Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Wakiwa na rasilimali chache sana, Zanzibar wamegundua ili waweze kuendelea haraka ni vizuri waachane na akili za ki Tanzania Bara.
Sisi tukiwa tunaendekeza ujinga eti uraia pacha utahatarisha usalama wao siku nyingi walishapitisha suala la Diaspora kushiriki kuwa sehemu ya uchumi wa nchi yao.
Tukiwa tunaendekeza ujinga sijui wageni wasiruhisiwe kumiliki ardhi wao siku nyingi walishapitisha suala la wageni kumiliki ardhi na matunda yameanza kuonekana kwenye uchumi wao.
Kwa sasa ukitazama kwa makini kwenye kila kitu Zanzibar wanafanya kwa viwango vya juu sana.
Sisi tukiwa tunapiga lopolopo kujenga miji ya kisasa na makazi bora kwa wananchi, Zanzibar wameanza kutumia fedha wanazopata kuboresha makazi ya wananchi wao kwa kuwajengea nyumba bora kwenye maeneo yaliyopangwa na kujengwa vizuri.
Kinachonifurahisha zaidi Zanzibar hawana madini, hawana gesi, hawana Mbuga za wanyama ila wameamua kutumia akili kufanya mambo ya maana ambayo yanawapa fedha na wanazitumia vizuri.
Kwa hali ilivyo haitazidi miaka 20 Zanzibar itaenda kuwa kama Singapore au Korea Kusini. Nina uhakika baada ya miaka 20 ijayo Tanzania bara tutaenda kujifunza Zanzibar kuhusu namna ya kutumia akili kuvutia mitaji na kufanya maendeleo sahihi na kwa haraka.