Si kila tatizo linahitaji kumweleza Mtu!

1. Kutangaziwa hapo ndo penyewe 😝unaweza kujuta kuelezea tatizo lako
Hii mwenyewe ni shahidi so mpka nakuja na hili bandiko nimejifunza
Na this time najifunza ku solve matatizo yangu madogo madogo bila kuomba ushauri
2. Kila mtu ana matatizo yake. Hapa nimejifunza kitu.unaweza kuomba ushauri kwa mtu ambaye hayuko huko kabisa na hata hakusikilizi.😜
Anaweza mtu kukusikiliza ukadhani utasaidika kumbe umemuuzia udhaifu ambao atautumia dhidi yako
Mimi Niko radhi kuomba ushauri kwa asiyenijua na nisiyemjua kabisa
Sahihi kabisa japo pia umakini unahitajika
 
In fact,
suala la kutegemeana kwa binadamu kwa mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kushauriana haliepukiki, na hakunaga bingwa wa maisha katika ulimwengu huu. Tunahitajiana sana kama binadamu.

Ni muhimu sana kujizuia kutoa siri za ufalme wako kwa watesi wako ambao saa zingine unaweza kudhani ni rafiki zako sana, kwasababu kwa kufanya hivyo unawapa urahisi wa kukuangamiza kwa namna ambayo hutatarajia.

Lakini pia,
ni vizuri kuepuka kujiuliza na kujijibu mwenyewe, hasa kwenye mazingira ambayo unahitaji jawabu mbadala la changamoto yako nje ya mawazo yao, athowise unaweza kujikuta jibu au suluhisho la ulichojiuliza ikawa ni kujinyonga, na kwamba hiyo ndio the best solution kwa ulichojiuliza.

Tugeuze changamoto tunazokumbana nazo kua fursa muhimu sana za kutufanya tuwe makini zaidi, tujipange upya, tujirekebishe, tujisahihishe na kufanya vizuri zaidi mbeleni 🐒
 
Unahitajika umakini mkubwa sana hapa pia.
Tukome Sasa kujieleza 😝
 
In fact,
suala la kutegemeana kwa binadamu kwa mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kushauriana haliepukiki, na hakunaga bingwa wa maisha katika ulimwengu huu. Tunahitajiana sana kama binadamu.
Gentleman nimesema sio mara zote unatakiwa kuomba ushauri
Kama jambo unalimudu limalize mwenyewe hii ni nzuri pia kuepka niliyoyasema kwenye mada yangu
Ni muhimu sana kujizuia kutoa siri za ufalme wako kwa watesi wako ambao saa zingine unaweza kudhani ni rafiki zako sana, kwasababu kwa kufanya hivyo unawapa urahisi wa kukuangamiza kwa namna ambayo hutatarajia.
Hapa nagongelea na nyundo mara zote watu wanao kumaliza ni wale uliowaamini na kuwauzia kila kitu kukuhusu mpka udhaifu wako
Narudia kwamba sisemi watu wasiombe ushauri

Nimesema watu wajaribu kutatua matatizo yao binafsi

lakini kama mzigo ni mkubwa basi ni sawa kuomba ushauri ila umakini uwe mkubwa mtu asiombe ushauri kwa watu wasio sahihi badala ya kupona kupata utatuzi wakakutana na majeraha mengine
Tugeuze changamoto tunazokumbana nazo kua fursa muhimu sana za kutufanya tuwe makini zaidi, tujipange upya, tujirekebishe, tujisahihishe na kufanya vizuri zaidi mbeleni 🐒
Exactly 🐒
 
Kuna watu nilikuwa nawaamini sana na kila nikitaka kufanya jambo nilikuwa nawashirikisha sasa walijikuta wanajua kila kitu pasipo wao eti siwezi toboa. Saivi nimekuwa mtu wa kujiamlia mambo acha waninunie mara ooh we jamaa umekuwa mjanja wakati ndo tumekupokea mjini. Namshukuru Mungu mambo yangu yanaenda fresh tu tangu niache kuwashirikisha mambo yangu. Leo kuna jambo nilitaka nisikie ushauri wao kuhusu wazo la kufuga samaki acha wakosoe mara huwezi kufuga samaki wa ziwani ukiwa Dodoma haaaaaah.
 
Wewe umeshaelewa na unaajua cha kufanya hapo sina la kuongeza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…