Siasa Michezoni (Simba vs Al Ahly): Azam TV wanapaswa kuonywa, kuadhibiwa au kufungiwa!

Siasa Michezoni (Simba vs Al Ahly): Azam TV wanapaswa kuonywa, kuadhibiwa au kufungiwa!

Kilichotokea jana kwenye ufunguzi wa mashindano ya African Football League kwenye mechi kati ya Simba na Al Ahly kupitia Azam TV ambapo kwa sekunde kadhaa kimakusudi walionyesha bango la mashabiki lenye maandishi yenye mlengo wa kushabikia siasa za mashariki ya kati (kifupi bango lile lilikuwa na maandishi ya kiingereza likipeleka ujumbe wa kuunga mkono harakati za taifa la Palestina), kitendo kile kilikuwa ni kitendo cha aibu na fedheha kubwa kuonekana michezoni kupitia matangazo ya moja kwa moja kwenye TV. Wadau kadhaa duniani waliofuatilia matangazo yale wameonyesha kusononeshwa na namna Tanzania kupitia Azam Media nk walivyoamua kimakusudi kushafua taswira nzima ya matangazo ya mpira wa Afrika.

Kwa kifupi sana kwa sheria za soka za FIFA na CAF lile lilikuwa ni kosa, na kama litashikiwa bango huenda Azam TV na mamlaka za soka hapa Tanzania zikajikuta matatani.

Kimantiki tukio lile lilipangwa (kwa waliokuwepo uwanjani hususani jukwaa lile wanaelewa vizuri) na kuratibiwa kikamilifu huku Azam media ikihusika kwa 100%. Na hapa nitachambua kwa kina;

1. Bango lile lilikuwa kubwa, pana, refu na maridadi. Hivyo waandaji walikuwa ni watu waliojipanga vizuri.

2. Bango lile liliingizwa uwanjani bila usumbufu wowote na liliendelea kuwepo uwanjani kwa uhuru karibu muda wote wa mchezo. Hii inaashiria mamlaka za soka na usalama hapa Tanzania zilibariki tukio lile kwa 100%.

4. Bango lile liliandikwa kwa kiingereza, lengo likiwa kufikisha ujumbe kimataifa (wahusika wakijua 100% Azam Tv watarusha lile tukio!)

5. Bango lile lilikuwa limeshikiliwa kwa ujasiri na mashabiki wengi wa Al ahly (wamisri) na wachache wa simba (watanzania). Hii inaashiria ushirikishi wa pamoja.

6. Video zinaonyesha walioshirikia lile bango wakiwa standby kuchukuliwa video na Azam Tv, na wengine wakikimbilia kulifikia bango ili video inayochukuliwa iwaonyeshe. Hii inaashiria wapiga picha wa Azam walikuwa 100% attention&concious kuhakikisha ujumbe unafika.

7. Live coverage ya tukio ilikaa kwa sekunde kadhaa hewani ili kila mtazamaji aone, lakini pia kuna namna coverage ilihamia kwenye kitu kingine na haraka ikarejea kwenye tukio lile lile. Hii inaashiria umakusudi wa 100% tukio lile liende hewani.

8. Watangazaji wa Azam Tv hawakusema chochote (walikaa kimya) kama vile hawaelewi chochote wakati tukio lile likiwa hewani, huenda kwa kuwa walihisi ukakasi, hawakuandaliwa au kuogopa kitu.

9. Azam media wamekuwa na mtindo wa kurudia kuonyesha video za mechi iliyochezwa hapo kabla, hivyo wangeweza kuhariri kwa kuondoa vipande vya video vyenye utata, lakini kwa tukio la jana wameliacha vile vile mpaka sasa. Nadhani lengo ni ujumbe ufike vilivyo.

10. Mpaka sasa hivi Azam media hawajaomba radhi wala kutaka kutolea ufafanuzi tukio lile kuruka kwenye matangazo yao. Hii kuashiria Azam media wanaamini walikuwa sahihi na walijiandaa kurusha tukio lile kikamilifu.
Subiri hapo wanakuja Wapalestina wa Chanika.
 
