Siamini kama bwawa la "stigler gorge" litamaliza tatizo la mgao wa umeme nchini

Siamini kama bwawa la "stigler gorge" litamaliza tatizo la mgao wa umeme nchini

Tulikuwa na rais kichaa ambaye aliwahi kutamka hadharani kuwa "mmi sishauriki, ten ukinishauri ndiyo unaharibu kabisa"

Huyu ndiye aliyeanza kumwaga mipesa kwenye mradi uliopitwa na zama wa kuzalisha umeme kwa maji. Mama anaingia madarakani tayari mipesa mingi imefukiwa pale. Anachofanya mama ni kuendelea kuimwaga mipesa ili walau turudishe hata 1 ya 10 ya mipesa iliyomwagwa pale.

Lkn kiukweli kwa mabadiliko ya tabia nchi yaliyoikumba dunia kujenga bwawa ni ushamba, upumbavu na kupoteza fedha. Dunia imehama huko hivi Sasa, ipo kwenye solar energy,, wind energy, geothermal energy, wave energy na nuclear energy.
Akili nnnyaaa
 
Wote tunajua bwawa hili linatumia maji ya mto/mito kama yalivyo mabwawa mengine tuliyo nayo hapa nchini.

Na kutokana na tatizo la mvua kwenye mabwawa yaliyopo tumekua tukiambiwa uzalishaji umeme umepungua kwasababu mvua zimepungua hivyo tujiandae kwa mgao.

Swali la kujiuliza ni hili..

Kwa uwepo wa mabadiliko ya tabia ya nchi na kutokana na ukweli kwamba bwawa la "stigler gorge" nalo linategemea mito/mvua je siku mvua zikipungua hatutakua na tatizo la mgao wa umeme?

NB: Hapa ninapoandika hii posti TANESCO wamekata umeme na simu ina 8% tu.
Bwawa moja haliwezi kumaliza matatizo

Mahitaji yetu Pia yanaongezeka kila kukicha

Lakini litasadia kupunguza matatizo
 
Acha ujinga basi hivi uchawa unawasaidia nini nyie mbuzi? sasa kosa la Magufuli ni nini pale kwenye lile bwana?

Mtu ameanzisha kitu kizuri halafu mnashindwa kupaform kwenye implementation halafu unaenda kumlaumu marehemu bila hatia mtu ameshajifia.
JPM alichukiwa na ataendelea kusemwa vibaya na watu wote wenye elements za Ufisadi !!
Hiyo inafahamika vizuri !
 
Umejenga hoja kijinga kweli. Hujafikiria kwamba nchi nyingi zinaathiriwa na jiografia. Sayansi gani unayo kichwani kwa kichekesho hiki ulichoandika??

Mm nilidhani unakuja na hoja za kisayansinkuoneaha udhaifu wa nishati ya solar na wind. Kumbe unaandika upuuzi.
Nchi za kiarabu zikonjangwani kwanini hawazalishi umeme WA jua na upepo,,tatizo kubwa ni initial costs na running costs za mitambo
 
Wat wanasema mabadiliko ya Tabia nchi kwamba mvua hazitakuwepo..Kam mvua hazitakuwepo basi tujiandae kufa Kwa njaaa.Lakini kama.majira yatabadilika mara mvua zinyeshe kipindi ch akiangazi badala ya masika..bado bwawa litakuwa na maji.Harfu kumbukeni tunagesi au jus lakini unajua unahitaji ekari ngapi za kufunga mitambo ya jua.Kumbuka kuvuma megawat 300 yajua unahitaki hecta zisizopungu elf 10.
umeme wa gas kuzalisha mega wat miatatu unahitaji mitambo yenye thamani ya billion 800 hadi 900 na bado running cost..Maana yake kuzalisha mega watt 2100 ni fedha nyingi sana
 
Litamaliza kama wahusika wakitaka iwe hivyo, ila kama ni mfumo uleule wa dili halitamaliza
Mfumo wa dili ndiyo tatizo wala siyo maji ya bwawa. Kwanza ukitaka kujua kwamba hilo bwawa halitakuja kulissaidia Taifa angalia mkandarasi aliyepewa hilo jukumu. Hana experience nzuri au stahiki ya kufanya kazi hiyo. Visingizio anavyotoa vya kuchelewesha ni vya kukosa "proper planning". Pili mitambo iliyofungwa pale ni chakavu, ya tangu miaka ya 80 (nineteen eighties) unategemea nini? Ikiweza kufanya kazi mfululizo kwa miaka sita itakuwa bahati na kwa gharama kubwa sana. Mark my words for reference in the future!
 
Wote tunajua bwawa hili linatumia maji ya mto/mito kama yalivyo mabwawa mengine tuliyo nayo hapa nchini.

