Siasa iwe kama mpira wa miguu. Usajili uwe kwa msimu

Siasa iwe kama mpira wa miguu. Usajili uwe kwa msimu

Malaria 2

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2023
Posts
6,846
Reaction score
10,288
Suala la kuhama Mwanasiasa kuhamia chama chengine iwe kwa msimu hasa kipindi Bunge lishavunjwa ili kujenga heshima katika siasa.

Mwanasiasa anaetaka kuhamia chama chengine asubiri muda huo. Hali ilivyo hivi sasa Watanzania wanyonge wanampigania Mwanasiasa ashinde uchaguzi hali na mali hadi wengine kupoteza maisha, baadae Mwanasiasa huyo anahama chama na kuanza kushusha matusi kule anakotoka na kuona wale walipoteza Rasilimali kwa ajili yake sio chochote.

Hii inawafanya wananchi wengi kukata tamaa na kuona hakuna ukweli katika siasa

Usajili uwe kama Simba na Yanga ufanyike mwanzo wa msimu kuwe CHADEMA DAY, CCM DAY, NCCR DAY, ACT WAZALENDO DAY, watuonyeshe usajili wao mpya kutoka vyama vyengine.

i. Hii itasaidia Kujenga heshima katika siasa
ii. Itaokoa fedha kwa Tanzania endapo Mbunge kati kati ya msimu kuhurusiwa kugombea chama chengine.
 
Madau ya usajili yawekwe wazi. Pia wakusanye kodi toka kwenye biashara hiyo, kuna matrilioni ambayo yangekusanywa kutoka kwenye biashara hiyo.
 
Back
Top Bottom