kiduni
JF-Expert Member
- Jun 26, 2015
- 348
- 341
Nafikiri sote tunakumbuka kilichofanyika baada ya kupanda kwa gharama za mawasiliano, tulilalamika waziri akijitokeza na kutulaghai yuko pamoja na sisi gharama zitashushwa ifikapo mwezi April cha kushangaza vilibaki vilevile na sisi tukaridhika.
Mwezi April ndo huu gharama zimeongezwa mara dufu, wamekuja kwa style tofauti kidogo ila dhumuni ni lilelile walitangaza ndani ya masaa 24 vifurushi visitishwe jambo ambalo halitatekelezwa tukikaa kimya.
Hakuna ubishi kwa sasa simu ina nafasi kubwa kwenye jamii tunapoongezewa gharama maana yake wanatuongezea ugumu wa maisha binafsi kwa sasa nimelazimika kutumia freebasic ili nisijiumize.
Wito tusiache kuwapigia kelele na tujitahidi kupunguza mapato yao mpaka gharama zishushwe hata vifurushi vilivyopita navyo ghali mno hawayaoni maumivu yetu wenyewe mishahara yao mikubwa na bado wanajilipa posho kwa zao, hawapati maumivu.