Si mmejifanya kumfukuza Pierre Lechantre kwa Majungu sasa Masoud Djuma laana inamuanzia huko Nakuru

Manji akiibuka anaye huyu. Tatizo la simba wajanjawajanja wako
wengi. Sisi kule mjanja wetu ni mzee Akilimali, akishushiwa gunia la viazi anatulia.
Umesema kweli Simba wajanja wajanja wengi,wapigaji tupu ,tuombe washinde la sivyo ht kagame watayumba
 
Umesema kweli Simba wajanja wajanja wengi,wapigaji tupu ,tuombe washinde la sivyo ht kagame watayumba
hawa simba ni balaa, wapigaji wao, mamende wao, wanunuzi wa mechi nao wamo, mwe!
 
Mleta Mada huwa ananifurahishaga sana,hapendi kbs kulea lea kitu ,safi sana

Ni kweli Mkuu na hivyo ndivyo nilivyo na sitobadilika. Simba SC tumefanya Kosa kubwa sana kama siyo mno kuachana na Kocha Mfaransa Pierre Lechantre kwa sababu za ' Kipumbavu / Hovyo Hovyo ' kabisa ambazo kwa Mtu ' very professional ' wa masuala ya mpira akiyasikia atastaajabu na kuushangaa Uongozi wa Simba SC.

Na ili muone kwamba ' impact ' ya Mzungu kutokuwepo tayari imeanza kuonekana angalieni jinsi Wachezaji wa Simba SC wanavyoonyesha ' nidhamu ' mbovu sana Uwanjani hali ambayo ulikuwa huwezi kuiona wakati Kocha Lechantre alipokuwa katika Benchi kwani Yeye alikuwa ni ' Non Nonsense Coach ' na Kwake ' nidhamu ' kwa Wachezaji wake ndiyo ilikuwa Kipaumbele chake.

Na Wachezaji wa Simba SC leo wanaonyesha ' nidhamu ' mbovu kwakuwa wanajua Kocha ' Mnafiki ' Masoud Djuma Irambona ni mwenzao, anawaogopa baadhi ya Wachezaji ' Waandamizi ' na wengi wao hula nae ' bata ' sana mitaani hivyo wanammudu vilivyo na Yeye hawezi kuwafanya lolote.

Nautizama mpira ' Kiufundi ' na siyo ' Kipuuzi ' kama wale Team Masoud Djuma Irambona walivyo na wanavyouona huu mpira. Kocha ' Mnafiki ' Masoud Djuma Irambona kuwa Kocha wa Timu kubwa kama ya Simba SC ni ' Kututukana ' Sisi ambao pengine tunaujua mpira wa ' Kisayansi ' zaidi kuliko hata Yeye.

Na ni huyu huyu ' Mnafiki ' Masoud Djuma Irambona ndiyo alimpikia ' Majungu ' Beki Mganda Juuko Murshid kwa Uongozi wa Simba SC ili aonekane mtovu wa nidhamu na asiwe anapangwa kisa tu Yeye ( Kocha Masoud ) ana urafiki mkubwa sana na Kiungo Jonas Mkude ambaye nae ana urafiki wa karibu sana na Mshkaji wake wa ' Kindakindaki ' Beki Yusuph Mlipili na kumpendelea kumpanga mara kwa mara na kumpuuza Beki Juuko Murshid ambaye hadi hivi sasa katika Timu ya Simba SC bado sijaona Beki wa kumweka Benchi Juuko ambaye panga pangua anapata namba katika Kikosi cha Timu ya Taifa ya Uganda ( The Cranes ) ambayo hata katika Viwango tu vya FIFA Uganda wametuacha Tanzania mbali sana.

Tufungwe tu leo na Gor Mahia mpaka tuheshimiane kudadadeki!!!!!!!
 
Big minds ignore tabula rasa

Halafu huwa siyo tabula rasa ni tabularaza ' Mpuuzi ' mkubwa Wewe. Ndiyo maana nakujibu hovyo kwani nimeshakusoma zamani sana Kichwani mwako kumejaa maji yale yanayopatikana sana katika yale ' Madimbwi ' saba ( 7 ) pale Mabibo.
 
Kwa aina ya mipango ambayo Simba wanaitaka Masoud hawezi kuwafikisha popote,hata wakishinda hii game wasiridhike

Mo afanye maamuzi magumu
Nakubaliana na sababu zako juu ya huyo kocha,ingawa wapo watakao kupinga
 
Hii game ya leo technically inawabeba Gor marhia..

Hivi kabisa Watu wa Simba SC mlijua kwa Kocha huyu ' Mnafiki ' Masoud Djuma Irambona Simba SC itaifunga Gor Mahia? Thubutu!

Hawa Gor Mahia nao wananiudhi na kunikera sana mbona hawatufungi magoli mengine? Nataka tufungwe kama goli 13 au 15 ili tuone sasa Mzungu Lechantre na Masoud Djuma nani ' Mwanamume ' na ' Fundi ' Kudadadeki.

Tufungwe tu leo hakuna namna!!!!!!!
 
Kwa aina ya mipango ambayo Simba wanaitaka Masoud hawezi kuwafikisha popote,hata wakishinda hii game wasiridhike

Mo afanye maamuzi magumu
Nakubaliana na sababu zako juu ya huyo kocha,ingawa wapo watakao kupinga

Anayejua mpira kama Wewe hawezi wala hawezi kunipinga ila wale ' Wapuuzi ' Team Masoud Djuma Irambona ndiyo watanipinga kwani hawajui mpira.

Asante Mungu Simba SC tumefungwa goli la pili muda si mrefu uliopita. Laana ya Kocha Pierre Lechantre inazidi kutuingia tu wana Simba SC.

Na bado!!!!!!!!
 
Halafu huwa siyo tabula rasa ni tabularaza ' Mpuuzi ' mkubwa Wewe. Ndiyo maana nakujibu hovyo kwani nimeshakusoma zamani sana Kichwani mwako kumejaa maji yale yanayopatikana sana katika yale ' Madimbwi ' saba ( 7 ) pale Mabibo.
Watu wanaokimbilia kutukana sana huwa wana Matatizo ya kifamilia..sikushangai mkuu.. Endelea kutumia matusi kama defense mechanism
 
the real definiton of shabiki maandazi
 
Mkuu namalizia kumsikiliza Didier Lacoste na kibao chake "Kingongolo" nirudi kwenye uzi wako mmmmmmhhh hizi wine huenda zimeingilia nerves za fahamu[emoji6]
 
Leo unawakataa wanyama wako siyo?Blackberryyyyyy
 
Watu wanaokimbilia kutukana sana huwa wana Matatizo ya kifamilia..sikushangai mkuu.. Endelea kutumia matusi kama defense mechanism

Mbona safari hii umeandika kwa nidhamu sana? Hopeless Wewe ulitaka unizoee hovyo na umekuja Kwangu Kichwa Kichwa na umevuna ulichokipanda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…