Si mmejifanya kumfukuza Pierre Lechantre kwa Majungu sasa Masoud Djuma laana inamuanzia huko Nakuru

Si mmejifanya kumfukuza Pierre Lechantre kwa Majungu sasa Masoud Djuma laana inamuanzia huko Nakuru

Nashukuru kwa kunielewa Mkuu. Na nilionya hadi nikaanzisha ' Uzi ' hapa hapa JF wa kumtaka Mo Dewji asiingie ' mkenge ' na kuwasajili akina Adam Salamba wa Lipuli FC na Marcel Kaheza wa Maji Maji kwakuwa nilishaona uwezo wao ni mdogo na kwa Simba SC Wachezaji hao hawatufai bado kuna ' Wapuuzi ' na ' Wajinga ' fulani wachache hawakunielewa ila nadhani sasa kwa aina ya Viwango vyao walivyovionyesha huko Nakuru nchini Kenya ndipo watajua kwamba GENTAMYCINE nina ' jicho ' kali na la ' Kiufundi ' zaidi na huwa sikosei na sijawahi kukosea kwa kile ninachokiamini.

Mpira umemalizika na tumefungwa goli 2 kwa 0. Safi sana na bakini na huyo ' Mnafiki ' wenu Kocha Masoud Djuma Irambona. Namkumbuka sana Kocha wangu Pierre Lechantre niliyemkubali na niliyemwona ndiye angetukomboa Simba SC hasa Kimataifa na kushindana na akina TP Mazembe, Al Ahly, Mamelodi Sundown na akina Enyimba.

Kipigo hiki kiwe ' Fundisho ' Kwetu Simba SC na tuache ' Professionalism ' ifanya Kazi yake huku tukiacha ' Uswahili ' wetu.
GENTAMYCINE wewe ni mchawi katika soka nimekuvulia kofia,huweki ushabiki mbele ila unachambua na kutafakari kila hatua inayopitia timu. wewe ni zaidi ya katibu mkuu wa simba.
pia suala la professionalism leo nimeliona. huyu kocha wa kogelo ni Kerr ambaye tulimtimua kwa aibu akiwa simba lakini leo hii anabeba ndoo ya pili ya sportpesa,kawapa ubingwa wa ligi na timu ipo makundi bila shaka watapita wao na USM Algier katika kundi lao. Kerr huyu huyu anaipeleka robo fainali ya caf gor mahia wakati kwetu simba tulimuona hafai.
mpira wetu wa mdomoni kamwe hatutaendelea.
 
Nashukuru kwa kunielewa Mkuu. Na nilionya hadi nikaanzisha ' Uzi ' hapa hapa JF wa kumtaka Mo Dewji asiingie ' mkenge ' na kuwasajili akina Adam Salamba wa Lipuli FC na Marcel Kaheza wa Maji Maji kwakuwa nilishaona uwezo wao ni mdogo na kwa Simba SC Wachezaji hao hawatufai bado kuna ' Wapuuzi ' na ' Wajinga ' fulani wachache hawakunielewa ila nadhani sasa kwa aina ya Viwango vyao walivyovionyesha huko Nakuru nchini Kenya ndipo watajua kwamba GENTAMYCINE nina ' jicho ' kali na la ' Kiufundi ' zaidi na huwa sikosei na sijawahi kukosea kwa kile ninachokiamini.

Mpira umemalizika na tumefungwa goli 2 kwa 0. Safi sana na bakini na huyo ' Mnafiki ' wenu Kocha Masoud Djuma Irambona. Namkumbuka sana Kocha wangu Pierre Lechantre niliyemkubali na niliyemwona ndiye angetukomboa Simba SC hasa Kimataifa na kushindana na akina TP Mazembe, Al Ahly, Mamelodi Sundown na akina Enyimba.

Kipigo hiki kiwe ' Fundisho ' Kwetu Simba SC na tuache ' Professionalism ' ifanya Kazi yake huku tukiacha ' Uswahili ' wetu.
Mkuu kwanini tusimchukue yule kijana Elias Maguli?
 
