Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Matuga ni kijana kutoka kijijini, alianza hustle zake baada ya kumaliza darasa la 12. Aliuza mazao na kuweka pesa mpaka alipofanikiwa kupata nauli na hela kidogo ya kujikimu alikwenda Afrika ya Kusini. Bahati nzuri aliongea Kiingereza cha kueleweka shukran imwendee kiongozi wake wa dini kwani aliwafunza na kuongea na vijana kwa lugha ya Malkia.
Alikua na kama $500 ilimtosha kukaa katika nyumba za wageni za bei rahisi na alifanikiwa kupata kazi ya kuuza duka. Alikua mwaminifu sana dukani kiasi ambacho mwajiri wake alimuamini katika mambo mengi. Mwajiri alikua mwanasiasa mwenyeji ambae hakuamini vijana wa Kizulu. Alimpa Matuga servants quarter na chakula alikula cha nyumbani. Matuga aliweka kila hela akiyoipata na baada ya miaka mitatu alikua na mtaji aliopangia kuufanyia biashara.
Alirudi Tanzania na kuanza kuchukua bidhaa Kariakoo nyingi kutoka China na kupeleka vijijini. Vitu kama jiko la mafuta ya taa, kwa kijijini linawekwa kwa dharura kama kuna mgeni au mvua kubwa imenyesha na hakuna kuni za kupikia. Alipeleka pia taa za battery, viatu hata na shuka. Kutoka kijijini alipeleka maharage na nafaka Kariakoo.
Uchumi wake ulikua vizuri sasa alianza kutafuta mke wa kuoa. Alirudi kijijini na kuwashirisha wazazi wake katika swala hili. Katika mchujo pale kijijini alipatikana Davina mtoto wa Mkatekista, mama Matuga alimsifu kwa kazi na ukarimu hasa wanapokwenda kusali jumuia kwao ni lazima awatengee chai na viazi vitamu au mihogo baada ya sala. Baba Matuga alimsifia kwa uhodari wake wa kuongoza sala hasa baba yake akiwa amepata majukumu.
Hatua za posa zilikamilika ingawa Davina alikua bado mwanafunzi katika shule ya sekondari ya kata. Matuga alimpa pesa ya kujikimu na vitu vingine alivyohitaji. Davina alipendeza kuliko wasichana wengi.
Kijijini kwao hakukua na bomba la maji, maji walichota kijiji cha jirani katika kisima cha mdundiko kilichojengwa kwa hisani ya serikali ya Denmark. Akiwa kidato cha nne Davina alikwenda kuchota maji jioni ili ampunguzie mama yake majukumu ya kesho yake yeye akiwa shule. Davina akiwa anarudi nyumbani alibakwa na mtu asiyemfahamu.
Ilikua huzuni kubwa kijijini, baba yake alifanikiwa kumpeleka polisi na hospital kwa pikipiki aliyonunuliwa na Matuga. Hospital walimpatia Post-exposure prophylaxis (PEP).
Baada ya mwezi mmoja Davina aligundua ni mja mzito na ni matokeo ya kubakia. Habari hizi zilimfikia Matuga na kwa masikitiko hata wazazi wake walimshauri aachane na Davina. Davina alilia sana hasa kukatishiwa safari yake ya masomo. Matuga alishangaza wengi kwa kutangaza ndoa na Davina. Harusi ilikua kubwa na kujijini kila mtu alikula pilau na wali pia na soda.