Si kwa ajili ya ubaguzi, bali namshauri Rais Samia aepuke kufanya maamuzi makubwa ya muda mrefu yanayohusu upande wa Tanzania bara peke yake

Si kwa ajili ya ubaguzi, bali namshauri Rais Samia aepuke kufanya maamuzi makubwa ya muda mrefu yanayohusu upande wa Tanzania bara peke yake

Najua kwamba Rais Samia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, lakini ni jambo lililo wazi kwamba yeye kama Rais wa Tanzania, maamuzi yake kwa zaidi ya 98% yanahusu upande wa Tanzania bara peke yake, kwa sababu upande wa Zanzibar wana raisi wao na serikali yao.

Katika hali kama hii, na ukizingatia kwamba Rais Samia anatokea upande wa Zanzibar, ningeshauri sana kwamba Rais Samia ajiepushe kufanya maamuzi makubwa ambayo ni ya muda mrefu (yana lock-in effect ya muda mrefu) upande wa bara peke yake. Kumekuwa na hisia zinazozidi kukua kwamba Rais Samia anafanya maamuzi ambayo baadaye yatakuwa na athari mbaya upande wa Tanzania bara, wakati yeye amemaliza muda wake na kurudi Zanzibar, na kuwaacha Watanzania bara wakisumbuliwa na matokeo ya maamuzi yake.

Mifano ya maamuzi ambayo Rais Samia anachukua juu ya mambo yanayohusu bara peke yake ni kama suala la mkataba wa bandari kwa DP Word ya Dubai, na hili la kuchimba madini ndani ya mbuga ya Serengeti na nyinginezo, ambapo, TANAPA, chombo cha utalii Tanzania bara, kilishalikataza sana.

Ingekuwa busara sana kama Rais Samia angeonyesha subira na kuacha maamuzi juu ya mambo makubwa kama hayo, yenye long term lock-in effect, yafanywe wakati Rais wa Tanzania ni mtu kutoka upande wa bara. Hii itasaidia kutokuza chuki na kutoa hofu upande wa bara kwamba Raisi Samia hafanyi mambo kwa manufaa ya watu wa bara, na labda ana ajenda ya siri.
Yote maisha tu
 
Tunapaswa kuiona nafasi ya uraisi kama nafasi ambayo imetangazwa kwa ajili ya watu ku-apply wakiwa na qualifications kujaza nafasi hiyo, kama ambavyo tungetangaza nafasi ya kazi ya Director General wa kampuni fulani. Sifa au umaarufu au ushabiki tu wa kisiasa, mara nyingine bila hata elimu ya mambo ya uongozi, sheria au uchumi, zitaendelea kutupa maraisi wasio na uwezo katika nafasi hii na kututia katika janga la maamuzi yasiyofaa, yakiwa na athari za muda mrefu kwa taifa hili.

Naam mkuu

Kupitia hili tunaweza kupata genius wa mambo yote muhimu katika Taifa.

Ikumbukwe pia kiongozi mamlaka ya juu kabisa {Rais} akiwa na upeo mdg na mawazo finyu (kuishi leo tu) kama haya si ajabu hata watendaji wake kuwa na utendaji m'bovu hata walotimamu kufifia katika utendaji wao.

N.B Siasa inatuletea viongozi wabovu sana kiakili na kulitia aibu Taifa nyanja nyingi sana.
 
Kweli kabisa, na hili litawezekana pale tu vyama vya siasa vitaweka maslahi ya nchi mbele ya maslahi ya vyama vyao au mtu mmoja mmoja binafsi
 
Sasa kuna haja gani yakuwa raisi wa JMT kama asifanye maamuzi ?

hakuna maamuzi aliyofanya Samia ambayo hayakuwa na baraka ya watanganyika ndani, tuache kumsukumia mpira.
 
Back
Top Bottom