Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
SIASA INAHITAJI UWE NA JICHO NA PUA YA BUNDI!
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.
Hakuna somo gumu kama somo la Siasa. Sio udaktari, sio uinjinia, sio ualimu, sio uanasheria, sio ukulima. Siasa ndio somo gumu zaidi Duniani. Kwa sababu Kabla ya yote Siasa ilitangulia na Baada ya yote Siasa ndio itamalizika. Kila kitu kilifanyika Kwa sababu ya Siasa, na wala pasipo Siasa hakuna chochote katika huu Ulimwengu ambacho kingefanyika.
Siasa unazungumzia Mwanzo Kabla ya mwanzo wenyewe na mwisho Kabla ya mwisho wenyewe. Siasa ni maslahi., Kufanya Jambo Kwa lengo la kulinda maslahi fulani ili maisha ya MTU au kikundi cha MTU au viumbe fulani waweze kuishi Kwa Amani na furaha. Na ili uyapate maslahi hayo Kwa urahisi lazima uwe na Power(nguvu), mamlaka na utawala.
Kuipata nguvu, mamlaka, madaraka na utawala hapo ndipo mtiti ulipo. Mchakato wa Kupata nguvu hiyo, kuilinda na kuitumia ndio huitwa SIASA.
Taikon bado nafikiri,
Ili uweze kupata Nguvu, mamlaka, madaraka, na utawala basi itakubidi uwe na mambo haya;
1. Roho ya Simba.
Nazungumzia Ujasiri. Hiyo ni Kanuni namba moja ya kuwa mwanasiasa. Lazima uwe jasiri. Usiwe mwogamwoga. Huwezi kuwa mwanasiasa kama unatabia ya uoga. Ujasiri ni Jambo la Kwanza Kwa mwanasiasa. Roho ya Simba itakusaidia kutawala, kutisha maadui, kukabiliana na changamoto na maadui.
Huwezi kuyapata madaraka, mamlaka, utawala kama hauna Roho ya Simba.
2. Uhusika wa Nyoka.
Moja ya Sifa ya Nyoka ni Ujanjaujanja, Werevu, lakini Mbaya zaidi ni Roho yake isiyo na huruma. Pia na unafiki. Ili uwe Mtawala ni lazima uwe na tabia ya Nyoka na umbo lake. Hauna miguu lakini unatembea, uwe MTU wa kufanya mambo yako chinichini kama Nyoka. Nyoka anaweza kuingia ndani ya nyumba yako akaishi miaka nenda Rudi mpaka likawa joka usijue. Hivyo ndivyo unavyotakiwa Ku- operate. Kimyakimya. Lakini usisahau unafiki.
3. Roho ya Kobe.
Lazima uwe na Gamba gumu, usiwe lainilaini. Siasa haihitaji Watu lainilaini ambao wakitupiwa maneno wanapiga kelele, au wanadhurika kirahisi iwe Kiroho, Kiakili, kihisia na kimwili. Ni lazima uwe na Gamba la Kobe litakalozuia mashambulizi.
Lakini pia mara nyingi uwe MTU wa kuingiza kichwa Gambani. Usiwe mtu wa kujibizana jibizana na watu.
4. Roho ya BUNDI.
Uwe na uwezo wa kuona gizani, kuona vilivyofichwa, kuona ambavyo wengine hawavioni kirahisi. Pia uwe na pua ya kunusa hatari, njama, hila na mitego ya maadui yako.
Huwezi kuwa mwanasiasa mkubwa hasa ukaingia katika ligi na wanasiasa wenzako ikiwa huna macho ya kuona na kutambua maana ya kila unachokiona, kunusa harufu na kujua maana ya kila harufu. Utakwama.
Lazima ujue Mbaya wako tangu siku ya Kwanza mnapokutana.
Kwenye Siasa Kanuni inayotumika ni ileile ya kidunia isemayo; Trust no one.
Kila mtu kwenye Siasa anaweza kuwa adui yako.
Kwenye Siasa, adui yako ndiye Rafiki yako. Na Rafiki yako ndiye adui yako. Ni Kwa sababu adui unayemjua ni Rafiki wa kweli, lakini Rafiki usiyemjua ndiye adui atakayekuangusha.
Ili mamlaka, utawala na mamlaka viendelee kuwa na Amani lazima haya yawepo;
1. Imani potofu hasa zenye lengo la kutisha wanaotawaliwa.
2. Kuficha ukweli na kuwafanya wawe vipofu. (Elimu ya kweli isitolewe au wajinga wawe wengi)
3. Dola, Jeshi lazima liwe na uaminifu Kwa Watawala
4. Uvamizi
Hii ni ikiwa jamii haina Mila potofu na wanaelimu ya kutosha basi lazima taifa moja livamie taifa jingine ili kulinda mamlaka na utawala wa taifa vamizi.
Mfano, siku ambayo Tanzania ikiwa na watu wasio na Mila potofu na watu wenye Elimu nzuri ndio siku ambayo kama taifa viongozi na Usalama wa taifa watapanga kuvamia mataifa mengine Kwa kulinda maslahi ya Tanzania.
Hivyo ndivyo Siasa zinavyofanya kazi.
Kama hakuna adui kwenye Siasa itamaanisha kuwa utawala huo umeanguka Kwa sababu hakuna Siasa bila uadui. Kitendo cha kuona huna adui kwenye Siasa za juu tafsiri yake anguko lako limefika, umeanguka.
Ikiwa utamuangamiza adui yako na ukaa muda mrefu pasipo adui hiyo haitakuwa nzuri kiutawala.
Ni lazima uunde Adui bandia kwaajili ya maslahi ya utawala wako.
Imani kupitia dini na Akili kupitia Elimu ndio Njia pekee ya kuwatawala Watu. Lakini ikiwa Watu watakuwa na Akili na Imani sahihi basi uvamizi maeneo mengine ni option isiyoepukika.
Taikon nimemaliza, mwenye swali aweza kuuliza.
Nawatakia maandalizi Mema ya Sabato.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam