TheForgotten Genious
JF-Expert Member
- Jan 18, 2014
- 2,087
- 3,156
Kumekuwa na wimbi kubwa la watu kujiua kwa namna tofautitofauti kutokana na changamoto za kimaisha, ndoa, kiuchumi nk.
Wengi tumekuwa tukisema "Ongeeni na watu" kuhusu matatizo ili pengine yatatuliwe, wanaamini kwamba wahanga hawawashirikishi watu wakati sivyo.
Watu wengi wanafanya maamuzi baada yakuwashirikisha watu wa karibu, ndugu, jamaa na marafiki pasipo msaada na yamkini katika hao wanaoshirikishwa wanakuwa ndio chanzo cha kuchochea maaumivu badala yakutatua.(Sio kwamba hawawashirikishi watu ila watu hawashirikishiki)
Mfano mtu ana matatizo ya kwenye ndoa yanayomtesa, anawashirikisha wazazi na ndugu wengine, badala ya kutatua tatizo wanaanza kuleta yakale ,"ohh tulikwambia hukusikia"na maneno mengine kama hayo.
Una rafiki unamshirikisha jambo ila anaishia kukwambia pole anaendelea na mishe zake na mkiachana wala hakufuatilii, na sio rafiki hata ndugu tu wanakaa kimya hata hawafuatilii,WATU WANASHIRIKISHWA ILA HAWATAKI KUSHIRIKISHIKA! Sasa unakuta mtu ni mwepesi,amekosa option,unafikiri atafanya nini kama sio kuchukua maamuzi magumu?.
Haya mtu anatatizo,ndugu badala yakujadili namna yakutatua tatizo wanaanza kujadili tatizo na maneno chungumzima hawajui namna gani lina muathiri kisaikolojia mhusika,litazame tatizo kwa ufupi kujua asili kisha tafuteni soultion yakulitatua na sio kuitisha vikao vyakukaa kujadili tatizo ni upungufu wa akili kichwani.
MAONI YANGU.
1). Watu wajifunze namna yakukabiliana na nyakati ngumu,wajifunze kitu inaitwa "EMOTION INTELLIGENCE ",usilipe nafasi tatizo liendeshe akili yako bali akili iwe na nafasi yakuliendesha tatizo lako.
2).Matatizo yako hususani yanayohusu madeni ni bora ukazungumza kinaga ubaga na wadeni wako na sio ndugu ama marafiki asilimia kubwa wanaishia kukuumiza tu, (japo si wote).
3).Usiumize kichwa sana kwa kitu ambacho umesha kielezea kwa mtu na hataki kuelewa muache afanye anachotaka maana yeye ndio mwenye maamuzi ya mwisho kwa wakati huo.
4).Usikubali kutoka kwenye focus ya kile unachokiamini na kukipambania kwa sababu ya changamoto unazokutana nazo,maana changamoto sio vitu bali ni watu wanaokuzunguka,wakabili.
5).Usiwe mtu wa rundo la watu wasio na msaada kwako hata kwa mawazo pevu,achana nao haraka.
6).Usipoteze muda kumfikiria mtu aliyegoma kukusaidia wakati anauwezo huo kwa asilimia nyingi,haitakusaidia maana kusaidiwa ni hiari ya mhusika na hailazimishwa.
7).Ifunze akili yako kuvumbua milinganyo mikubwa kwa utulivu.
8).Sio kila kitu chakuwashirikisha watu,maana wanaweza kukikuza wakati hakukuwa na ulazima huo,chuja.
9).Usimlazimishe mtu kukusaidia maana msaada ni hiari.
10).Usiwe mtumwa kwa mtu anayekudai au lah,,atakufanya mtumwa wa fikra.
Mimi nimechagua kuishi Kivyangu maana nitakufa kivyangu,na nina amini kama kuna mtu ataumia baada ya kifo changu ni Wanangu,Mama yangu na mke wangu kama atakuwa ananipenda kweli ,na baada ya kifo changu thamani yangu haitakuwa na utofauti na mzoga wa fisi hata kama nitazikwa kwenye jeneza la mamilioni,naisui kwa falsafa,mifumo na kanuni zangu.
Usipingane na nyakati utaathiri Hatima,zikubari nyakati
MTU AKISHINDWA KUNIELEWA HUWA NA ACHANA NAYE MAPEMA SANA.
MPASI N.A