Si kwa ajili ya ubaguzi, bali namshauri Rais Samia aepuke kufanya maamuzi makubwa ya muda mrefu yanayohusu upande wa Tanzania bara peke yake

Si kwa ajili ya ubaguzi, bali namshauri Rais Samia aepuke kufanya maamuzi makubwa ya muda mrefu yanayohusu upande wa Tanzania bara peke yake

Kwa nini mnapenda kuiita TANGANYIKA , Tanzania Bara? Mbona Zanzibar hamuiiti Tanzania Visiwani?

Ukiamua kutumia Tanzania Bara ku adress inshu za Tanganyika, basi na Upande wa Pili tumia jina Tanzania Visiwani badala ya Zanzibar.
Asante
Okay, you have a point there, I will grant you that. Ila pia ni kwa sababu serikali ya sasa kule haiitwi serikali ya Tanzania Visiwani, hatusikii raisi wa Tanzania Visiwani.
 
Na madai yote hayo yatamzuia raisi Samia, leo hi, kusema chimbeni madini ndani ya Serengeti, uamuzi ambao utakaa nasi huku Tanzania bara, kwa kipindi cha miaka 20-30 ijayo?

..umekosea tena, andika TANGANYIKA.

..Rais Samia yuko hapo kutokana na muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

..Naunga mkono jitihada zako za kupinga uchimbaji madini ktk mbuga ya Serengeti.
 
Yote haya yamesababishwa na katiba mbovu ambaye imetulazimisha makamu ambaye hatukumchagua kuwa rais.siku zote mtu ambaye hakuchaguliwa hawezi kuumia kuhusu ugawaji holela wa maliasili za taifa zaidi atagawa hovyo Kwa wageni kama anavyofanya na kuacha za kwao zanzibar.katiba yetu ilitungwa na vichaa.Nchi zote duniani rais akifariki makamu hurithi miezi mitatu,zingine minne,na zingine mwaka mmoja basi lakini sisi haieleweki yaani hata kama rais akiapishwa Leo na Bahati mbaya baada ya siku Moja akafariki eti makamu anapata mserereko wa urais.katiba ya hovyo sana
 
Okay, you have a point there, I will grant you that. Ila pia ni kwa sababu serikali ya sasa kule haiitwi serikali ya Tanzania Visiwani, hatusikii raisi wa Tanzania Visiwani.

..Ni kwasababu wananchi wa Zanzibar walikataa nchi yao kuitwa Tanzania Visiwani.

..Kilifanyika majaribio na jitihada za kufuta jina Zanzibar, na kuita Tanzania Visiwani, lakini zilikutana na upinzani.

..Kwa upande wa Tanganyika hatukusimama kidete kutetea utambulisho wetu, na ndio maana leo hii rasilimali za Tanganyika zimekuwa kama hazina wenyewe.
 
Okay, you have a point there, I will grant you that. Ila pia ni kwa sababu serikali ya sasa kule haiitwi serikali ya Tanzania Visiwani, hatusikii raisi wa Tanzania Visiwani.
Uko sahihi kaka. Nimerejea kwenye Katiba ya JMT sura ya kwanza, imeeleza kuwa, "Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania inapakana nayo"
 
Kwa nini mnapenda kuiita TANGANYIKA , Tanzania Bara? Mbona Zanzibar hamuiiti Tanzania Visiwani?

Ukiamua kutumia Tanzania Bara ku adress inshu za Tanganyika, basi na Upande wa Pili tumia jina Tanzania Visiwani badala ya Zanzibar.
Asante
Mkuu ile ni Nchi na inaotw Zanzibar na wala zio Tanzania Visiwani! Tanzania Visiwani ni kama Mafia n.k. na utaiita jina gani: "Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ama Jamhuri ya Watu wa Tanganyika"
 
Wale jamaa waliokuwa wanasitakufanya maamuzi wapewe mauwayao.
 
Mbona umekasirika hivyo?Twende polepole kwa lugha za kiungwana.
Anakasirika kusikia tu tunasema maamuzi kama ya bandari kwa DP World, kuchimba madini ndani ya Serengeti, Samia asiyafanye kwa sasa, bali yaje yafanywe na raisi kutoka bara kwa sababu impact yake iko zaidi upande wa bara, na kama ni makosa isije ikasemwa mtu wa Zanzibar alituponza. Huyo lazima ana wajomba kule uarabuni.
 
Najua kwamba Rais Samia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, lakini ni jambo lililo wazi kwamba yeye kama Rais wa Tanzania, maamuzi yake kwa zaidi ya 98% yanahusu upande wa Tanzania bara peke yake, kwa sababu upande wa Zanzibar wana raisi wao na serikali yao.

Katika hali kama hii, na ukizingatia kwamba Rais Samia anatokea upande wa Zanzibar, ningeshauri sana kwamba Rais Samia ajiepushe kufanya maamuzi makubwa ambayo ni ya muda mrefu (yana lock-in effect ya muda mrefu) upande wa bara peke yake. Kumekuwa na hisia zinazozidi kukua kwamba Rais Samia anafanya maamuzi ambayo baadaye yatakuwa na athari mbaya upande wa Tanzania bara, wakati yeye amemaliza muda wake na kurudi Zanzibar, na kuwaacha Watanzania bara wakisumbuliwa na matokeo ya maamuzi yake.

