Si lazima kila Ukweli usemwe, ukweli mwingine is FYE only! Uzalendo wa kweli ni pamoja kuwa na Kabbah, unahifadhi ukweli kifuani mwako, unakufa nao

Kosa ni la Kabendera au waliompa information?
 
Hii excuse haiwezi kumhusu Raisi muuaji, mbakaji, mporaji na mbaguzi kama Jiwe. Lazima vizazi vifahamishwe na vijifinze.

Mbona tunasoma na kifundishwa ukatili wa kina Iddi Amin, Hitler wengineo?
Analeta excuse zake za ajabu zisizo na mashiko. Huyu mzee amejaa majisifu na kujitukuza mara oohh sisi wasukuma na blaahh blaaahh kama hizi. Unapata kuona mtu na Degree zake mbili anaongea vitu havina mantiki bora huo muda wa kusoma hayo madegree angeenda VETA akajifunze ufundi ili akistaafu apate kazi ya kufanya na kuweka mwili na akili busy kuliko hii kazi ya UCHAWA.
 
Uzushi? Ukweli? Which is which? Pascal ameuita ukweli japo anadai haukupaswa kuwekwa public ili 'kuwalinda' walioandikwa kwenye kitabu husika, by the way no one is hundred percent sure kama yote yaliyomo ni ukweli au ni uongo so we give it probable chances 50/50.
Kitabu kingesomwa na watu wengi zaidi ila itambulike kuna ambao naturally si wasomaji wa vitabu lakini out of curiosity wanakitafuta ila si kila mtu ana-afford kukipata(kwa sasa) ndiyo maana kuna waja wanaulizia soft copy ya hicho kitabu.
Pasina kuwa na facts kama yaliyomo kwenye kitabu ni uzushi au la lazima uwe na facts zako vinginevyo nawe utakuwa ni muongo/mnafiki kwa kipinga bila ya kuwa na facts. Prove him wrong otherwise just let it flow.
 

Paskali unataka kusemaje .

Tatizo la Tanzania ni ufisadi .
Haiwezekani nchi yenye watu mil.65 kuwa na pato la Taifa dogo kiasi cha kushindwa kuwapa huduma bure watu wetu wachache wenye Matatizo ya figo .

Kama tunatoa milion kumi kwa goli moja halafu hatutaki ukweli usemwe basi tutakuwa wabaya kuliko viumbe wote waliowekwa duniani.

Ukweli unaitwa ukweli kwa sababu umejulikana ,usiojulikana basi hakuna jambo lolote . Siri ni huko chumbani kwako lakini kwenye masuala ya umma hakuna kuficha uovu.

Wasema ukweli wanamuwakilisha Mungu maana wanaweka kila uovu hadharani .

Yesu Masihi aliyekuja kujenga ufalme wa Mungu duniani alitufundisha kuwa wakati ukifika kila jambo liilofanyika gizani litawekwa nuruni. Na hakuna taa inayowashwa na kuwekwa chini ya uvungu bali huwekwa juu ya Mnara ili utumike mji wote.

Huyu Kristo ndiye Mfalme wa wafalme .Na hatutaogopa kusimamia tawala wa Mungu duniani maana ndiyo njia ya haki bila kujali maslahi ya watu wachache wapiga dili.
Tutofautishe maslahi ya Taifa na maslahi ya viongozi au watawala .
Siri za nchi zinakua kwenye majeshi sio kwenye siasa na wanasiasa.

Nikisikia mtu anatoa siri za Jeshi kwa kweli huyo nitapambana naye mchana na usiku ikiwezekana hata kumtafutia makazi mengine lakini haya mambo ya maadili ya familia za watawala na kujitafutia umaarufu na mali kwenye uongozi haya yanahitaji wao wenyewe kufungua kesi za madai au kujisafisha wao vinginevyo jamii itawakataa kwenye sanduku la kura .

Nchi iko salama kwa sababu wafu wanatunza siri za majeshi yetu kwa ujumla wake .
 
Naamini Pascal Mayalla Ni mkristu.
Kama ndiyo hivyo, asome ujumbe wa bwana wake Yesu Kristo. 👇

"Basi, msiwaogope, kwa maana hakuna neno lililositirika, ambalo halitafunuliwa; wala lililofichwa, ambalo halitajulikana."

Mathayo 10:26



Binafsi yangu:
=>Manufaa ya ukweli tija yake huwa Ni Kubwa (>90%)
=>Manufaa ya uongo tija yake Ni (<10%)
 
NUSU NAUNGA MKONO:
1. Mfano hai juu ya ndoa yako. Kwenye mahusiano mahali unapokubali ukweli na kuomba msamaha, ni pale umefumwa live au mwanamke kupata mimba nje ya mumewe na ushahidi uwe wazi. Kwamba mumewe amekuwa masomoni nk. Kile ulifanya kama angefanya mkeo (huenda naye alifanya kosa kama lako ila yeye akawa na kifua) pia hata wewe lingekutesa maisha yako yote. Mapenzi yanauma, yanauwa. Kisa chako kinafanana na kisa cha kweli cha jamaa mmoja. Hadi leo hali ni mbaya. 2. Kuhusu ukweli mwingine, baba acha usemwe hadharani. Raisi kama baba wa familia kama alizuia watoto kusema, watoto watasubiri aondoke na waseme yale aliyopitiwa na shetani. Kwa kuwa wewe ni mkristo unaamini ktk maandiko, Ona wafalme walipopitiwa na shetani maovu yao yalisemwa. Sulemani anaoa wanawake 700 na michepuko 300 yalisemwa. Daudi anazini na mke wa Uria na anamwua Uria kwa siri ilisemwa 2 SAMUEL 11:1-27. Sasa, wale waliojifanya malaika wa nuru kumbe ni... acha ukweli usemwe.
 
Imagine Kuna watu tunao katika hii nchi ambao kwa ukaribu wao na kiongozi wa juu wanajua Kama lisemwalo ni kweli au sio kweli lakini wapo kimyaa
 
Mkuu Pascal ahsante sana kwa bandiko lako zuri.

Kuna ukweli aina nyingi sana kulingana na mahali na mazingira na mtu anaeambiwa huo ukweli.

1.Ukweli mtupu hiyo nothing but the truth
2.Ukweli Nusu
3.Ukweli uliochanganyika (Controversial truth)

Sasa kwenye siasa na sehem kubwa ya maisha namna 2 na 3 ndizi hutumika.

Huyo Bwana anaeimbwa kwamba ni msema kweli, mara nyingi sana huwa anatumia namba 2 na mara nyingine uongo mtupu.

Hakuna political survivor aliedumu kwenye siasa miaka 20 akawa msema kweli... Ni porojo za kijinga tu.

Huyo mtu tunaomjua huwa anachagua side alafu anaamua kuichafua kwa kutengeneza maneno...

Lakini kuna mara anaropoka mambo ya ndani ya familia yake, hiyo sio kusema siri, hiyo ni immaturity.

Ahsante
 
Masihi alisema ambaye ndiye Mfalme wa wafalme .
Sisi ni nani hata tujaribu kuficha ukweli ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…