Si niliwaambia msioe? Hebu tujiulize haya juu ya DED Mafia na Mkewe

Si niliwaambia msioe? Hebu tujiulize haya juu ya DED Mafia na Mkewe

Liverpool VPN

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2020
Posts
6,958
Reaction score
16,358
INTRODUCTION:
Nawasalimu kwa jina la muungano wa Tanzania...!!

BODY
Tarehe 18/04 Mtukufu Rais wetu alitengua uteuzi wa DED wa Mafia Bwana Kassim Seif Ndumbo, ila wajuzi wa mambo wanasema, kosa alilonalo ni kashfa ya kubaka binti (minor) ambae alikuwa "House girl" wake.

SCENARIO
Ila Mimi kwenye hii kesi/kashfa nina maswali yafuatayo...

1. Mkewe DED ndiye aliyeishikilia kidete kesi hii. Kwamba aliamua kuchagua upande wa binti na kumchomo mumewe mwenye hela.

2. Taarifa zinasema "Binti alikataa hela alizoletewa na polisi ili akaushe asiseme popote" Ila usisahau hapo kabla, binti na DED walikua na uhusiano..!! NI TAARIFA TU LAKINI.

3. Ni mwanaume gani anayepata mshahara wa LSSE 1, posho kibao, safari za kikazi kibao ila akaamua kwenda ku"date" na kabinti akaacha wanawake kibao ambao kwa status yake HAWEZI KUWAKOSA?

4. Kama binti na DED walikuwa na uhusiano, inakuaje keo Binti akatae pesa za bwana ake?

5. Inakuaje binti awe na uhusiano na DED halafu leo achoke ghafla aende kumshtaki DED polisi?

CONCLUSION
Anyway tuachie polisi wafanye kazi yao. Ila usisahau kwenye hii kesi mtoa taarifa mkuu ni MKE WA DED..!!

Na hizi ndio NDOA ZENU.

Endeleeni kushupaza shingo na KUOA.

Mwenzenu kakomaa na uchawa akapata uteuzi, leo hii uteuzi wake unatenguliwa na taarifa/kashfa kutoka kwa MKEWE..!!!

Pia soma: Mkurugenzi aliyetenguliwa Mafia, kuchunguzwa kwa Ubakaji
 
Kuna maswali umeyahoji hadi mtu anajiuliza "is he really serious!!!"
Yaani kama sio nyie ambao huwa mnashadadia ujinga wa kuwabaka house girls humu. Mambo yakiwageukia ndio mnajua wapo mabinti wa "status zenu".

Haki itendeke, safi sana mke kasimama kama mama.
 
Kusingiziwa huwa kupo na hatuombei kutokee, lakini hakuna kitu kibaya kama kujichanganya mwenyewe afu udakwe na ushahidi juu

Hapo hata kama ulijisahau tu hakuna rangi utakayoacha kuona na mbaya zaidi kama mtu alikuwa anakutafutia rada kitambo tu afu umeingia kwenye kumi na nane zake
 
Kuna maswali umeyahoji hadi mtu anajiuliza "is he really serious!!!"
Yaani kama sio nyie ambao huwa mnashadadia ujinga wa kuwabaka house girls humu. Mambo yakiwageukia ndio mnajua wapo mabinti wa "status zenu".

Haki itendeke, safi sana mke kasimama kama mama.
Nani kakwambia kuwa DED kabaka.
What if ni hujuma za Bint na Mama Vs DED?

Ni mashaka na yanayoendelea huko kwenye NDOA YAO.

Huu ni mgogoro wa ndoa.

#YNWA
 
DED unaishi na binti wa miaka 16 kama mfanyakazi wako sio umri wa kuwa shule huu??

Swali langu la kwanza hili mimi kujiuliza.

La pili wawe na mahusiano yaani hata miaka 18 bado binti awe na mahusiano na boss wake tena mteule wa rais.

HAPANA KUNA SHETANI HAPA KATI.
 
Unajuaje huyo DED katika uhusiano wake na huyo binti hakumtishia asiseme wala asimwambie mkewe?
Lakini hata kisheria haiwezi kumsaidia huyo DED kwa sababu bint yuko chini ya umri wa miaka 18.
Ushauri,Polisi wa Mafia wasihusike kupeleleza na kuendesha hiyo Kesi watapotosha ushahidi,waletwe wa kutoka Makao makuu Dodoma.
 
Mkuu umenishangaza sana, kwahiyo ulitaka mke afunike kombe DED aendelee kujilia dada wa kazi?
Tayari mke alikuwa na sababu ya kufanya hivyo kwa hasira na maumivu ya kusalitiwa tena kwa mtu ambae wanaishi nae.

Itoshe kusema ndoa sio kichaka cha kufichia maovu/waovu, haki itendeke hawa mabeki tatu wanadhalilishwa sana kuna nyumba unakuta kaliwa kuanzia na baba mpaka last born.

Kataa ndoa isikufanye ushindwe kuona hata uovu uliotendeka.
 
Umeandika mawazo yangu, nashukuru nimepitia kwanza kabla sijaandika maana umesema kila kitu.
Hii post imekupa heshima yangu.
 
Mkuu umenishangaza sana, kwahiyo ulitaka mke afunike kombe DED aendelee kujilia dada wa kazi?
Tayari mke alikuwa na sababu ya kufanya hivyo kwa hasira na maumivu ya kusalitiwa tena kwa mtu ambae wanaishi nae.

Itoshe kusema ndoa sio kichaka cha kufichia maovu/waovu, haki itendeke hawa mabeki tatu wanadhalilishwa sana kuna nyumba unakuta kaliwa kuanzia na baba mpaka last born.

Kataa ndoa isikufanye ushindwe kuona hata uovu uliotendeka.
Ni kweli kabisa; mabinti wengi wa kazi wamekuwa abused na baba na vijana wa familia. Na wengine wanaishia kuambukizana gonjwa familia nzima.

Hawa mabinti wa kazi karibia wote wanatoka kwenye familia zisizojiweza; wapo hapo kwa ajili ya kutafuta kipato kwa ajili ya kusaidia familia zao. Kuna hatma za familia zao wamezibeba wao kupitia kazi hiyohiyo. Badala ya nyie kuwatreat kama mabinti zenu; mnawalazimisha kuwa wake zenu kinguvu. Mwanaume anayeshindwa kumuheshimu binti wa kazi ambaye ni sawa na binti yake; sitoshangaa kusikia amelala na mabinti zake wa kuwazaa; hapo ndugu wa kike wa mke ndiyo weka mbali kabisa. It's so despicable

Hela mnazo, si mkatafute makahaba wenzenu huko nje; ukaharibu maisha ya binti wa watu, kisa kimshahara chako cha 50k?? Apandacho mtu; ndicho atakachovuna
 
All in all hii case jamaa ana chomoa mapema tu hakuna rape za kijinga hivi ..wanao fungwa kwa rape huwa wame jitakia tu kwa hawa police wetu na watoa ushahidi wa kibongo .kuchomoa ni rahisi kama una kunywa maji
 
Back
Top Bottom