Wakiwa na rasilimali chache sana, Zanzibar wamegundua ili waweze kuendelea haraka ni vizuri waachane na akili za ki Tanzania Bara.
Sisi tukiwa tunaendekeza ujinga eti uraia pacha utahatarisha usalama wao siku nyingi walishapitisha suala la Diaspora kushiriki kuwa sehemu ya uchumi wa nchi yao.
Tukiwa tunaendekeza ujinga sijui wageni wasiruhisiwe kumiliki ardhi wao siku nyingi walishapitisha suala la wageni kumiliki ardhi na matunda yameanza kuonekana kwenye uchumi wao.
Kwa sasa ukitazama kwa makini kwenye kila kitu Zanzibar wanafanya kwa viwango vya juu sana.
Sisi tukiwa tunapiga lopolopo kujenga miji ya kisasa na makazi bora kwa wananchi, Zanzibar wameanza kutumia fedha wanazopata kuboresha makazi ya wananchi wao kwa kuwajengea nyumba bora kwenye maeneo yaliyopangwa na kujengwa vizuri.
Kinachonifurahisha zaidi Zanzibar hawana madini, hawana gesi, hawana Mbuga za wanyama ila wameamua kutumia akili kufanya mambo ya maana ambayo yanawapa fedha na wanazitumia vizuri.
Kwa hali ilivyo haitazidi miaka 20 Zanzibar itaenda kuwa kama Singapore au Korea Kusini. Nina uhakika baada ya miaka 20 ijayo Tanzania bara tutaenda kujifunza Zanzibar kuhusu namna ya kutumia akili kuvutia mitaji na kufanya maendeleo sahihi na kwa haraka.
View attachment 3195947View attachment 3195948View attachment 3195949View attachment 3195950
Zanzibar hii ambayo wanaagiza nyanya chungu, nyanya, vitunguu na ,vizazi mbatata kutoka bara???🤣🤣🤣🤣🤣 .
Majengo yasikutishe, wametumia nafasi ya mama kuwa kiongozi wa Nchi.
Mama anastahili pongezi bkwa kutumia nafasi yake vizuri.Kama tunaangalia zaidi!! Majengo, tumajengo ni wivu wa kijinga sana.
Kifupi hatuna la kujifunza Toka Zanzibar,kupitia Muungano, Zanzibar tumeitawala ,tumewanyonya sana.
Miradi ya maendeleo ya Zanzibar mikubwa ni sahihi kabisa!!
Natamani kama Mama Abdul atashinda, japo sitaki itokee afanye mambo makubwa zaidi, kwa sababu nafasi ndio sasa!!!
Hongera sana Mama Abdul kwa kuchota pesa kupeleka maendeleo Zanzibar.
Kabla ya uchaguzi mkuu fanya hivi Mama.
1.Teua Jaji Mkuu mzanzibari,
2.DG TISS, mzanzibari,
3.IGP Mzanzibari
4. Kamishna General Uhamihaji mzanzibari
5.Kamishna Mkuu TRA Mzanzibari
6.Governor BOT Mzanzibari
....
Mama endelea kupiga kwenye mshono!!!
Mpaka , mama zamu ni Yako, mama nguvu ni zako, mama ufalme ni wako.
Mwisho mwishoni mteue BAMBO NA AFANDE sele, au Muhogo mchungu awe mbunge na mmoja awe mjumbe wa bodi ya utalii TANZANIA.
Ni hayo tu, hongera sana kwa kazi na kwa kukupigia mwingi Zanzibar!!!🤣🚴🚴🙏