Siasa Michezoni (Simba vs Al Ahly): Azam TV wanapaswa kuonywa, kuadhibiwa au kufungiwa!

Siasa Michezoni (Simba vs Al Ahly): Azam TV wanapaswa kuonywa, kuadhibiwa au kufungiwa!

Lakini Bongo tumesema hatuutaki Ujinga wao. Ukarine Kidogo unaweza kuwatetea hawakuipiga Urusi ila walionesha dharau kwa Urusi lakini Hamasi walienda Kuwapiga Waisreal kwenye Ardhi yao. Sasa hapo Wakutetewa sahihi ni yupi kati ya Israel na Parestine. Infact: Wakutetewa na kuungwa Mkono ni Israel maana ndiye aliyeonewa lakini cha Kupingwa ni Vita inayoendelea na siyo kuungana na Mkorofi.
Tunazungumzia kanuni ya fifa kuingiza siasa kwenye mpira. Hatuzungumzii nani kamuanza nani. Israel ndiyo ameanza kuikalia nchi ya watu kimabavu
 
Shida siyo watu kuonesha hisia, wakati wa kuchukua video au picha za matukio za mpira kuna taratibu na sheria ili lengo la mpira usiharibike.

Ebu fikiria wanaoisapoti Israel nao wangeingia na mabango zao humo kweli maana ya burudani ingekwepo?
Walichofanya Azam ni sawa na kuonesha picha ya mchazaji alievunjika uwanjani huku miguu ikichuruzika damu kitu ambacho hakitakiwi, iwapo kamera imeinasa kwa bahati mbaya unatakiwa kuiondoa kwa uharaka na baadae inafutwa.
Mbona kila mechi huko uingereza kuna armbands za Ukraine.... mabango ya Ukraine etc why kwa Palestine ndio nongwa?
 
Ireland na wa scottish wazi tu wana support Palestine na sababu kubwa hata wao wana history ya kukaliwa kimabavu na kunyanyaswa wanajuwa machungu yake ndio maana kwenye mechi ya Celtic bendera za Palestine kibao shida hawa huku wenye makanisa kama mabanda ya kuku na bendera za Israel bila kujuwa maana yake. Mungu ni wa wote hakuna aliyempendelea na kama yuko huyo Mungu anapendelea basi natamka hakuna Mungu.
Israel na dini ya Uyahudi hawaamini kabisa katika mrengo wa kushoto lakini wao wamo tu kujikweza
 
Kilichotokea jana kwenye ufunguzi wa mashindano ya African Football League kwenye mechi kati ya Simba na Al Ahly kupitia Azam TV ambapo kwa sekunde kadhaa kimakusudi walionyesha bango la mashabiki lenye maandishi yenye mlengo wa kushabikia siasa za mashariki ya kati (kifupi bango lile lilikuwa na maandishi ya kiingereza likipeleka ujumbe wa kuunga mkono harakati za taifa la Palestina), kitendo kile kilikuwa ni kitendo cha aibu na fedheha kubwa kuonekana michezoni kupitia matangazo ya moja kwa moja kwenye TV. Wadau kadhaa duniani waliofuatilia matangazo yale wameonyesha kusononeshwa na namna Tanzania kupitia Azam Media nk walivyoamua kimakusudi kushafua taswira nzima ya matangazo ya mpira wa Afrika.

Kwa kifupi sana kwa sheria za soka za FIFA na CAF lile lilikuwa ni kosa, na kama litashikiwa bango huenda Azam TV na mamlaka za soka hapa Tanzania zikajikuta matatani.

Kimantiki tukio lile lilipangwa (kwa waliokuwepo uwanjani hususani jukwaa lile wanaelewa vizuri) na kuratibiwa kikamilifu huku Azam media ikihusika kwa 100%. Na hapa nitachambua kwa kina;

1. Bango lile lilikuwa kubwa, pana, refu na maridadi. Hivyo waandaji walikuwa ni watu waliojipanga vizuri.

2. Bango lile liliingizwa uwanjani bila usumbufu wowote na liliendelea kuwepo uwanjani kwa uhuru karibu muda wote wa mchezo. Hii inaashiria mamlaka za soka na usalama hapa Tanzania zilibariki tukio lile kwa 100%.