Kweli mkuu hata mm niliona Ile kitu Azam walipuyanga kwakweli
Wewe una udini ndani yako. AZAM si televisheni ya taifa na wala aliyeleta hilo bango hakutumwa na azam. Kwa taarifa yako sisi kama nchi tunapinga kila aina ya ukandamizaji, dhulma na unyimwaji wa uhuru, ndo mana tuna ubalozi wa palestina hapa nchini.
Mbona tv za kimataifa zinaonesha maandamano mbali mbali duniani ikiwemo huko huko magharibi kupinga uchukuaji wa ardhi na mabavu ya Israel. Hujasikia mdudu yoyote anaesema wafungiwe sijui waonywe
 
Hana kosa kwani Hana wahariri, akiona mtu yupo uchi wa mnyama ataionyesha hiyo picha live?
Uchi wa mnyama ni kinyume na maadili, Kuunga mkono Palestina siyo kinyume na maadili wala desturi za jamii, labda kinyume na desturi yako
 
Kwenye kanuni na sheria za mpira wa miguu za FIFA, CAF na TFF haiko hivyo, hisia zinazoruhusiwa ni hisia za soka tu. Kila hisia ikiruhusiwa huzaa fujo na kuwagawa mashabiki. Kifupi ni kosa.
Ila kusemea na kutangaza ushoga ni sawa?

Acheni udini, au kama hamuwezi punguzeni,
Pale oalestina hata wasio na dini wapo na hili ni jambo msilolijua, jueni sasa
 
Ila kusemea na kutangaza ushoga ni sawa?

Acheni udini, au kama hamuwezi punguzeni,
Pale oalestina hata wasio na dini wapo na hili ni jambo msilolijua, jueni sasa
Umewaelewesha vizuri, sana sana watatukana tu.
Naweka mkazo: je kutangaza ushoga kwenye soka ndiyo maadili? Mjibu hili.
Wazungu wanakupeleka pabaya, undumilakuwili, yaani watakuambia hakuna siasa michezoni lakini bendera za kuunga mkono Ukraine zimejaa, za kuunga mkono siasa za ushoga tele uwanjani!!
 
Sisi tuliopigania Uhuru tuliitumia Dar Young Africans katika harakati zetu

Hapo unasemaje?
P9th mmq

Wakati huo hakuna timu ya Tanzania iliyokuwa inatambuliwa na FIFA. Hivyo hatukuwa tunabanwa na sheria yoyote ya FIFA.
 
Uchi wa mnyama ni kinyume na maadili, Kuunga mkono Palestina siyo kinyume na maadili wala desturi za jamii, labda kinyume na desturi yako
Watakachoweza kukujibu ni kukwambia hujasoma, ila hoja hawawezi kujibu
Na wakiona unawashinda watakutusi
 
P9th mmq

Wakati huo hakuna timu ya Tanzania iliyokuwa inatambuliwa na FIFA. Hivyo hatukuwa tunabanwa na sheria yoyote ya FIFA.
FIFA hawa hawa walioitoa Russia kushiriki World cup kwa sababu za kisiasa?
 
Watanganyika tunamatatizo sana, inawezekana Azam wanamakosa au hawana ila kwanini sisi wakazi wa Kazulamimba,Matombo,kisemvule,Kitelewasink tunauona huo mgogoro kwetu ni very sensitive kiasi hiki wakati kila siku waafrica wenzetu wanakufa hapo Congo,Sudan na maeneo kadhaa hapa hapa barani kwetu,kwamba wale ni special sana? Tukombolewe kifikra,yaani watu mnatunisha misuri kubishana........ kwakweli mablack tunashida kubwa sana
We acha mkuu yani mimi mwenyewe nashangaa hili suala jinsi waafrika wanavyolichukulia kwa hisia kali kuliko hata vita zilizopo kwenye nchi za waafrika wenzao.
 
Kilichotokea jana kwenye ufunguzi wa mashindano ya African Football League kwenye mechi kati ya Simba na Al Ahly kupitia Azam TV ambapo kwa sekunde kadhaa kimakusudi walionyesha bango la mashabiki lenye maandishi yenye mlengo wa kushabikia siasa za mashariki ya kati (kifupi bango lile lilikuwa na maandishi ya kiingereza likipeleka ujumbe wa kuunga mkono harakati za taifa la Palestina), kitendo kile kilikuwa ni kitendo cha aibu na fedheha kubwa kuonekana michezoni kupitia matangazo ya moja kwa moja kwenye TV. Wadau kadhaa duniani waliofuatilia matangazo yale wameonyesha kusononeshwa na namna Tanzania kupitia Azam Media nk walivyoamua kimakusudi kushafua taswira nzima ya matangazo ya mpira wa Afrika.

