Pre GE2025 Siasa kuingia kwenye michezo na wanamichezo kutumika kisiasa hatujali kuibomoa sekta hii?

Pre GE2025 Siasa kuingia kwenye michezo na wanamichezo kutumika kisiasa hatujali kuibomoa sekta hii?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu kwema?

Tumeshuhudia mara kadhaa siasa kupenyezwa taratibu kwenye michezo na wakati mwingine hata kushawishi baadhi ya baadhi maamuzi kufanyika kwa utashi wa kisiasa!

Mara watu kwenda na mabango uwanjani yenye kusifia chama fulani cha kisiasa, mara simu kupigwa wakati wa sherehe ya vilabu kwa kisingizio cha 'kuwasalimia', yaani ili mradi tu wa-make a statement kwenye hadhira hiyo na kuonesha kuwa hata upande huo pia wanakubalika!

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Kwa upande wa soka ipo wazi kabisa ikibanika siasa kuingia kwenye michezo FIFA wanaweza kufungia timu husika kushiriki kwenye michezo na hii itakuwa na madhara makubwa kwa wanamichezo wenyewe na hata kwa taifa kwa ujumla.

Mbali na kufahamu haya yote kwa nini yanaendelea kufanyika? Ni kwamba hatujali athari za vijana na wote waliokuwa kwenye sekta hii?

Matukio ya siasa kuingia kwenye michezo:

~ Msigwa: Ufafanuzi wa suala la Simba
~ Serikali iwe makini, itaigawa Nchi
~ Hili halikubaliki ni kama ubaguzi kwenye timu kama Simba
~ Ahmed Ally: Si jambo jema hata kidogo Serikali kutoa Posho ya 1.2M pamoja na Usafiri kwa Mashabiki wa Yanga, Mpira ni Starehe
~ Serikali yaonesha ushabiki wa wazi kwa Yanga kupeleka mashabiki South Africa
~ Waziri Ndumbaro, kama kweli wewe ni mzalendo wa kweli amuru Mabango ya Rais Samia yaache kuingizwa uwanjani
~ Mambo haya ndiyo yanaidharaulisha nchi yetu
~ Mabango yenye picha ya Rais Samia yapuuzwa kwenye mapokezi ya Yanga
~ Suala la Rais Samia kutoa pesa na ndege kwa timu kusafiria ni kwa gharama ya nani?
~ Rais Samia atatoa Ndege kuipeleka Yanga jijini Mbeya
~ Rais Samia Suluhu Aahidi Kutoa Ndege Kwa Yanga Mchezo wa Fainali Pamoja na Milioni 20 Kila Goli
~ Rais Samia aibua shangwe na Nderemo kwa mashabiki wa Simba baada ya kupiga Simu moja kwa moja uwanja Wa Taifa
~ Nadhani kuna kitu hakiko sawa huyu sio Ahmed Ally tunaemjua, aipigia kampeni CCM
~ Rais Samia awabubujisha machozi ya furaha wana Yanga, awapigia simu Uwanja wa Taifa
~ Mwigulu awaomba viongozi wa Yanga wapotezee suala la Kagoma ili aweze kucheza Simba
~ Ally Kamwe aibua shangwe akiyakata mauno kwenye Tamasha la Kizimkazi
~ Ligi ya Bashungwa Karagwe CUP 2024 yahitimishwa kwa kishindo, Rais Samia apewa tano
~ Mlioelewa alichokizungumza Rais Samia kuhusu Simba SC na Yanga SC naombeni kueleweshwa
~ Muda umefika serikali kuingilia kati kufanya maamuzi magumu kuliko kuiachia TFF pekee
~ Waziri Bashungwa achangia milioni 15 kuboresha Uwanja, apongeza Dkt. Biteko kwa msaada katika Sekta ya Michezo
~ Siasa imeendelea kupenyezwa kwenye michezo bila kujali athari zake mbeleni, mpaka Tanzania tufungiwe ndio akili zitakaa sawa!
~ Taratibu inaanza kuwa kawaida kuwa na picha za wanasaisa kwenye jezi za timu, mwisho timu zitakuwa kama vikundi vya wanasesere kwa wanasiasa
~ Mnaoshangaa Rais Samia kutoa tsh 10m kwa kila Goli mjue Rais Nguema wa Equetorial Guinea ametoa bonus ya Euro million 1 kwa timu ya Taifa!
~ Kule AFCON kuna timu nyingine ina Bango la Rais wao uwanjani zaidi ya Tanzania?
~ Kama Nchi Tunataka AFCON '27 Isiwe Aibu? Ondoa CCM '25 Vinginevyo ni Majuto
~ Mbunge Juliana Shonza Akabidhi Mifuko 30 ya Saruji (690,000) Ujenzi Ofisi ya UWT Kata ya Ibaba
~ Video: Rais Samia apewa zawadi ya ng'ombe na madereva bodaboda
~ Bondia Abdul Ubaya akabidhiwa milioni 5 za Mama
~ DC Kilakala asema Samia Cup imehamasisha wananchi kushiriki kwenye kujiandikisha Uchaguzi Serikali za Mitaa
~ Mbunge Mavunde Akabidhi Uwanja wa Michezo wa Kisasa Shule ya Sekondari K/Ndege Dodoma
~ Makonda aanzisha mchezo wa mashindano ya pikipiki Arusha
~ Mbunge Mavunde Akabidhi Uwanja wa Michezo wa Kisasa Shule ya Sekondari K/Ndege Dodoma
~ Mashindano ya Dk. Samia, Gekul Cup yahitimishwa Babati Mjini, washindi wajinyakulia Tsh. Milioni 1
~ Tufanyeje ili wanasiasa wenye agenda zao wasiingilie michezo? Ni wavugaji wanaoua michezo
~ TAMISEMI michezo sio chombo cha propaganda, tafuteni njia nyingine ya kupenyeza siasa zenu
~ Rais Samia aipa Taifa Stars Milioni 700 kufuzu AFCON
~ Mwana FA: Ushindi wa Taifa Stars ni maalum kwa Rais Dkt. Samia Suluhu
~ Mwakinyo atetea Ubingwa wa WBO Afrika kwa KO, atwaa Milioni 10 za Rais Samia
~ Rais Samia alivyopiga simu usiku kwenye pambano la 'KO ya Mama'