Na kutokana na tatizo la mvua kwenye mabwawa yaliyopo tumekua tukiambiwa uzalishaji umeme umepungua kwasababu mvua zimepungua hivyo tujiandae kwa mgao.

Swali la kujiuliza ni hili..

Kwa uwepo wa mabadiliko ya tabia ya nchi na kutokana na ukweli kwamba bwawa la "stigler gorge" nalo linategemea mito/mvua je siku mvua zikipungua hatutakua na tatizo la mgao wa umeme?

NB: Hapa ninapoandika hii posti TANESCO wamekata umeme na simu ina 8% tu.
Hilo Mimi Ninavyo ona ni mawazo mazuri kutumia pia maji ya mvua kuzalishia umeme kuliko kuyaacha yaende yakajaze bahari bila kuyatumia
Wasiwasi wangu ni kuungana nawe
Kua mabwawa hayo si suluhisho la kudumu kutokana na mazingira yaliyopo
Mabwawa
 
Hayo mabwawa manne yapo katika ukanda mmoja
Ukanda wa kusini Dodoma Mbeya Iringa Morogoro na Pwani
Mtera. Kidatu. Kihansi. Na Julius Nyerere yenye uwezo wa kutoa mw 2579
Ikitokea ukanda huo ukapungukiwa na mvua nchi ina kumbwa na uhaba wa umeme
Hivi sasa kuna tatizo linayo ikumba dunia mabadiliko ya tabia nchi
Kutegemea mitambo inayo tegemea mvua itatugharimu huko mbele ya safari
Vyanzo hivyo Kwa kua ni enderevu vinapata malighafi (maji) kila mwaka vitumike kama mbadala wa kupunguza matumizi mitambo ya gas na mafuta Kwa kua Mali gafi hiyo ina mwisho na ina gharama kuioata
Pia tusisahau ku angalia vyanzo vingine vya asili upepo jua joto ardhi mawimbi nk
 
Ukisikia mradi wa serikali ukipambwa na vibwagizo vya 'unakwenda kumaliza tatizo fulani', fanya mambo yako usipoteze muda. Haijalishi ukubwa wa mradi wenyewe. Sijui huwa kuna ulazima gani wa kutumia lugha sweeping kuuza miradi Kwa umma.
 
Narudia tena kusema.
Bwawa la nyerere hata likitoa umeme wa kutosha kiasigani.
Huo umeme una wenyewe kwa lengo na kuhamisha malighafi zetu. Labda kwa wana nchi wataingiza mw200 tu. Subilini muone.
 
Narudia tena kusema.
Bwawa la nyerere hata likitoa umeme wa kutosha kiasigani.
Huo umeme una wenyewe kwa lengo na kuhamisha malighafi zetu. Labda kwa wana nchi wataingiza mw200 tu. Subilini muone.
Daah
 
Mfumo wa dili ndiyo tatizo wala siyo maji ya bwawa. Kwanza ukitaka kujua kwamba hilo bwawa halitakuja kulissaidia Taifa angalia mkandarasi aliyepewa hilo jukumu. Hana experience nzuri au stahiki ya kufanya kazi hiyo. Visingizio anavyotoa vya kuchelewesha ni vya kukosa "proper planning". Pili mitambo iliyofungwa pale ni chakavu, ya tangu miaka ya 80 (nineteen eighties) unategemea nini? Ikiweza kufanya kazi mfululizo kwa miaka sita itakuwa bahati na kwa gharama kubwa sana. Mark my words for reference in the future!
Nilikuwa nasikiliza clip a Mbunge machachari Mh. Mpina leo nikakumbuka comment ya mwezi Januari kuhusu hili bwawa la kufua umeme lililopewa Arab Contrators kutoka Misri!
 
Wote tunajua bwawa hili linatumia maji ya mto/mito kama yalivyo mabwawa mengine tuliyo nayo hapa nchini.

Na kutokana na tatizo la mvua kwenye mabwawa yaliyopo tumekua tukiambiwa uzalishaji umeme umepungua kwasababu mvua zimepungua hivyo tujiandae kwa mgao.

Swali la kujiuliza ni hili..

Kwa uwepo wa mabadiliko ya tabia ya nchi na kutokana na ukweli kwamba bwawa la "stigler gorge" nalo linategemea mito/mvua je siku mvua zikipungua hatutakua na tatizo la mgao wa umeme?

NB: Hapa ninapoandika hii posti TANESCO wamekata umeme na simu ina 8% tu.
Ingekua negative…. Thread ingekua page 2022

ILA kwasababu mna Ona changes, mko poa

Bladifakin
 
Naona kuna kamdudu kananing'inia kwenye nyaya, kazi yake ni kukata umeme. Mpaka kaondolewe kwa maombi.
 
Back
Top Bottom