4. Bango lile liliandikwa kwa kiingereza, lengo likiwa kufikisha ujumbe kimataifa (wahusika wakijua 100% Azam Tv watarusha lile tukio!)

5. Bango lile lilikuwa limeshikiliwa kwa ujasiri na mashabiki wengi wa Al ahly (wamisri) na wachache wa simba (watanzania). Hii inaashiria ushirikishi wa pamoja.

6. Video zinaonyesha walioshirikia lile bango wakiwa standby kuchukuliwa video na Azam Tv, na wengine wakikimbilia kulifikia bango ili video inayochukuliwa iwaonyeshe. Hii inaashiria wapiga picha wa Azam walikuwa 100% attention&concious kuhakikisha ujumbe unafika.

7. Live coverage ya tukio ilikaa kwa sekunde kadhaa hewani ili kila mtazamaji aone, lakini pia kuna namna coverage ilihamia kwenye kitu kingine na haraka ikarejea kwenye tukio lile lile. Hii inaashiria umakusudi wa 100% tukio lile liende hewani.

8. Watangazaji wa Azam Tv hawakusema chochote (walikaa kimya) kama vile hawaelewi chochote wakati tukio lile likiwa hewani, huenda kwa kuwa walihisi ukakasi, hawakuandaliwa au kuogopa kitu.

9. Azam media wamekuwa na mtindo wa kurudia kuonyesha video za mechi iliyochezwa hapo kabla, hivyo wangeweza kuhariri kwa kuondoa vipande vya video vyenye utata, lakini kwa tukio la jana wameliacha vile vile mpaka sasa. Nadhani lengo ni ujumbe ufike vilivyo.

10. Mpaka sasa hivi Azam media hawajaomba radhi wala kutaka kutolea ufafanuzi tukio lile kuruka kwenye matangazo yao. Hii kuashiria Azam media wanaamini walikuwa sahihi na walijiandaa kurusha tukio lile kikamilifu.

IMG_4339.jpg

Vipi na hii ilikuwa leo katika mechi ya Liverpoll na Everton, itakuwa hawa wazungu wa sky sports wadini sana kama Azam sports
 
Hamasi walienda Kuwapiga Waisreal kwenye Ardhi yao.
Ardhi yao? Ile ardhi ilikua ya Palestine ila Israel waliipora 1960s huko. Yaani ni sawa na Idd Amin angeipora kagera alafu ipite miaka 30 tukija ipigania tuambiwe tumevamia ardhi ya Uganda!! Are you serious?
 
Fikiria Mashabiki wa Simba waende Misri na Bango la Kuisifu Izrael wakalioneshe uwanjani..

we fikiria tuu...

endelea kufikiria vizuri...

ndio maaana sheria zikawekwa kupiga marufuku hisia za kisiasa michezoni.
Sheria ipi hiyo?
 
Sheria zifuatwe.

Serikali iidhibu TFA na pia awaadhibu Azam TV kwa faini kama zile za TCRA kwa mitandao ya simu wanapokiuka sheria ba kanuni.

FIFA iwaadhibu TFA/Tanzania kwa kanuni zake.

Watu binafsi waliohusika na hiyo mipango yote viadhibiwe vikali kwa kuichafua nchi, kwa kupeleka siasa kwenye michezo.
Isn't this against free speech? Tukianza kupangiwa cha kuongea ndio itakua kaburi la media hapa Tanzania
 
media inakosa gani media wamepewa kazi kuonesha matukio yote yaliyokuwepo pale , roho inakuuma kwa sana hilo bango lingeoneshwa dakika5 ungepasuka
Hisia ulizonazo ni negativity
 
Watanzagiza mnapenda kulalamika hamjui watu weupe wapo na Akili Sana na wanapenda haki na sio mbumbumbu Kama nyie
 
Free Palestine ndio udini.????? Kwani Palestine WA anakaa waislamu peke Yao.???

