Siamini katika biashara yoyote ile ya kushirikiana na mtu

Siamini katika biashara yoyote ile ya kushirikiana na mtu

Biashara ipi nzuri zaidi ya hiyo unataka kwa mtaji wa 300k.?

Angalia mzunguko wa hiyo biashara, ukitulia hutoamini. Fanya Mkuu hutojuta!

Ingawa ni kweli Partnership Business ni changamoto hasa kwa mtaji mdogo kama huo.
 
Hilo ni kweli,

Mfano:
1. Kreti moja ya Soda za Pepsi inauzwa 10,000 ikiwa na soda 24.
Maana ake kila soda ameinunua sh.416
Wakati Bei Soda Mtaani ni sh.500

KiUHALISIA,
Faida yake ni sh. 84 kwa kila chupa ya soda atakayouza.

2. Mkanda wa vocha 10 za Jero, Anauziwa na Wakala mkuu sh.4800.

Akiuza zote zikaisha anapata 5,000

Maana ake Kila vocha anakula faida sh.20

My Take:
Vijana acheni kupenda shortcut, Na hizo Biashara zenu za Kwenye Vitabu.

Hizo faida mnazo ona nyie ni ndogo.

Ndizo matajiri kila siku wanazikimbilia na Kufungua Biashara kila Siku.

Na ndizo zinazowaweka mjini Matajiri wakubwa wenye mahoteli, Baa,Nightclubs,Kumbi za Mikutano, Supermarket, shopping Malls n.k

Kikubwa Wanachoangalia Kwao ni Mzunguko wa Mzigo

SHAURI YENU

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama ulikuwa na mimi nilitaka ni mshauri hiv hiv asante mkuu umeniwakilisha vema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo biashara nikidogo sana. Hamuwezi Fanya partnership, kama wewe unafanya Fanya, kama unamsaidia mdogo wako afanye msaidie. Napenda nikukumbushe hivi kila biashara huwa INA boom time ikikubali mzunguko wake inalipa vibaya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usidanganywe mkuu,

Hii Biashara inawalipa vijana sana, tena faida yake ni 50%

Iko hivi,

Kijana anakusanya Chupa nyingi za plastic tupu za Lita 1 za maji.

Anaenda sheli na kuwaambia kua kila chupa wapime ya 2,000

ie: Inakua imepelea kidogo sana ujazo kufika Lita 1 kamili ambayo inauzwa 2300

Akifika mtaani,
Anauza kila chupa sh.3,000, faida yake 1,000

Sasa kwa haraka haraka,
Ukiletewa lile chupa, huwez gundua kua haujafika Lita 1.

Utatia kwenye chombo yako utaondoka na Utajihisi hamna faida.

Kumbe kiuhalisia,
Kapiga faida kwa 50%

****MJINI SHULE***

Sent using Jamii Forums mobile app
Ina maana mkuu, hao vijana wanaenda petrol station na makopo hayo ya maji ili wapiwe hayo mafuta ya buku mbilimbill kwa kila kopo? Kwamba kama anataka lita 20 basi anaenda na makopo 20 petrol station na kuyapimia mafuta ya buku 2?
...mkuu kama ulimaanisha hivyo, basi unataka kulisha watu tangopori!
 
Wengine wanaenda nayo, Wengine hawaendi nayo.

Hao ambao Unaona hawaendi Nayo, Wanafanya hivi.

Yaani
Kwa Mara kwanza Anaenda na Kopo,

Akishawekewa mafuta ya 2000, Analichora alama yalipoishia hayo mafuta ya 2000

Na hicho ndio kinakua kipimo chake cha Siku zote.

Baada ya hapo anakua anaenda na Madumu.

Akishafika chemba,
Anachukua kipimo chake na kupima hayo mafuta ya 2000 na kujaza kwenye machupa.