Kwa kifupi sana kwa sheria za soka za FIFA na CAF lile lilikuwa ni kosa, na kama litashikiwa bango huenda Azam TV na mamlaka za soka hapa Tanzania zikajikuta matatani.

Kimantiki tukio lile lilipangwa (kwa waliokuwepo uwanjani hususani jukwaa lile wanaelewa vizuri) na kuratibiwa kikamilifu huku Azam media ikihusika kwa 100%. Na hapa nitachambua kwa kina;

1. Bango lile lilikuwa kubwa, pana, refu na maridadi. Hivyo waandaji walikuwa ni watu waliojipanga vizuri.

2. Bango lile liliingizwa uwanjani bila usumbufu wowote na liliendelea kuwepo uwanjani kwa uhuru karibu muda wote wa mchezo. Hii inaashiria mamlaka za soka na usalama hapa Tanzania zilibariki tukio lile kwa 100%.

4. Bango lile liliandikwa kwa kiingereza, lengo likiwa kufikisha ujumbe kimataifa (wahusika wakijua 100% Azam Tv watarusha lile tukio!)

5. Bango lile lilikuwa limeshikiliwa kwa ujasiri na mashabiki wengi wa Al ahly (wamisri) na wachache wa simba (watanzania). Hii inaashiria ushirikishi wa pamoja.

6. Video zinaonyesha walioshirikia lile bango wakiwa standby kuchukuliwa video na Azam Tv, na wengine wakikimbilia kulifikia bango ili video inayochukuliwa iwaonyeshe. Hii inaashiria wapiga picha wa Azam walikuwa 100% attention&concious kuhakikisha ujumbe unafika.

7. Live coverage ya tukio ilikaa kwa sekunde kadhaa hewani ili kila mtazamaji aone, lakini pia kuna namna coverage ilihamia kwenye kitu kingine na haraka ikarejea kwenye tukio lile lile. Hii inaashiria umakusudi wa 100% tukio lile liende hewani.

8. Watangazaji wa Azam Tv hawakusema chochote (walikaa kimya) kama vile hawaelewi chochote wakati tukio lile likiwa hewani, huenda kwa kuwa walihisi ukakasi, hawakuandaliwa au kuogopa kitu.

9. Azam media wamekuwa na mtindo wa kurudia kuonyesha video za mechi iliyochezwa hapo kabla, hivyo wangeweza kuhariri kwa kuondoa vipande vya video vyenye utata, lakini kwa tukio la jana wameliacha vile vile mpaka sasa. Nadhani lengo ni ujumbe ufike vilivyo.

10. Mpaka sasa hivi Azam media hawajaomba radhi wala kutaka kutolea ufafanuzi tukio lile kuruka kwenye matangazo yao. Hii kuashiria Azam media wanaamini walikuwa sahihi na walijiandaa kurusha tukio lile kikamilifu.
Well Noted Mkuu

Cc Yericko Nyerere
 
Simhusudu mtu yeyote, bali utu na uhuru wangu. Mtu hawezi kunilazimisha nisikie anachotaka nisikie.
Haujalazimishwa chochote mkuu ila mtazamo wako kwa wazungu upo wazi na hii si mara moja kukwambia hiki kitu.
 
Azam wangeenda Buza Kwa Mpalanger kurusha Hilo tangazo sawa ila kama coverage ilikuwa uwanjani Sasa wangefanyaje kuchambua kipi kioneshwe na kipi kisioneshwe! Cameras zinacover sehemu za uwanja na vyote vilivyomo!

We ni mdini haswa na umejidhihirisha, kwahiyo ulitaka cameras zioneshe na kusifia Israel ambao ni wauwaji wa watoto wasio na hatia wa kipalestina?

Je wewe utakubali, utafurahi na kukaa kimya majitu kutoka msikojua yaje yavamie bongo yaikalie kinguvu na kuua watoto wetu?

