Siasa Michezoni (Simba vs Al Ahly): Azam TV wanapaswa kuonywa, kuadhibiwa au kufungiwa!

Hapa wizara husika ya michezo, wizara ya mambo ya nje na TFF wanatakiwa watoe maelezo kuhusu uwepo wa bango hilo, kwa upande wa Azam Tv wao wamejikita kwenye udini kama ilivyo kawaida yao na huenda liliandaliwa Zanzibar.
Ulinzi ulikua chini ya caf na FIFA,Azam walionesha matukio yatokeayo uwanjani
 
Sijaona tatizo lolote hapo kuhusu hilo bango sababu ni hisia zao, ingekuwa jamba tofauti ikiwa wangesema Tanzania tupo pamoja nao hii ingemaanisha wanatuunganisha sote ilhali sio wasemaji wetu wala wawakilishi wetu


ila nachelea kusema kila unachokiona hapo kwenye live coverage huwa kimekusudiwa unless ni cha ghafla, sababu kwenye live yoyote switcher (anayekuwa kwenye OB) anaona picha kutoka camera zote zilizopo uwanjani (ziwe 10 hata zaidi) hivyo anaamua picha ipi iende kwa maelekezo pia ya Director, na yeye ndio huamua shot gani iwepo na ipi isiwepo


So hiko ni kitu cha kawaida sana, umeoneshwa ili uone.
 
Nenda kasome sheria za soka za FIFA na CAF ndio utanielewa.
Milengo ya kisiasa kwenye soka huwa hairuhusiwi.
Kila mtu ana hisia zake, sasa kila mtu akaruhusiwa kuweka hisia zake uwanjani hali itakuwaje?

Zile nyimbo walikua wanaimba Morocco na wenyeji world cup iliyopita kuunga mkono Palestina zilikiuka sheria za FIFA?

Au chuki binafsi na Azam? Palestina ni nchi sio dini. ANC South Africa wanaunga mkono juhudi za wapalestina kujitafutia uhuru wao, nao ni wadini?
 
Picha?
 
Wabongo wanatia sana ujuaji sana,
Ila ile match ya jana mtu yeyote anayejua mpira akiitazama angejua Azam pale ana commentators tu ila video hana yeye, Watangazaji walikuwa hawana control ya video kabisa, eg replay kuwakuta ghafla wakiwa kwenye story na vitu ka hivyo
 
nenda israel ukaungane nao kuishambulia hamas
 
Beba bango la kuikosoa serikali uone kama Azam Tv watalimulika hata kwa bahati mbaya!!
 
expand...
Kwanini Israel miaka yote anasaidiwa na America, Uk; France na silaha kubwa wanazo na wanazitumia. Lkn juzi wametekwa kama anakamatwa kuku ktk kibanda chake? Wenye nia mbaya yoyote na waislamu mwisho hushindwa wao
 
Umejitahidi sana kuandika lakini kwa hali ilivyo huko Gaza yalipaswa kuwepo mabango mengi zaidi.
Israel ni magaidi kama magaidi wengine.
expand...
Kwanini Israel miaka yote anasaidiwa na America, Uk; France na silaha kubwa wanazo. Lkn juzi wametekwa kama anakamatwa kuku ktk kibanda chake? Ukiingia vita na uislam mwisho wa siku utakua mbaya
 
Sio wajuaje pia hawana walijualo kuna mmoja nilimsikia anasema eti refa kabeba team ...🤣🤣

Hivi unaweza kutongoza Demu mwingine mbele ya Baba mkwe wewe!
 
Kumbe wajinga mpo wengi kiasi hiki?

Andaa hata mabango milioni lakini usiyapeleke kwenye viwanja vya michezo. Siyo mahali pake, na taratibu za mpira zimepiga marufuku soka kutumika kwa mlengo tofauti.
Udini umekujaa ..

Fifa kampiga Ban Urusi mashindano ya kimataifa mpaka UEFA kisa vita ya Ukraine.

Halafu huko Ulaya kipindi cha vita vya Ukraine mabango yalikuwa mengi tu tunayaona DSTV ,na Laliga ikawa kila mechi ukicheki kwenye Tv kuna Benders za Ukraine.
 
Watu wameonesha hisia zao tatizo Nini? Mtoa madam Acha woga wazungu wasitawale fikra zako kijana
Hata huko kwa wakubwa wa Dunia Amerika na Uingereza watu wanaandamana na kuonyesha mabango ya hisia zao na hakuna shida yeyote. !!
Usilolijua ni Usiku wa giza !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…