Hahaha kashindwa kujiongeza kama ni paper ana ziro

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo biashara nikidogo sana. Hamuwezi Fanya partnership, kama wewe unafanya Fanya, kama unamsaidia mdogo wako afanye msaidie. Napenda nikukumbushe hivi kila biashara huwa INA boom time ikikubali mzunguko wake inalipa vibaya.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ya mkuu ww umenielewa sana yani

Kwamchanganuo huo kwa partnership ningumu kutoboa lazm kutakua nakuangushana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wengine wanaenda nayo, Wengine hawaendi nayo.

Hao ambao Unaona hawaendi Nayo, Wanafanya hivi.

Yaani
Kwa Mara kwanza Anaenda na Kopo,

Akishawekewa mafuta ya 2000, Analichora alama yalipoishia hayo mafuta ya 2000

Na hicho ndio kinakua kipimo chake cha Siku zote.

Baada ya hapo anakua anaenda na Madumu.

Akishafika chemba,
Anachukua kipimo chake na kupima hayo mafuta ya 2000 na kujaza kwenye machupa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli nimeamini biashara bila dhuluma hufanikiwi hapa bongo. Yani lazima kuwe na chembechembe ya usanii na kuumizana!
 
Kweli nimeamini biashara bila dhuluma hufanikiwi hapa bongo. Yani lazima kuwe na chembechembe ya usanii na kuumizana!
Kwanini umesema hivo,

Hiyo Inaitwa kufa kufaana mkuu.

Huna pa kukwepa,
Hata wenye sheli, kuna wengine wanajaza upepo kwanza kabla mafuta hayajaingia.

Dawa yao,
Nenda Sheli na Measuring Cylinder.

Na wakikuona umekuja Nayo, Mafuta hawakuuzii.

Akili Kumkichwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli nimeamini biashara bila dhuluma hufanikiwi hapa bongo. Yani lazima kuwe na chembechembe ya usanii na kuumizana!

Sio bongo tu ni dunia nzima unapoona kuna loopholes, wajanja wanafanya yao. Hata Amazon, google, ebay, Facebook, apple, Starbuck, wametumia hizo tactics, strategies kufika hapo walipo. Mbinu nyingi sana unaweza kutumia

The tech giants will never pay their fair share of taxes – unless we make them | David Pegg
https://www.theguardian.com/technol...017/oct/04/facebook-uk-corporation-tax-profit.
 
Hii biashara ilkuwa na faida enzi za kikwete. Kipind mafta yanauzwa 1600. Mitaani ilikuwa 2000. Ni kipind ni 2000 mitaan ilkuwa 2500. Sasa hiv kila m2 anaenda kununua kwenye filling station. 200 ni nying sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila unaamini katika ushirika wa kuitana wawili watatu muende mkanywe pombe etc
 
mkuu biashara huanza kwenye daftari kwa kuangalia gharama zote na kuangalia kipatikanacho. ukiona kipatikanacho ni kikubwa ni jambo jema sana ila ikiwa gharama nazo ni kubwa ibakiayo ni ndogo ambayo ukiangalia haikupi unaangalia nini uongeze maana hata hizo biashara za vocha na soda usizani watu wanazifanya peke yake wanakuwa na bidhaa nyingine ambazo ukichanga zote kufika jioni panakuwa na kitu flani

ikiwa katika hiyo biashara ya mafuta hamna biashara nyingine unaweza kuweka hapo kusaidiana na hiyo ya mafuta bora ukae kando ama ufanye peke yako maana kiuhalisia huo mgao utamchosha mtu na hapo ndo ataanza kukpiga panga zito atachukua mzigo wake binafsi na atachukua wa jumla atauza wake kwanza ukiisha ndo atauza wa pamoja,

kikubwa tafuta bidhaa nyingine kama oil za kulainisha vipuri, mafuata ya breki, grees na vitu vingine vinavyoendana ili kupandisha kipata , na hapo ndo mnaweza fanyakazi pamoja
 
Back
Top Bottom