2025
Januari

~ Wabunge Mashabiki wa Simba, Yanga kuumana azania bank Bunge bonanza

Februari
Machi
 
Wakuu kwema?

Tumeshuhudia mara kadhaa siasa kupenyezwa taratibu kwenye michezo na wakati mwingine hata kushawishi baadhi ya baadhi maamuzi kufanyika kwa utashi wa kisiasa!

Mara watu kwenda na mabango uwanjani yenye kusifia chama fulani cha kisiasa, mara simu kupigwa wakati wa sherehe ya vilabu kwa kisingizio cha 'kuwasalimia', yaani ili mradi tu wa-make a statement kwenye hadhira hiyo na kuonesha kuwa hata upande huo pia wanakubalika!

Kwa upande wa soka ipo wazi kabisa ikibanika siasa kuingia kwenye michezo FIFA wanaweza kufungia timu husika kushiriki kwenye michezo na hii itakuwa na madhara makubwa kwa wanamichezo wenyewe na hata kwa taifa kwa ujumla.

Mbali na kufahamu haya yote kwa nini yanaendelea kufanyika? Ni kwamba hatujali athari za vijana na wote waliokuwa kwenye sekta hii?
Subiri itakapo fifia halaf watafute wa kumrushia lawama, kama vile sekta zingine zilizopatea na matatizo similar
 
Subiri itakapo fifia halaf watafute wa kumrushia lawama, kama vile sekta zingine zilizopatea na matatizo similar
Ni kweli, fikiria ajira zitakazopotea hayo yakikitoea ni balaa... tunatengeneza matatizo makubwa kwa sababu ya maslahi binafsi ya mtu mmoja
 
"sisiemu siyo chama bali ni dola,mambo mengi ya msingi sisiemu wamesiasisha na ngumu sana kupata maendeleo,kikatiba nchi yetu ina mfumo wa vyama vingi ila kimatendo tupo kwenye chama kimoja" - Yericko Nyerere
Ni kweli kabisa, lakini chama si kinajegwa na sisi wenyewe?!
 
Back
Top Bottom