Si kila anayetoka Kagera ni Mhaya

Mkuu, ninatamani sana kufika Wilaya moja inaitwa Kyerwa. Ninasikia katika Wilaya hiyo moja kuna mipaka ya nchi mbili za Uganda na Rwanda?
Nadhani ilikuwa hiyo kabla ya Karagwe haijagawanywa wilaya mbili.

Kwa upande wa Uganda ni Wilaya ya Kyerwa kata ya Murongo. Huko kuna pombe inaitwa Uganda walaji hiyo usipime.

Kwa upande wa Rwanda sina kumbukumbu nzuri lakini ni wilaya ya Karagwe kata za Bweranyange, Nyaishozi etc. Nakumbuka miaka ya 2004-2006 walienda kijiji kimoja mpakani wakakuta 90% ya wakazi ni Wanyarwanda. Tatizo wanahamia na mifugo yao yaani ni shida kabisa.
 
Missenyi imepakana na kyerwa na bukoba, ukitoka Missenyi utaenda kyerwa halafu Karagwe.

Mkuu hujui chochote kuhusu Kagera, Missenyi imepakana na Bukoba na Karagwe then ndo Kyerwa. Hii wilaya ya Kyerwa ipo mpakani huko mwa Rwanda na juu Uganda
 
Mkuu hujui chochote kuhusu Kagera, Missenyi imepakana na Bukoba na Karagwe then ndo Kyerwa. Hii wilaya ya Kyerwa ipo mpakani huko mwa Rwanda na juu Uganda
Mkuu, Missenyi na kyerwa si zote mwanzo zilihesabika Karagwe?
 
Mkuu hujui chochote kuhusu Kagera, Missenyi imepakana na Bukoba na Karagwe then ndo Kyerwa. Hii wilaya ya Kyerwa ipo mpakani huko mwa Rwanda na juu Uganda
Mi sijapinga kuhusu kupakana, labda kwa kuwa sijasema inapakana na Karagwe, na aliyetoka Missenyi akapita Karagwe akaenda Kyerwa ndio akafika rusumo labda ndio umueleweshe vizuri mkuu.
 
Mkuu hujui chochote kuhusu Kagera, Missenyi imepakana na Bukoba na Karagwe then ndo Kyerwa. Hii wilaya ya Kyerwa ipo mpakani huko mwa Rwanda na juu Uganda
Mkuu nisamehe bure[emoji16][emoji16] nimepitia komenti yangu sikumaanisha kutoka Misenyi unaingia kyerwa maana huko ni kuzunguka, lakini pia inategemea unatokea Missenyi sehemu gani, japo Misenyi huko ndani sipafahamu
 
Ukitoka Karagwe Wakati Unakwenda Rusomo Ndiyo Utapita
Kyerwa
We jamaa acha uongo,Rusumo ipo karibu na biharamulo,ni njia ya kwenda N'gara,Kama unataka kahama,unapita nyakanazi(,njia panda ya kigoma,)
Kufika kyerwa,unaweza kupitia karagwe,au Kama unataka bukoba mjini,unaweza ukapita kagera sugar,ukaingia Uganda,then unaibukia kyerwa,karibu na Mulongo border
 
Wengine sisi ni Waingereza Ila kwetu Kanyigo
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kuna ile clip Mzee wa kihaya anawasilisha rambirambi msibani
 
Ulifika Hadi pande za Ngara
🤔
 
Unapajua Kyanyamisa?
yupo sahihi ukitoka Rusumo unakuja Benaco then unaingia pori la Kimisi hapo Kyanyamisa ndio barrier ya mwisho ya polisi na ipo wilaya ya kyerwa ukitoka hapo unaitafuta omurushaka Karagwe.
 
Katika wilaya zote za Kagera Ngara ipo good Sana landscape yake
 
Unapotoka Bukoba mjini mpka Kyaka pale kuna njia panda ya kwenda Mtukura yaani mpk wa Uganda na Tanzania alafu kushoto unaenda Karangwe ambapo unaenda mpk Ngara ambapo utapata mpaka wa Rwanda na Tanzania alafu Burundi na Tanzania ila mipaka hiyo ipo kwenye wilaya tatu tofauti lakini zipo kwenye ukanda moja... Sema ni raha sana kwa sababu kuna utamu wa vitu vya mpakani....
 
Unapajua Kyanyamisa?
yupo sahihi ukitoka Rusumo unakuja Benaco then unaingia pori la Kimisi hapo Kyanyamisa ndio barrier ya mwisho ya polisi na ipo wilaya ya kyerwa ukitoka hapo unaitafuta omurushaka Karagwe.
Hapana,hapo bado kabisa kufika wilaya ya Kyerwa hapo ni Karagwe ili kufika wilaya ya Kyerwa kwa barabara hiyo ni baada ya kupita Omurushaka uelekee Nkwenda siyo Kayanga
 
Nakushauri kasome tena historia vizuri ya mkoa wa Kagera. Wanahistoria wengine wanasema kuwa neno "haya" lilitokana na matatizo ya mawasiliano kati ya wageni/wakoloni wa mwanzo na wenyeji wa mkoa wa Kagera wa wakati huo. Kutokana na matatizo ya lugha ya mawasiliano miongoni mwa wenyeji wa Kagera na wakoloni, wazungu hawa walishangaa kila wakiongea na wenyeji neno "haya" linaloashiria kukubali au kusema "ndiyo" lilijitokeza sana kwa wenyeji wa Muleba, Bukoba Mjini na Vijijini na Karagwe.

Hata hivyo kwa wilaya ya Biharamulo na Ngara ilikuwa tofauti, hawakusikia hili neno "haya". Hawa hawako kwenye kundi la Wahaya kwa utafiti wa wakoloni.

Kwahiyo wazungu hao collectively wakawabatiza wenyeji hawa "Wahaya". Kwahiyo kiuhalisia Kagera hakuna kabila linaitwa wahaya. Wahaya ni mkusanyiko watu wanaojiita WanyaIhangiro (Muleba), Waziba, Wahyoza (Bukoba M/V), Wanyambo (Karagwe) nk. Acha niishie hapa kwa leo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…