Ila free Ukraine ilikuwa sio udini.???

Kuna watanzania hawa hawana akili za kufikiria hata kidogo ,wao kilichopo mbele Yao ndio wanakiamini.
Hawa ndio watu wanaofanya vita ichochewe. Nonsense kabisa

Cha msingi vita isitishwe watu wasiuliwe kuna waislam Israel lakini kuna wakristo palestina

The point ni kusitisha mapigano hatupendezwi nayo.
 
Azam ndio mwenye kosa kubwa zaidi.
Bila Azam Tv huenda hakuna mtu angemjua hicho kitu unless aliyekuwepo uwanjani, jukwaa lile.
We jamaa ni mjinga na mbumbumbu sana. Mabango yako kila mahala. Wewe mwenyewe ID yako umeweka bango, acha watu wafikishe jumbe zao usiwapangie. Uwanja mzima umeliona bango hilo moja tu? Umepangilia mwenyewe sijui hoja 10 kumbe zote pumba(vu).

Nikikunukuu, "Wadau kadhaa duniani waliofuatilia matangazo yale wameonyesha kusononeshwa na namna Tanzania kupitia Azam Media nk walivyoamua kimakusudi kushafua taswira nzima ya matangazo ya mpira wa Afrika", hao wadau wamekuambia kua hawakupenda? Umewasikia wapi?
 
Kilichotokea jana kwenye ufunguzi wa mashindano ya African Football League kwenye mechi kati ya Simba na Al Ahly kupitia Azam TV ambapo kwa sekunde kadhaa kimakusudi walionyesha bango la mashabiki lenye maandishi yenye mlengo wa kushabikia siasa za mashariki ya kati (kifupi bango lile lilikuwa na maandishi ya kiingereza likipeleka ujumbe wa kuunga mkono harakati za taifa la Palestina), kitendo kile kilikuwa ni kitendo cha aibu na fedheha kubwa kuonekana michezoni kupitia matangazo ya moja kwa moja kwenye TV. Wadau kadhaa duniani waliofuatilia matangazo yale wameonyesha kusononeshwa na namna Tanzania kupitia Azam Media nk walivyoamua kimakusudi kushafua taswira nzima ya matangazo ya mpira wa Afrika.

Kwa kifupi sana kwa sheria za soka za FIFA na CAF lile lilikuwa ni kosa, na kama litashikiwa bango huenda Azam TV na mamlaka za soka hapa Tanzania zikajikuta matatani.

Kimantiki tukio lile lilipangwa (kwa waliokuwepo uwanjani hususani jukwaa lile wanaelewa vizuri) na kuratibiwa kikamilifu huku Azam media ikihusika kwa 100%. Na hapa nitachambua kwa kina;

1. Bango lile lilikuwa kubwa, pana, refu na maridadi. Hivyo waandaji walikuwa ni watu waliojipanga vizuri.

2. Bango lile liliingizwa uwanjani bila usumbufu wowote na liliendelea kuwepo uwanjani kwa uhuru karibu muda wote wa mchezo. Hii inaashiria mamlaka za soka na usalama hapa Tanzania zilibariki tukio lile kwa 100%.

4. Bango lile liliandikwa kwa kiingereza, lengo likiwa kufikisha ujumbe kimataifa (wahusika wakijua 100% Azam Tv watarusha lile tukio!)

5. Bango lile lilikuwa limeshikiliwa kwa ujasiri na mashabiki wengi wa Al ahly (wamisri) na wachache wa simba (watanzania). Hii inaashiria ushirikishi wa pamoja.