Mkuu Kaheza, Salamba na Mo aliyetoka Prisons bora kina Mavugo
Hata mimi nakuunga mkono, nilisikia tetesi kuwa SC watamchukua Elias Maguli katika usajili wao, mara nasikia ooh hapana Adam Salamba ni zaidi ya hao wakina Maguli na wengine kisa tu Salamba aliifunga Simba huu kweli ushabiki mandazi na usajili uchwara.
 
Hata kama alikuwa anataka alipwe hiyo 43 Million Shillings nadhani kwa uwezo wake mkubwa alikuwa anastahili. Tofauti na wengi Mimi huyu Kocha nimemfuatilia kote alikopita na niseme tu kwamba kama kulikuwa na Kipindi ambacho Simba SC tulipata bahati na tumeichezea ya kumpata Kocha mzuri ambaye angetusaidia na kutupeleka mbali basi alikuwa ni huyu Mzungu Mfaransa Pierre Lechantre. Nimeumia na nimesikitika sana kwa Yeye Kufukuzwa au Kuachwa kama vile hakuna alichotufanyia Kizuri na cha kutusaidia.

Tufungwe tu leo na Gor Mahia ili tuheshimiane kudadadeki!!!!!!!
Bora wangemuacha baada ya mashindano kwisha.

Halafu unaenda kwenye mashindano unaawacha wachezaji muhimu kama Okwi,Bocco,Kotei etc, inakuwaje?
 
Tatizo nyie mikia mshazoea kufukuza makocha, sasa sijui mnamtaka kocha wa namba gani... Maanacsiku zote naona kiwango ni kilekile..
Sasa nawauliza umnamtaka kocha gani na mcheze kiwango gn ambacho mnauona mlishawahi kuwa nacho..?
 
MKUU ,KWAKWELI TOKA ULE UZI WAKO WAJUZI NAONA MAMBO YANAZIDI KUPINDA.

LEO NINAHASIRA KINYAMA...HUYU MSENGE MASUDI ANA MAJUNGU...NAHAJAWAH HATA KUIFADISHA TIMU..***** ZAKE.

TUMEPOTEZA EXPOSURE ISOKUJA KUSAHAULIKA YANI
 
Uongozi wa Simba hauna malengo kabisa ya kimataifa, hivi kweli salamba uyu kweli wakusajiliwa simba, mechi ya leo bora pale mbele wangemuweka mavugo uyo salamba hajui hata anachotakiwa kufanya pale
 
Kocha Mzungu hajafukuzwa, ni kwamba mkataba wake aliosaini kuitumikia Simba sc, imekwishwa.
Alisaini mkataba wa kuitumikia Simba sc kwa miezi sita tu.
Nayo imeisha.
Sasa mwenzetu nani kakuambia kuwa amefukuzwa ?
Majungu sio mazuri.
 
Na kama Kocha akibaki huyu huyu ' Mpuuzi ' wenu na ' Mnafiki ' Masoud Djuma Irambona sahauni kupata mafanikio mnayoyataka. Ni Kakocha ' Kapumbavu ' halafu nakachukia kweli kwakuwa ndiye Mtu mwenye ' Majungu ' ndani ya Timu huku akiwagawa mno Wachezaji na bahati mbaya sana Uongozi wa Simba SC unamlea.
Sawa mkuu, tumepata pa kuanzia na sidhani kama Mo dewji atakuwa na mambo ya kiswahili kuelekea kwenye mabadiliko makubwa ya club yetu pendwa..ushauri nini kifanyike kwa kuwa bado Lechantre yupo hapo hapo dsm akisubiri huruma ya Mo dewji, hatutaki kurudi kule tulipotoka awali!
 
Funfact: Tokea mashindano ya sportpesa cup yaanze mwaka 2017 simba haijawahi kufunga hata goli moja ndani ya dk 90..
 
Back
Top Bottom