Si kila tatizo linahitaji kumweleza Mtu!

Tufe na tai shingoni sio ?

Wanasaikolojia wanasema, ile tu kumsimulia mtu changamoto unazopitia, hata kama hujatatua hio changamoto kuna namna unapona maumivu/msongo/msononeko
 
Binti:

Huwa napendelea sana mada zako maana, kwa kiasi fulani, zinaonyesha ukomavu katika baadhi ya mambo. Hata hivyo kuna wakati huwa nahisi kama wakati mwingine thread zako zinakuwa ndefu unnecessarily. Kama unavyojua attention span ya watu wengi siku hizi ni shida. Hivyo pengine kuna watu wengi tu ambao wanakosa busara zako kwa uzi kuwa mrefu bila sababu za msingi. Kama ukiweza, na kama ulimwelewa vizuri mwalimu wako wa Ufupisho darasa la 4 somo la Kiswahili, hebu jaribu kuwa unazifupisha hizi thread bana bila kuzipotezea utamu na mguso wake. Huu ni ushauri na observation yangu tu na so lazima uuzingatie πŸ™πŸΏ.

Back to the topic: Privacy is power hasa kwetu introverts. Mpaka nikaseme kitu kwa mtu aisee labda sijui iweje. Labda nikiambiwa nina terminal cancer na nina mwezi mmoja tu wa kuishi. Naamini kwamba mbali na mama yangu, hakuna mtu mwingine anayenitakia mema kwa asilimia 100 hapa duniani. Hata marafiki zangu naamini hawapendi wakisikia I am doing better than them. Ndo maana hata ikitokea nikawashirikisha kitu (kizuri au kibaya), sisemi ukweli wote. Nasema ambacho nadhani kitaendana na uhalisia wao. Ndivyo ninavyoishi. Nikibanana sana afadhali nikaongee na therapist huko asiyenijua au bro wangu asiye na makuu Evelyn Salt πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Zaidi ya hapo ni mimi na Mungu wangu tunasaidiana kutatua changamoto zinazotukabili πŸ™πŸΏ
 
Siyo kwa ubaya pia lakini naomba nikusahihishe Mkuu.

Iko hivi, unapozungumzia mambo ya kina kama emotional intelligence, healing, na self counseling unahitaji context, ukiandika kifupi unaua picha halisi ya tatizo na unamnyima msomaji nafasi ya kutafakari hatua kwa hatua.

Watu wengi ambao huwa wanakimbia threads ndefu ukifuatilia walio wengi huwa hawana uwezo wa kusoma kwa umakini, unapowaandikia kifupi hapo unawalisha chakula kilichotafunwa.

Ni heri kuwa na wasomaji na wachangiaji hata 10 ambao watakuwa wameelewa context nzima kuliko kuwa nao 100 ambao wataishia kusoma juu juu tu na wasielewe context nzima ya mada.
 
Exactly πŸ’―
πŸ‘πŸ‘πŸ‘
Sawa sawa
Kaka ❀️❀️
Aiseeee πŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™Œ
β€οΈβ€οΈβ€οΈβ€οΈβ€οΈβ€οΈβ€οΈβ€οΈβ€οΈβ€οΈβ€οΈβ€οΈβ€οΈβ€οΈβ€οΈβ€οΈβ€οΈπŸ‘πŸ™
 
Tufe na tai shingoni sio ?

Wanasaikolojia wanasema, ile tu kumsimulia mtu changamoto unazopitia, hata kama hujatatua hio changamoto kuna namna unapona maumivu/msongo/msononeko
Hapana sijasema usishirikishe watu ila sio kila tatizo ni la kushirikisha watu

Maana wakati mwingine tunaweza kutatua wenyewe bila kushirikisha watu na pengine hao watu wasiwe watu sahihi wa kuwashirikisha
 
Asante kwa maoni yako karibu tena
Hongera sana bro karibu tena
 
Upo sahihi ngoja tuende na wachache wanaolewa

Uzuri ni kua nina aina nyingi za mada
Mara nyingine nakua kwenye siasa
Kwenye habari kama hizi za leo
Bila kusahau mada za wakubwa πŸ˜…

So kila mmoja anaependa kusoma mada zangu ata enjoy tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…