6. Video zinaonyesha walioshirikia lile bango wakiwa standby kuchukuliwa video na Azam Tv, na wengine wakikimbilia kulifikia bango ili video inayochukuliwa iwaonyeshe. Hii inaashiria wapiga picha wa Azam walikuwa 100% attention&concious kuhakikisha ujumbe unafika.

7. Live coverage ya tukio ilikaa kwa sekunde kadhaa hewani ili kila mtazamaji aone, lakini pia kuna namna coverage ilihamia kwenye kitu kingine na haraka ikarejea kwenye tukio lile lile. Hii inaashiria umakusudi wa 100% tukio lile liende hewani.

8. Watangazaji wa Azam Tv hawakusema chochote (walikaa kimya) kama vile hawaelewi chochote wakati tukio lile likiwa hewani, huenda kwa kuwa walihisi ukakasi, hawakuandaliwa au kuogopa kitu.

9. Azam media wamekuwa na mtindo wa kurudia kuonyesha video za mechi iliyochezwa hapo kabla, hivyo wangeweza kuhariri kwa kuondoa vipande vya video vyenye utata, lakini kwa tukio la jana wameliacha vile vile mpaka sasa. Nadhani lengo ni ujumbe ufike vilivyo.

10. Mpaka sasa hivi Azam media hawajaomba radhi wala kutaka kutolea ufafanuzi tukio lile kuruka kwenye matangazo yao. Hii kuashiria Azam media wanaamini walikuwa sahihi na walijiandaa kurusha tukio lile kikamilifu.
AZAM Lazima watetee warabu wenzao!
 
AZAM ni wadini sana, nshasema AZAM hawana ETHICS za habari. Matangazo yao yapo kidini zaidi na sijajua kwanini Wasirivoke leseni yao ya matangazo kutoka kuwa chombo cha habari cha kijamii SECULAR na kuwa cha kidini non SECULAR.
Ni ujinga kufikiri kuwa kuiunga mkono palestina ni udini,kuna watu wajinga humu wanafikiri Israel ni wakristu,Israel sio wakristu,wana dini yao ya kiyahudi,mpk mda huu wanaamini masiha bado hajaja na hajazaliwa,wao hawana injili wanatumia torati.palestina tunamuunga mkono kwa sababu za kibinadamu juu ya madhila anayofanyiwa,hayakubali kwa binadamu yoyote mwenye akili timamu.
 
Kwenye kanuni na sheria za mpira wa miguu za FIFA, CAF na TFF haiko hivyo, hisia zinazoruhusiwa ni hisia za soka tu. Kila hisia ikiruhusiwa huzaa fujo na kuwagawa mashabiki. Kifupi ni kosa.
Nyie acheni upuuzi wenu,kwa nn Russia kaadhibiwa kwenye fifa na uefa? Kama siasa kwenye michezo haimo?
 
Nenda kasome sheria za soka za FIFA na CAF ndio utanielewa.
Milengo ya kisiasa kwenye soka huwa hairuhusiwi.
Kila mtu ana hisia zake, sasa kila mtu akaruhusiwa kuweka hisia zake uwanjani hali itakuwaje?
Na vipi kuhusu putin na Ukraine? Huhawahi kuona bango lolote likisema stop putin in war, na kwa nn Russia imeondolewa kwenye muchezo ya kimataifa kama soka na siasa ni mbalimbali?
 
We acha mkuu yani mimi mwenyewe nashangaa hili suala jinsi waafrika wanavyolichukulia kwa hisia kali kuliko hata vita zilizopo kwenye nchi za waafrika wenzao.
Watu wanabishania Dini zilizoletwa na Wazungu na Waarabu mpaka povu linatoka ! Kisha watu hao hao eti kwenye thread nyingine wanahimizana wawe na umoja wa kuiondoa CCM madarakani 😂😂😂😂😂

Ndoto za Alinacha kupata umoja huo hapa Nchini ! 🇹🇿 Mungu ibariki Tanzania 🙏🙏🙏
 
Back
Top Bottom