Elius W Ndabila
JF-Expert Member
- Jul 17, 2019
- 339
- 678
KABLA YA 1992 TANZANIA TULIKUWA NA MFUMO WA VYAMA VINGI.
Na Elius Ndabila
0768239284
Ipo dhana inayojengeka kuwa mfumo wa vyama vingi nchini ulianza mwaka 1992 baada ya Tume ya Nyalali. Binafsi ninajaribu kuona kama dhana hii ina kinzani na historia halisi ya nchi yetu ambayo ni matokeo ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Mwaka 1992 ilikuwa ni kurejeshwa kwa vyama vingi na si kuanzishwa kwa Vyama vingi.
Hoja yangu inajikita kuanzia kwenye kuanzisha baraza la kutunga sheria chini ya Uingereza mwaka 1926.
Niwarejeshe nyuma kidogo, bunge la Tanganyika lilianzishwa tarehe 19/3/1926 chini ya gavana wa Kiingereza Donald na kupitisha sheria ya The Tanganyika (Legislative Council) Order in Council, 1926. Lakini kwa kipindi hicho halikujulikana kama bunge bali Baraza la kutunga sheria.
Wakati Baraza hili likitungwa Tanganyika ilikuwa chini ya uangalizi wa Uingereza. Idhini hii ilipewa na Umoja wa mataifa kwa kuisimamia Tanganyika mpaka ipate uhuru. Ninajaribu kusema haya ili baadaye tuje tuelewe dhana halisi ya mfumo wa vyama vingi nchini.
Ikumbukwe kuwa sheria hii ya kuanzisha baraza ilichapishwa ktk gazeti la serikali tr 18/6/1926. Baraza hili lilijulikana kama LEGCO, Baraza hili lilizinduliwa Disemba 7, 1926 DSM chini ya Gavana wa Uingereza ambaye kwa wakati huo alikuwa kama mwenyekiti wa Baraza Sir Donald Cameron. Baraza lilikuwa na wajumbe 20 wote wakiwa wameteuliwa na gavana.
Kumbuka hawa ndio tunawaita wabunge kwa sasa. Baraza hili likitunga sheria basi zilikuwa zinapelekwa Uingereza ya kupata idhini ya kuanza kutumika kama ambavyo leo sheria zikitungwa lazima ziende Ikulu kwa Mh Rais kusaini.
Mabadiliko yalianza kutokea mwaka 1953 baada ya gavana kuondolewa kuongoza baraza na nafasi yake kuchukuliwa na Spika Bregedia William Erick Halstead Sculphan ambaye aliapishwa novemba mosi 1953 kuwa spika wa kwanza. Hapa ndipo utaratibu ulianza kubadilika. Kwa mfano sheria zikitungwa zilikuwa haziendi tena Uingereza bali zilipelekwa kwa gavana aliyepo nchini.
*Historia inatueleza kuwa mwaka 1958 kwa mara ya kwanza baraza lilipata wajumbe wa kuchaguliwa. Yaani Uchaguzi ulifanyika. Wakati wa uchaguzi huu kulikuwa na vyama vitatu ambavyo viliingia kwenye mtanange huo. Vyama hivyo ni TANU(Tanganyika African National Union), UTP (United Tanganyika Party), na ANC(African National Congress).
Katika uchaguzi huu chama cha TANU pekee ndicho kilishinda na kushiriki kwenye LEGCO*. Kwa tafsiri hii unasemaje kuwa mfumo wa vyama vingi ulianzishwa 1992 wakati kumbukumbu zinatueleza wazi mwaka 1958 kulikuwa na uchaguzi wa vyama vitatu vikitafuta wajumbe wa Baraza(Wabunge)?
Neno baraza lilibadilika mwaka 1960 na kuitwa Bunge haya yote yakiwa ni maandalizi ya kuipatia Uhuru Tanganyika baada ya Hayati Baba wa Taifa na wenzake harakati zao kupamba moto za kudai uhuru. Kubadilisha jina kutoka Baraza na kuwa Bunge kulikuwa kunaandaa nafasi ya chombo hiki kusimamiwa na Tanganyika na kimpatia Rais kushika mamlaka aliyokuwa nayo Gavana.
Hivyo basi baada ya uhuru wa Tanganyika 1961 pamekuwa na mabadiliko makubwa mengine matatu ambayo ni Bunge kuwa na sura ya muungano 1964 baada ya Tanganyika na Zanzibar kuungana, Bunge kurejeshwa kuwa la chama kimoja mwaka 1965. Mfumo huu ulirrjeshwa ili kuipa nchi utulivu wa kuijenga. Tanganyika ilibaki na TANU na Zanzibar ilibaki na ASP. Ili kuongeza nguvu ya mashirikiano na kwa kuwa waliona malengo ya TANU na ASP yanafanana basi mwaka 1977 kwa makubaliano ya pamoja waliamua kuviunganisha vyama hivi na kuwa CCM.
Baada ya mabadiliko ya Dunia Tanzania ililazimika kurejesha mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini mwaka 1992 ambapo ulifanya bunge kuwa la vyama vingi mwaka 1995 ijapo Uchaguzi wa vyama vingi baada ya kurejeshwa ulifanyika mwaka 1994. Huu ulikuwa ni uchaguzi mdogo ambao ulifanyika Ileje na Kwimba (Kama nitakuwa sahihi). Kwa vipi vyote utaona kulikuwa na mabadiliko makubwa ya Wajumbe/ Wabunge kutoka 20 mwaka 1926 hadi 320+ kwa sasa.
Kwa mkutadha huu ninaomba niruhusu mjadala, je mfumo wa vyama vingi nchini ulianzishwa mwaka 1992 au Ulirejeshwa mwaka 1992?