"Bila Dai yule dogo nina uhakika asingejulikana kokote. Bila Dai asingekuwa na maisha aliyonayo sasa"
Naona hapo juu unajipa nafasi ya Uungu sasa, Kwa kusema bila Dai una UHAKIKA asingejulikana popote
Vipi kuhusu Marioo bila nani asingefika hapo alipo, je vipi Jay melody? Kwahiyo sidhani kama uko sahihi kusema hivo, kwa sababu ana kipaji angefika tu japo kwa njia ingine kama wasanii wengine
Cha Kwanza ni kipaji tu, ata Diamond aliwekeza kwa sababu anaamini katika kipaji cha Harmonize na akaona hii ni hela hapo mbeleni ndomana akawekeza hela zake
Ukiwa na kipaji,nidhamu na kujituma mafanikio ni swala la muda Tu, ila utapitia njia gani kufikia mafaniko yako ndio huwezi kujua, kwahiyo Diamond ametumika kama Daraja Tu Ku unlock kipaji cha Harmonize
Ndomana huyo huyo Diamond kashindwa kumsaidia dada yake queen Dareen ili nayeye awe msanii mkubwa kama zuchu, jibu ni simple tu kwa sababu Hana kipaji ambacho kina Harmonize,Rayvany,Mboso,zuchu,D-voice wanavyo