Mifano ya maamuzi ambayo Rais Samia anachukua juu ya mambo yanayohusu bara peke yake ni kama suala la mkataba wa bandari kwa DP Word ya Dubai, na hili la kuchimba madini ndani ya mbuga ya Serengeti na nyinginezo, ambapo, TANAPA, chombo cha utalii Tanzania bara, kilishalikataza sana.

Ingekuwa busara sana kama Rais Samia angeonyesha subira na kuacha maamuzi juu ya mambo makubwa kama hayo, yenye long term lock-in effect, yafanywe wakati Rais wa Tanzania ni mtu kutoka upande wa bara. Hii itasaidia kutokuza chuki na kutoa hofu upande wa bara kwamba Raisi Samia hafanyi mambo kwa manufaa ya watu wa bara, na labda ana ajenda ya siri.
Hoja za kibaguzi huwa hazitusaidii tukiwa taifa moja la Tanzania. Samia anaweza kuja kuwa rais bora kuliko wote watano waliomtangulia.

Watangulizi wake wameweka mazingira mazuri yenye kumuwezesha kufikiria kwenye ukuzaji wa uchumi peke yake.
 
Hatuongelei uraisi wa Samia ukilinganisha na maraisi wengine, tunaongelea specifically issues kama uamuzi wa kuchimba madini Serengeti. Unawahusu nini Zanzibar? Kwani Samia ni raisi wa Tanzania bara? Basi angalau awe anatafuta maoni ya wadau wa bara juu ya mambo makubwa kama haya. Sema ukweli, leo tukifanya referandum huku bara kama tuchimbe au tusichimbe madini Serengeti, unafikiri itapita?
 
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, elewa maana ya maneno 'Jamhuri ya Muungano'.
 
Huo Utanganyika feki unakuwa ukitengenezwa wakati wa urais wa mzenji lakini JPM alifanya madudu mengi tu na hakuna wa kumyooshea kidole kisa ni mtanganyika mwenzetu.

Tunashindwa kutenganisha hoja za kibaguzi na suala zima la rais kuwa mzenji.
 
..Tume ya Warioba ilifanyia kazi mapendekezo ya aina mbalimbali za muungano, na ikaja na pendekezo la serikali 3.
Hakuna Tume au Kamati iliyoundwa kuhusu muungano iliyokuja na pendekezo jingine zaidi ya serikali 3. Hakuna!
..sasa kama unapinga findings za Tume ya Warioba inabidi utueleze chanzo cha mapendekezo ya serikali moja ni nani, na utafiti ulifanyika lini, na waliwasilisha wapi mapendekezo yao.
Tume ya Mkandara iliyoundwa na SSH iilikatazwa isiangalie suala la Muungano kwasababu hata mwendawazimu hawezi kukwepa hoja ya S3. Hakuna utafiti unaoonyesha suluhu ni S2 AU S1. hakuna!

Siku Watanganyika watakapoamka hata hizo S3 hawatataka, watajiuliza ni kwa faida gani! just matter of time
 
Sasa Huku umepaita Tanzania bara alafu Kule umepaita Zanzibar, Sasa Tanzania visiwani ni ipi? Mbona mmoja kapoteza jina lake kati ya hao wawili?

Hii Ni Tanganyika wakubali wakatae.
 
Kaka watanganyIka wenzetu walimzunguka Rais ndiyo wanatuuza, wanatumaliza.

Yeye akistaafu atakwenda kizmkazi atatuachia magofu huku Tanganyika tuhangaike nayo na vitukuu vyetu.
 
Sasa kama watanganyika wamelala unategemea afanye nini zaidi ya kuuza kila kitu.
Ni kweli wamelala sana. Kitendo cha Watanganyika kudai serikali 3 ni sehemu ya usingizi pia.
Wanaotakiwa kudai serikali 3 ni Wazanzibar! Tanganyika haihitaji Zanzibar

Watanganyika kudai serikali 3 ni 'favor' kwa Wazanzibar! Tanganyika haihitaji Zanzibar
 
Hivi leo hii kati ya Tanzania bara na visiwani, nani ana mhitaji nani? Labda tuanzie hapo
 
..Ni kwasababu wananchi wa Zanzibar walikataa nchi yao kuitwa Tanzania Visiwani.

..Kilifanyika majaribio na jitihada za kufuta jina Zanzibar, na kuita Tanzania Visiwani, lakini zilikutana na upinzani.

..Kwa upande wa Tanganyika hatukusimama kidete kutetea utambulisho wetu, na ndio maana leo hii rasilimali za Tanganyika zimekuwa kama hazina wenyewe.
Na ndio maana Wazanzibar wale wale waliokataa jina Tanzania na hivi karibuni kukana Bungeni wanashinikiza sana iweke formula ya kugawana rasilimali za Tanzania kwa jina la JMT ambazo ni za Tanganyika.

Kauli hiyo ameitoa Balozi Amina S. A akimtaka Rais SSH aweke 'Fomula' ya kugawana rasilimali za Tanganyika.
Kuna ushahidi wa video hapa JF.

Rasilimali za Tanganyika hazina msimamzi wala hazina mwenyewe
 
Back
Top Bottom