Si sahihi kuwaita watumishi wezi kwani wanaotoa sadaka hutoa kwa hiari yao bila kulazimishwa

Si sahihi kuwaita watumishi wezi kwani wanaotoa sadaka hutoa kwa hiari yao bila kulazimishwa

Mganguzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2022
Posts
1,604
Reaction score
3,715
Mimi nikiwa mkristo huru na ninaeheshimu haki na uhuru wa watu kuabudu ! Kutoa sadaka kwa mujibu wa Imani zao kwa hiari yao bila kulazimishwa na mtu yeyote ,kwenda kuhudhuria makongamano na mikutano mikubwa na midogo kwa hiari yao bila kulazimishwa na mtu yeyote nipo kinyume na dhana ya kuwaita watumishi Hawa au wachungaji Hawa au mitume na manabii kuwa ni wezi ni uongo na upotoshaji mkubwa!

Dhana ya kudhani waumini hawana akili za kufikili au kudhani Hawa waumini ni maskini au wasio na elimu ni uongo pia! Kwenye makongamano haya na mikutano hii na ibada hizi wanaohudhuria ni maelfu ya watu! Wakiwemo wanasiasa ,maprofesa ! Ma doctor viongozi wa juu wa serikali na watu wa ulinzi na usalama ! Sio vichaa na si kweli kwamba hawana akili ! Pesa wanazotoa ni pesa zao halali na wanatoa kwa hiyari yao kama vile mtu anapoamua kutoa pesa ,ama kuhonga au kulewa na ama kununua magari ya kifahari huwezi kumwambia aliyehongwa ni mwizi au muuza bar ni mwizi au muuza magari ni mwizi!

Pesa iliyotolewa ni halali kwa kuwa aliyetoa ametoa katika mapato yake ! Iweje umuone kwamba anaibiwa wakati sio pesa zako ni zake ? Na ametoa akiwa hajalewa Wala kulazimishwa?? Mwandishi wa gazeti mwananchi ,anaitumia kalamu yake vibaya! Kwa hiyo ameona jarida la mwananchi ndio uwanja pekee wa Kutukana, kukashifu na kudhalilisha watumishi wa Mungu na Imani za watu bila kuwataja waliotapeli na waliotapeliwa!

Namfahamu mwandishi huyu hana adabu kabisa pale anapotaja jambo linalohusiana na ukristo ! Kila mtu akiamua kutumia kalamu kuandika maovu ya kufikirika na kuchafua Imani za wengine kwa maneno ya kebehi na dhihaka nchi yetu haitakuwa salama Tena! Kwenye hiyo mikutano inayomuumiza kichwa Rajabu ni uamsho wa watu kuanza kusilimu na kuukimbilia ukristo kwa Kasi kubwa ! Uwingi wa watu wanaohudhuria kwenye mikutano hii kama ule wa juzi pale kawe kwa mwamposa akina Rajabu na wenzao wanalala matumbo joto !

Sasa hata wahariri wa gazeti wamejikuta kwenye mkenge huu kukosa contenti na kuanza kuvurumisha kashfa kwa watumishi wa Mungu ! Wewe mwandishi achana na Imani isiyokuhusu simamiq Imani yako ! Kama unaona wanaoenda kwenye makanisa wanaibiwa zile ni pesa zao na wanatoa kwa hiyari hakuna anayewalazimisha kuzitoa! Na kama wamekwambia wanaibiwa waelekeze waende misikitini ambako hawataibiwa!

Watu kwa sasa wameamka sio wajinga Tena ! Kama ulivyochapisha habari za makakasisi kuwa ni matapeli ndivyo uchapishe na habari za mashekhe wanaowauzia watu mafuta na madawa ya kisuna na mapete ya bahati naliomba gazeti la mwananchi litoke hadharani na kuwataja wachungaji matapeli kwa ushahidi na kuwapeleka mahakamani kinyume chake tutalifungulia mashtaka hili gazeti kwa kupotosha umma na kutumika kuchafua na kudhalilisha Imani za watu wengine badala yake wawaombe radhi watumishi waliojaribu kuwahusianisha na porojo hizi kupitia gazeti la Mwananchi.
 
Ndgu haribu basi kufuata alama za uandishi ili walau bandiko lako lisomeke kirahisi.

Hakuna aya, nukta wala mkato ni viulizo na kuserereka mwanzo mwisho.
Hata huyu Rajabu atashindwa kusoma ajue makosa yake.
 
Hawa ni mangumaru ambao wanatoa laki tano kumuona tapeli mmoja huko

USSR
 
Gazeti la Mwananchi liko sahihi, haiwezekani waumini wawe wanakamuliwa fedha kuliko "kausha damu" makanisani.
Hizo pesa wanazokamuliwa uliwasaidia kutafuta au ni umaskini unakuwasha mwilini ,pesa yangu unanipangiaje matumizi
 
Hawa ni mangumaru ambao wanatoa laki tano kumuona tapeli mmoja huko

USSR
Wewe ambae sio ngumbaru una nini? Nyie si ndio mnashinda sinza kutafuta madada poa pesa yote inaishia hapo si ni Bora hata hawa wanaombewa kwa sadaka
 
Kwani hao waliotajwa ni Kina Nani..?

Ni Vizuri tukiwq na mifano halisi ...

Watu Wanatajirika kuipitia Sadaka tunawaona hivi hivi... !

Wakati tunafundishwa tajiri ni ngumu kuuona Ufalme Wa Mungu...Hatutaki tuwaache Siku ya Mwisho hao manabii....!
 
Hapana utajiri ni akili ya mtu na kuwa mtumishi au kuwa kiongozi haimaanishi uwe maskini ! Watumishi wengi wa zamani walikuwa matajiri wakubwa ni Leo tu tunaona ajabu mtumishi kuwa tajiri
 
Mimi ni mkristo ila gazeti la mwananchi linafakazi nzuri wezi , matapeli na majambazi wa madhabahuni wote lazima wamulikwe

USSR
Umekosa kazi za kufanya tafuta kazi utaacha kuona wivu kwa pesa za watu
 
Mleta uzi ni mfano halisi wa msemo 'jiwe limetupwa gizani ukisikia mtu analia jua limempata'

Pole sana
 
Ndgu haribu basi kufuata alama za uandishi ili walau bandiko lako lisomeke kirahisi.

Hakuna aya, nukta wala mkato ni viulizo na kuserereka mwanzo mwisho.
Hata huyu Rajabu atashindwa kusoma ajue makosa yake.
Alama unazozitafuta weka wewe
 
Mleta uzi ni mfano halisi wa msemo 'jiwe limetupwa gizani ukisikia mtu analia jua limempata'

Pole sana
Mbona nyinyi akiguswa mtu mmoja wa kwenu nchi inasimama
 
Back
Top Bottom