njaa, uzalishaji ukapungua.
Kupata bidhaa kama sigara na mchele au unga ikawa Kwa kupanga foleni na kupigana vikumbo kwenye maduka ya vijiji na mitaa. Hali ikawa mbaya zaidi vita ya Uganda ilipofika.
Wakati Mwinyi anachukua nchi hali ilikuwa mbaya sana ikabidi aanze na kuruhusu watu binafsi wafanye biashara hizo ndogo ndogo kama kuuza mikate, mchele na sigara ili serikali itoke huko. Kampuni kama co cabs ya Taxi ikabidi iaachwe ife kifo cha kawaida, maduka ya RTC ikabidi nayo yafe, watu wenye exposure kidogo na biashara.
Wahindi, waarabu since Wana mitaji ya ndugu zao nje uzoefu wakawa wa kwanza kushika biashara hizo kabla ya waswahili, wachaga, wakinga n.k kuja later kuzishika na kuwa replace kabisa baadae. Wakati haya yote yanayokea alichoambulia Mwinyi ni matusi tu ya "kuuza nchi "na "kuwapa wahindi na waraabu" njia za uchumi as if kuna mswahili aliezuiwa kumiliki duka la kuuza mchele na sigara.
Leo hiii Kariakoo yote imejaa watu wa makabila tofauti, watu wamejiongeza now wanaenda wenyewe popote pale iwe China au Uturuki, haijalishi we mkinga au mchaga unafanya biashara popote Kwa uwezo wako wa akili na mtaji.
Popote leo ukianzisha mashine ya kusaga na kukoboa mchele au duka la jumla hakuna wa kukuita bepari wala kabaila, wala kukutisha.
Kilelele ilikuwa mwaka 1992 ambapo Mwinyi alifuta kabisa Azimio la Arusha na kuleta Azimio la Zanzibar ambalo lilipiga kabisa marufuku ya wananchi kunyayaswa Kwa aina yoyote kuhusu vibali vya biashara, wala kuuliza uliza watu kuhusu biashara wanazotaka kufanya na kuanza kuwaletea zengwe la "makabaila na mabepari"
Matusi aliyopata Mwinyi kuwa "anauza nchi" yalikuwa makubwa sana na mambo ya kumuita Mzanzibari tunataka Tanganyika yalikuwa mengi Sana kama sasa tu au pengine zaidi lakini alipokuja Rais Mtanganyika watu walikuwa tayari washazoea "matunda ya Rais Mwinyi' kiasi washasahau kuwa walikuwa wanataka turudi nyuma tena kwenye maduka ya serikali na taxi za Serikali na maduka ya vijiji na serikali kuuza mikate na sigara.
Sometimes kuwatoa watu kwenye kiza unaweza ambulia matusi makubwa sana. Hadi watu hao wafike kwenye mwanga ndo wanakuja kugundua aaha kumbe tulikuwa tunakuja huku.