Fyi , Israel na wazungu Wote Wala sio wakristo ni wapagani kama unawaza Kwa chuki za kidini! Na makanisa ulaya na marekani hayana kazi na hayana waumini , yamebaki kuwa majumba ya kihistoria na hutumika bure kwa sherehe za kijamii kama kipaimara, kitchen party, vikao vya familia, vikao vya harusi, mikutano ya vyama vya kikabila na associations na mnaruhusiwa kupiga mziki kucheza na kulewa! Sisi wabongo hufanyia sherehe za uhuru kanisani tunacheza bongofleva na kulewa chakari!!

Kila kanisa Lina caretaker tu wa kutunza usafi!!

Amka!
 
Abu Dhabi, United Arab Emirates

Live mechi mzima pamoja na uchambuzi wa kina kutoka uwanja wa Benjamin Mkapa National station, bango udhamini lenye jina Benjamin, BET wazee wa mikeka, pia majina ya wachezaji kama Israel hayakuminywa , ishara za peace za baadhi ya wachezaji Al Ahly zimeonekana ktk chombo hiki tajwa cha Mashariki ya Kati na wengi wameifurahia mechi hii ya soka bila kuleta hisia za kisiasa, kiimani bali roho zote zilijkita ktk burudani ya mchezo

View: https://m.youtube.com/watch?v=p0JTpdv9wew&pp=ygUKQUQgU3BvcnRzIA%3D%3D

Comments za wanamichezo waliongalia mechi hii nzima pamoja na mambo kibao yaliyoambatana kabla na baada ya mechi live kwa masaa matatu kote Mashariki ya Kati, Ghuba, Afrika ya Kaskazini n.k ktk channel ya AD Sports wakisisitiza soka michezo ni amani
اللهم صل على 🌸سيدنا محمد🌸🌸صلاة تحسن بها الأخلاق🌸 وتيسر بها الأرزاق 🌸وتدفع بها المشاق🌸 وتملى فيها الآفاق🌸 وعلى آله وصحبه وسلم🌸 صلاة دائمة🌸 من يوم خلقت الدنيا🌸 إلى يوم التلاق🌸 واسترنا بين🌸 يدك 🌸يا عزيز يا خلاق🌸
🌸اللهم صلي وسلم🌸 وزدوبارك على🌸 خيرخلق الله سيدنا 🌸محمد وعلى🌸 آله وأصحابه🌸 أجمعين عدد خلقك 🌸وزنة عرشك 🌸ورضا نفسك🌸 ومداد كلماتك🌸 وعددماخطه 🌸القلم وعدداوراق🌸 الشجر🌸 وعددماكان 🌸وعددمايكون🌸 وعددكل.متحرك🌸 وعددماسكن لي 🌸وأرضى اللهم عن🌸 أصحاب🌸 رسول ألله وعن🌸 التابعين🌸 وتابعيهم 🌸بإحسان وعلينا🌸 معهم بمنك🌸 وفضلك وكرمك

Comment nyingine :
فى ضربة جزاء واضحة للاهلى فى الشوط الأول بعد عرقلة محمود كهربا فى منطقة جزاء سيمبا !! غريبة آوى إنها متحسبتش

Comment nyingine :

هل صليت على النبي محمد اليوم صلي الله عليه وسلم تسليما كثيرا طيبا مباركا فيه ❤❤❤❤❤❤❤
 
Kwahiyo ni sawa kuutangaza ushoga kuliko kuwasemea watu waachwe huru?
 
Azam Media huwa ninawakosoa katika mambo mengi. Ila katika hiyo ishu ya bango sijui limefanya nini!!! Aisee niko upande wenu.
Mtoa mada atakuwa ndiyo wale wenzangu na mimi wanaokaririshwa eti hao Mayahudi (Zionists) ni wateule wa Mungu!! Jambo ambalo siyo sahihi hata kidogo.

Hao Mayahudi ni majitu fulani tu hivi makatili na malowezi kutoka Ulaya na Marekani, yaliyoingia Palestina kibabe kuanzia miaka ya 1900's! Na kuanza kuwaonea hao Wapalestina kwa kuwafunga kwenye jela zao, kuwaua na pia kuwapora ardhi yao. Sasa katika mazingira kama hayo, kwa nini Wapalestina wasijitee?
 
Back
Top Bottom