Siasa chafu na dhulma zinapojitokeza; ni nini tufanye?

Siasa chafu na dhulma zinapojitokeza; ni nini tufanye?

Azizi Mussa

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2012
Posts
9,199
Reaction score
7,562
Kuna matukio mengi mabaya ambayo yanajitokeza katika siasa za Tanzania ambayo pamoja na ukweli kuwa yanasababishwa na watu; mimi na wewe pengine hatuna uwezo wa kuyazuia yasitokee.Mengine yanahusisha siasa chafu, mengine dhulma kwa watu wengine n.k

Katika mazingira ambayo yanatokea mambo mabaya bila kujali kiwango cha ubaya wake au anayeyafanya, tunapaswa kujiuliza maswali haya; Je! Ningeweza kuzuia jambo baya lililotokea, linalotokea au linalotaka kutokea lisitokee? Kama jibu ni ndio, basi fanya unachoweza kuzuia lisitokee hata kama utashindwa; lakini wewe utakuwa ni shujaa uliyetimiza wajibu wako.

Kama ukipata jibu kwamba jambo/mambo yaliyo au yanayotokea huna uwezo wa kuyafanya yasitokee; uamuzi bora zaidi ni kuamua kuangalia uzuri uliojificha kwenye jambo hilo baya linalotokea na kuuchukua uzuri huo kisha kuufania kazi. Ikumbukwe hata jambo liwe baya kiasi gani, ndani yake lazima kutakuwa na ka - uzuri flani ambako ukikatambua na kukatumia vizuri; kanaweza kusadia baadae na kutengeneza uwezekano wa jambo kubwa zuri kuibuka.

Katika nchi zilizofanikiwa kwenye mambo mbali mbali, huangalia Zaidi uzuri uliojificha katika ubaya badala ya kuangalia ubaya wenyewe, ubora uliojificha katika mapungufu na uwezekano uliojificha katikati ya changamoto. Kwa upande wetu bado hatujajijengea uwezo huu wa kujifunza kutoka kwenye mambo mabaya au makosa yanayotokea.

Katika muktadha wa mada hii; nitatoa mfano halisia, na uzuri tunaoweza kuupata ndani ya jambo baya.

Miaka kadhaa iliyopita, Waliibuka wanasiasa wakadai mzee Lowasa ni mtu mbaya sana asiyefaa kabisa.Walipoulizwa watoe ushahidi shida yake nini, wakawa hawatoi bali wanasisitiza tu kuwa ikibidi inafaa apigwe mawe. Kwa vyovyote vile hilo lilimwathiri sana mzee wa watu ila akaamua kuvumilia. Mwishowe waliomchafua wakampa nafasi ya kugombea urais; nafasi yenye heshima ya juu sana. Mada hii hailengi kujadili undani wa suala hilo na yatokanayo, bali kuonesha jinsi linavyoweza kutokea jambo baya ambalo wewe au mimi hatuwezi kulidhibiti ila tunaweza kujifunza vitu vya msingi ndani yake.

Ijapokuwa hili lilikuwa ni jambo baya sana ila ndani yake kuna uzuri flani. Uzuri huo ni kujifunza mambo kadhaa ya msingi ambayo kama tukiyazingatia na kuyafanyia kazi yatakuwa na faida kubwa.

Kwanza, tunajifunza kwamba usimfanyie ubaya mtu mwingine bila sababu za msingi na bila kujali ni nani; vinginevyo kuna siku ubaya ulioufanya utakurudia kwa namna ambayo hukuifikiria na kukugharimu kwa kiasi usichokitarajia.

Pili, Hata kama mtu anakufanyia ubaya; usi ‘Over react’ shungulika naye kwa kadiri ambayo utadhibiti ubaya anaoufanya usilete madhara au asiendelee kuleta madhara ila ujiepushe usije ukamdhuru hata kama una uwezo wa kufanya hivyo, ispokuwa tu kama kuna ‘Ulazima’ wa kufanya hivyo na hakuna njia mbadala. Hii ni kwa sababu adui yako wa leo, kesho anaweza kubadilika na kukusaidia kwenye jambo kubwa sana au kuwa rafiki. Na

Tuwe makini na mambo tunayosema hasa kuhusu ubaya wa watu wengine maana ipo siku yataturudi na kutuharibu kabisa.

Mfano huu nilioutoa ni mmoja tu ila mifano iko mingi na hata sasa kuna matukio yanatokea ambayo sio mazuri . Bila kujali mfanyaji ni nani na kwa nini, tuwe tunajiuliza, kilichotokea au kinachotokea; mimi na wewe tuna uwezo wa kukifanya kisitokee? Kama hatuwezi, hata kama ni kibaya kiasi gani, inashauriwa kutotumia muda mwingi sana kulalamika bali kuona ndani ya ubaya huo tunaweza kujifunza nini kizuri na kukifanyia kazi.

Kwa kufanya hivyo, haitatumalizia changamoto zilizopo na zinazoendelea kujitokeza lakini angalau tutapata matokeo bora zaidi kuliko kuamua kinyume chake.
 
Sasa mbona kichwa cha habari hakiendani na maelezo yako ya ndani!
 
Sasa mbona kichwa cha habari hakiendani na maelezo yako ya ndani!
sory, nimeandika haraka haraka nilikuwa sija edit vizuri.
Kwa muhtasari ninachosema, tumetawaliwa na utamaduni wa siasa chafu na wakati mwingine matukio ya dhulma. Lakini kwa bahati mbaya ni kwamba mara nyingi mambo hayo hutokea katika mazingira ambayo mimi na wewe hatuwezi kuyazuia,sasa ni nini cha kufanya? ndio msingi wa mjadala.
 
Mimi nimemuelewa sana pale alipomtaja Lowassa na waliompa ridhaa ya kugombea urais. Nia yake ni kuwananga CHADEMA maana ndo mtaji wenyewe siku hizi.
Usiwe na mtizamo mfupi kiasi hicho. Huo ni mfano tu ili kuelezea hoja ya msingi. Unapotaja mwanasiasa Tanzania lazima awe ni mwanachama wa chama flani, na unapotoa mfano wa tukio, lazima pawe na wafanyaji. Sasa suala tu ni kwamba kinachotolewa mfano kweli kipo na kimetokea kama kilivyo jajwa au laa. Hiyo ni simple logic.

Unachotakiwa kuangalia ni msingi wa hoja, achana na ushabiki wa kitoto.

Ila nimejifunza kitu kutoka kwenye signature yako. Shukuran.
 
Usiwe na mtizamo mfupi kiasi hicho. Huo ni mfano tu nimeutoa ili kuelezea hoja ya msingi. Unapotaja mwanasiasa Tanzania lazima awe ni mwanachama wa chama flani. hiyo ni simple logic.
Unachotakiwa kuangalia ni msingi wa hoja achana na ushabiki wa kitoto.
Wala sinaga ushabiki wa kitoto kama wewe. Uzuri pia mimi na wewe sio wageni hapa jukwaani. Nakuelewa sana wazee wa manumberi.
 
Wala sinaga ushabiki wa kitoto kama wewe. Uzuri pia mimi na wewe sio wageni hapa jukwaani. Nakuelewa sana wazee wa manumberi.
sasa kama mimi nimetoa mfano ambao si sahihi, wewe pia si una nafasi ya kutoa mfano sahihi? au wewe nafasi yako ni kulaumu? haya mfano wangu si sahihi, wewe toa mfano sahihi sasa! hoja ya kwamba mimi na wewe tunafahamiana, inasaidia nini kwa hapa?

Any way hoja ya msingi umeielewa lakini?
 
sasa kama mimi nimetoa mfano ambao si sahihi? wewe pia si una nafasi ya kutoa mfano sahihi? au wewe nafasi yako ni kulaumu? haya mfano wangu si sahihi, wewe toa mfano sahihi sasa!

Any way hoja ya msingi umeielewa lakini?
Never argue with...............
 
Siasa chafu zipo Dunia nzima tunatofautiana kiwango na uelewa wa Raia kutafsiri hizo Siasa

kuna Mfaransa alikuwa anataka kumtoa Rais wake Sarkozy kwenye Uchaguzi Mkuu, alikuwa ndie Mkurugenzi Mtendaji wa IMF jijini Washington

Siku anajiandaa kwenda Airport kurudi Paris alitokea Mwanadada mwenye asili ya Ki Africa ambae ni mhudumu wa Hotel akajikamatisha kwa jamaa ili apate skin contact na Jamaa

Jamaa haku notice Akaenda zake Airport akakuta wameshaandaliwa Askar na Camera za Waandishi akakamatwa kwa tuhuma za Sexual harrasment

Ikawa headline Ufaransa yote matokeo yake akazuiwa kusafiri akashindwa kuchukua fomu ya kuwania Urais na akatakiwa Ku resigns u DG wa IMF

Baada ya uchaguzi Yule Mwanamke akajitokeza na Ku omba radhi kwa igizo lile japo
Wenzie kishakosa kazi IMF na Urais kaukosa

Trump kawafanyia umafia Hilary Clinton na sasa joe Biden kupitia Ukraine
 
Dah aiseee! uko sahihi mzee. Lakini tunafanyaje sasa maana kuna mambo yanaathiri watu wengi na pengine vibaya sana hasa Afrika.
 
sory, nimeandika haraka haraka nilikuwa sija edit vizuri.
Kwa muhtasari ninachosema, tumetawaliwa na utamaduni wa siasa chafu na wakati mwingine matukio ya dhulma. Lakini kwa bahati mbaya ni kwamba mara nyingi mambo hayo hutokea katika mazingira ambayo mimi na wewe hatuwezi kuyazuia,sasa ni nini cha kufanya? ndio msingi wa mjadala.
Haya usirudie tena siku nyingine sawa mtoto mzuri![emoji1787]
 
Back
Top Bottom