Siasa ilileta uhuru na amani kwa Tanzania na Siasa itaondoa uhuru na amani kwa nchi ya Tanzania

Siasa ilileta uhuru na amani kwa Tanzania na Siasa itaondoa uhuru na amani kwa nchi ya Tanzania

Pang Fung Mi

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2022
Posts
6,653
Reaction score
13,919
Salamu,

Napata wakati mgumu sana nikiwaza juu ya kuuawa kwa Rtd Officer, Ally Mohammed Kibao, natafakari sana na sijaweza kuwa sawa kuhusu kifo cha huyu mtu muhimu sana kwa Taifa.

Nawaza ya kwamba waliomuua Ally Kibao wana leseni ya kumuua awaye yeyote yule.

Mti wenye damu huzaa matunda yenye damu, je kwa sasa vyombo vya dola kazi yao ni kuua uhuru na amani?

Je, kazi ya vyombo vya dola ni kufifisha uhuru wa kufikiri, maoni, na mawazo?

Je, nalo hili ni Taifa la watu kusahau haraka kadhia ya mauaji na kupotea?

Je, historia hujirudia kwa kila jambo?

Utamaduni wa kusahau haraka ndio utadumisha uovu uendelee, kuhubiri amani kwenye majonzi ni kazi bure.

Maisha yapo na maisha yanaendelea, je kuna hiari nyingi na kusudi nyingi katika haya Kuzaliwa, kufa, kuua, kuuwawa na kuishi?

Je, kifo ni adhabu? Kuua ni adhabu? Ni sifa ya kupongezwa? Nini nafasi ya Mungu katika Taifa?

Ni maswali tu maisha ni kuishi na katika kuishi kuna kuzaliwa na kisha kufa.

Nyuma na mbele inategemea na ulipo, mbele inaweza kuwa nyuma na nyuma inaweza kuwa mbele.

Alikuwepo Thadei Ole Mushi lakini Leo hii hayupo na watu wamesahau.

Maisha ni abstract term.

Wadiz
 
Katika awamu zote za uongozi Tanzania imeendelea kuwa na amani tele kwa sababu ya weledi na hekima za viongozi wetu

Mama Samia Suluhu ameendelea kuhakikisha nchi yetu inabaki kuwa "kisiwa cha amani na upendo" na amejidhatiti kulidumisha hilo.

Siasa chafu za wapinzani wachache wasiojua thamani ya amani yetu ndizo chanzo cha machafuko katika nchi nyingi

TUZIEPUKE
 
Alikuwepo Thadei Ole Mushi lakini Leo hii hayupo na watu wamesahau.
Ooh! Shakalo bababa lo sakalolo. Imenibidi ninene kwa lugha baada ya mleta mada kunikumbusha mauaji ya huyu ndugu
 
Katika awamu zote za uongozi Tanzania imeendelea kuwa na amani tele kwa sababu ya weledi na hekima za viongozi wetu

Mama Samia Suluhu ameendelea kuhakikisha nchi yetu inabaki kuwa "kisiwa cha amani na upendo" na amejidhatiti kulidumisha hilo.

Siasa chafu za wapinzani wachache wasiojua thamani ya amani yetu ndizo chanzo cha machafuko katika nchi nyingi

TUZIEPUKE
Shukrani, Ila katika mataifa duni mhimili wa Serikali ni nguzo ya kuharibu utulivu na amani, uhuru wa kufikiri, maoni na mawazo yenye kukinzana ndio uhai, Taifa lolote lenye kutumia vyombo vya dola kufifisha uhuru na Demokrasia ni ishara mbaya sana kama maneno , akili na mawazo unapiga nyundo vipi kupigania vita?

Taifa la aina hio hata vitani litashindwa maana raia wake watasaliti.

Sio vema mwenye nguvu kuonesha udhaifu kwa njia ya mabavu ya kificho.

Mkosaji aitwe wazi kwa barua wananchi wajue na sheria ifuatwe.

Karma is real ndiomana wauaji na watekaji wanavuta bangi na kufanya ulevi wa pombe kuimarisha unyama ndani ya nafsi zao.

Na katika hili Serikali ya CCM inawajibu wa kuenzi dira,,misingi, ahadi kuu za mwana CCM ni zenye misingi ya utu , ubinadamu na upendo wa Mungu.

Ikitokea CCM ikaona uonevu, mauaji na utekaji kuwa ni mzaha na vichekesho basi Mungu aliye wetu sote ndio jibu.

1..Utu kwanza

1.Ubinadamu kwanza

1.Utanzania kwanza

Vyama sio msingi wa maisha yetu na Taifa la hovyo ni lenye kupuuza mambo msingi ambayo ni msingi na mtambuka.

Mambo bayana yenye kubeba dhana kuu ya sisi sote.

Isitokee CCM au mwana CCM akajiona yeye ni Mtu, Binadamu, na Mtanzania muhimu kuliko wengine.

Ubaguzi una tabia ya kuzaana wenyewe kwa wenyewe, mfano huyu ni CCM ila ni mgeni, huyu dini fulani, huyu hana mkia, huyu kabila fulani, huyu dini fulani, huyu wa Mkoa fulani huyu wa Kanda ile.

Fanya sherehe, Cheka, Fanya mauaji, tesa watu, teka watu, poteza watu.

Mungu ni Mkuu siku zote.

Siku Moja ikawe siku ya toba na kuomba msamaha na iratibiwe kitaifa yawe ni maombi na toba jumuishi yenye muktadha mseto.

Mungu ni nguzo ya wahanga wa Jana, Leo na kesho kama alivyo yeye ni wa Jana, Leo na Kesho, hivyo yeye ni wa milele daima
 
Back
Top Bottom