Siamini katika biashara yoyote ile ya kushirikiana na mtu

Siamini katika biashara yoyote ile ya kushirikiana na mtu

TEAM 666

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2017
Posts
4,399
Reaction score
8,594
Kuna Jamaa anataka nimpe mtaji wa pesa kama laki3 anataka kuanzisha kibanda cha kuuza mafuta ya petrol na Oil lkn kila nikiiangalia hiii biashara faida yake ndogo sana

Lita moja filling station inauzwa 2,440 kwa Dungu LA Lita 20 jumla 48,800

Ukija kuuza mtaani bei ya Lita moja 2,700 kwahiyo kila Lita moja unapata faida ya 260

Ukiweka mtaji wa 244,000 sawa na mdungu 5 ya petrol unapata faida ya Tsh 26,000 ghalama ya usafili Tsh 10,000 kwa madungu 5

Kwahiyo mdungu 5 yakichukua siku3 na jamaa akila 2000 kila ck ndani ya siku izo 3 inakua 6,000 mtaji wa 244,000 nisubiri faida ya 10, 000 Alf tupo 2 sote tugawane hiyohiyo pesa na jamaa anaweza mwanzo akawa muaminifu lkn mwisho wa siku akiona biashara imesimama antaanza usanii

Kiukweli nahitaji sana michango yenu wana jamvi

Nahitaji maoni yenu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usife moyo kwa paper work nakusihi uijaribu wazo la biashara yako sokoni japo kwa madumu 2 uone mzunguko wa biashara.
Maana biashara nyingi zinafaida ndogo sana tena unakuta 50/- au 100/- mkuu kikubwa ni mzunguko tuu.
Halafu mnapo anza mtenge pesa ya matumizi binafsi mbali na pesa ya mtaji na faida hadi biashara itakapo anza jitegemea.
Kumbuka ni bora kuthubutu kuliko kutothubutu
 
Wewe si mtu mzuri unawadanganya wenzio

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usidanganywe mkuu,

Hii Biashara inawalipa vijana sana, tena faida yake ni 50%

Iko hivi,

Kijana anakusanya Chupa nyingi za plastic tupu za Lita 1 za maji.

Anaenda sheli na kuwaambia kua kila chupa wapime ya 2,000

ie: Inakua imepelea kidogo sana ujazo kufika Lita 1 kamili ambayo inauzwa 2300

Akifika mtaani,
Anauza kila chupa sh.3,000, faida yake 1,000

Sasa kwa haraka haraka,
Ukiletewa lile chupa, huwez gundua kua haujafika Lita 1.

Utatia kwenye chombo yako utaondoka na Utajihisi hamna faida.

Kumbe kiuhalisia,
Kapiga faida kwa 50%

****MJINI SHULE***

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ushauri wangu kwako ni "USIANGALIE SANA BIASHARA KWA NJIA YA KITABU!". Fanya kumuamini huyo rafiki/jamaa yako mpe hiyo hela aizungushe!.
By the way yeye ndio atahustle kukutafutia faida, utakacho risk kwake ni fedha yako tu hata muda wako hautaupoteza kwenye hiyo biashara!..
 
Usife moyo kwa paper work nakusihi uijaribu wazo la biashara yako sokoni japo kwa madumu 2 uone mzunguko wa biashara.
Maana biashara nyingi zinafaida ndogo sana tena unakuta 50/- au 100/- mkuu kikubwa ni mzunguko tuu.
Halafu mnapo anza mtenge pesa ya matumizi binafsi mbali na pesa ya mtaji na faida hadi biashara itakapo anza jitegemea.
Kumbuka ni bora kuthubutu kuliko kutothubutu
Hilo ni kweli,

Mfano:
1. Kreti moja ya Soda za Pepsi inauzwa 10,000 ikiwa na soda 24.
Maana ake kila soda ameinunua sh.416
Wakati Bei Soda Mtaani ni sh.500

KiUHALISIA,
Faida yake ni sh. 84 kwa kila chupa ya soda atakayouza.

2. Mkanda wa vocha 10 za Jero, Anauziwa na Wakala mkuu sh.4800.

Akiuza zote zikaisha anapata 5,000

Maana ake Kila vocha anakula faida sh.20

My Take:
Vijana acheni kupenda shortcut, Na hizo Biashara zenu za Kwenye Vitabu.

Hizo faida mnazo ona nyie ni ndogo.

Ndizo matajiri kila siku wanazikimbilia na Kufungua Biashara kila Siku.

Na ndizo zinazowaweka mjini Matajiri wakubwa wenye mahoteli, Baa,Nightclubs,Kumbi za Mikutano, Supermarket, shopping Malls n.k

Kikubwa Wanachoangalia Kwao ni Mzunguko wa Mzigo

SHAURI YENU

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi hapa kwenye kibada cha unga na mafuta ya rejareja ili nifikishe faida ya 15000 natakiwa nifanye mauzo ya sh. 450000. Maana kuna vitu vinafaida ya sh. 20 hadi 50. Na ndio vinatoka. Na hapo nimeingia dukani saa1:kamili asubuhi hadi saa 5 usiku. Sasa wewe hiyo unadharau na haufanyi wewe. Cha msingi fanya utafiti wa mzunguko ndio utaona kama unalipa au hapana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi hapa kwenye kibada cha unga na mafuta ya rejareja ili nifikishe faida ya 15000 natakiwa nifanye mavuzi ya sh. 450000. Maana kuna vitu vinafaida ya sh. 20 hadi 50. Na ndio vinatoka. Na hapo nimeingia dukani saa1:kamili asubuhi hadi saa 5 usiku. Sasa wewe hiyo unadharau na haufanyi wewe. Cha msingi fanya utafiti wa mzunguko ndio utaona kama unalipa au hapana

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu kuna neno hapo juu inaonesha huwa unalitumia sana mpaka ukiandika MAUZO hilo neno linajitype!
 
Ndugu huo mchanganuo ni nzr kila kitu ni taratibu, mtaanza na 5 baada mtakuwa mnafanya zaidi ya 10. Uoni faida itakuwa ni kubwa utarudisha mtaji wako
 
Hilo ni kweli,

Mfano:
1. Kreti moja ya Soda za Pepsi inauzwa 10,000 ikiwa na soda 24.
Maana ake kila soda ameinunua sh.416
Wakati Bei Soda Mtaani ni sh.500

KiUHALISIA,
Faida yake ni sh. 84 kwa kila chupa ya soda atakayouza.

2. Mkanda wa vocha 10 za Jero, Anauziwa na Wakala mkuu sh.4800.

Akiuza zote zikaisha anapata 5,000

Maana ake Kila vocha anakula faida sh.20

My Take:
Vijana acheni kupenda shortcut, Na hizo Biashara zenu za Kwenye Vitabu.

Hizo faida mnazo ona nyie ni ndogo.

Ndizo matajiri kila siku wanazikimbilia na Kufungua Biashara kila Siku.

Na ndizo zinazowaweka mjini Matajiri wakubwa wenye mahoteli, Baa,Nightclubs,Kumbi za Mikutano, Supermarket, shopping Malls n.k

Kikubwa Wanachoangalia Kwao ni Mzunguko wa Mzigo

SHAURI YENU

Sent using Jamii Forums mobile app
Am blessed bro

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom