Siasa na walimu wapya 2020, hajapewa hela ya kujikimu wala mshahara mwaka huu

KAGAMEE

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2013
Posts
4,457
Reaction score
5,454
Hope kila mmoja ameshiba pilau.

Bila kupoteza muda, naomba niende moja kwa moja kwenye lengo la Uzi huu. Namshukuru Mungu mtoto wa baba yangu mkubwa ni moja ya kijana walibahatika kupata ajira ya ualimu mwaka huu(alikuwa mzigo), But alipangiwa mkoa wa mbali sana na tulipo hivyo baada ya kuripoti hakurudi kwa ajili ya kujiandaa so akawa ameganda huku huko.

Cha kushangaza Mpaka sasa analia hana pesa ya matumizi kwa sababu hajapewa hela ya kujikimu wala mshahara hajaingiziwa mwaka huu. Nimejaribu kufanya tafiti nikagundua baadhi ya Halmashauri walishawapa pesa ya kujikimu walimu hao ikiwemo Bukoba na Njombe, Dogo mkurugenzi wake hajasema chochote. Naomba mnisaidie uelewa juu ya hili.

Pesa hiyo inatolewa na kitengo kipi??

Kama ni mkurugenzi, kwanini wakurugenzi wengine washatoa na Wengne hawajatoa? Kila Mkurugenzi anatoa kwa namna anavyojisikia?.

Ina maana dogo mshahara wa mwezi wa 12 ndio hapati/hatapata?

Hawa wakurugenzi hawaoni wanapoteza morari ya hawa vijana?

Mpaka Rais aseme ndio pesa itoke??

Nawasilisha.
 
Hope kila mmoja ameshiba pilau.

Bila kupoteza mda naomba niende moja kwa moja kwenye lengo la Uzi huu.Namshukuru Mungu mtoto wa baba yangu mkubwa ni moja ya kijana walibahatika kupata ajira ya ualimu mwaka huu (alikuwa mzigo),But alipangiwa mkoa wa mbali sana na tulipo hivyo baada ya kuripoti hakurudi kwa ajili ya kujiandaa so akawa ameganda huku huko...
Pole sana kwa hayo yaliyomkuta mdogo wako. Kama ni binti basi kwa huo ukata usishangae ukipata bwana haraka na kutandikwa mimba chap chap. Na kama ni kijana wa kiume hilo usiwaze sana, atapambana kiume hata kuopoa single mother mmoja ambaye ni teacher mwenzake amtunze fresh.
 
Hapo tafuta namna umkopeshe au aanze ajira na mkopo. Hakuna namna mkuu
 
Mishahara ambayo haijalipwa itakuwa madai, unaposikia walimu wanalia kuhusu malimbikizo yao ni pamoja na hiyo mishahara ambayo haikulipwa, fedha za likizo pamoja na uhamisho.

Kuhusu baadhi ya halmashauri kulipa na nyingine kuchelewa ni kawaida kabisa. Mwalimu anaajiriwa na halmshauri husika, scope ya ajira yake inaishia kwa mkurugenzi wake.

Ukipangiwa halmashauri ya hovyo hata mshahara unaweza kuchelewa sana kwa sababu ya uzembe wa afisa utumishi wa halmashauri yake, kwani yeye ndiye anayeingiza taarifa zako kwenye mfumo wa malipo ya mishahara.

Kuhusu fedha ya kujikimu, nayo kama hawatamlipa itakuwa sehemu ya madai yake.

Kwakifupi halmashauri zetu ni upumbavu mtupu, ukiambiwa uzembe uliopo huko unaweza kupasuka kwa hasira, kuna majitu incompetent kwa namna ya kustaajabisha kabisa.
 
Pole sana kwa hayo yaliyomkuta mdogo wako. Kama ni binti basi kwa huo ukata usishangae ukipata bwana haraka na kutandikwa mimba chap chap. Na kama ni kijana wa kiume hilo usiwaze sana, atapambana kiume hata kuopoa single mother mmoja ambaye ni teacher mwenzake amtunze fresh.
Asante boss
 
Sasa hapo siasa ni ipi?

Kwanza lazima uelewe kuna ambao walichelewa kuripoti na hivyo kusababisha taarifa zao kuchelewa kufanyiwa kazi. Hawa hawawezi kupata salary ya Dec.

Muhimu amepata ajira, elewa tu atapata mshahara wake na kuhusu madai ya fedha za kujikimu kuna watu wana miaka zaidi ya 3 tangu waajiriwe hawajaipata hiyo fedha.

Serikalini kitu kikubwa upate salary yako tu.
 
Unathubutu kuandika mtoto wa baba yako mkubwa alikuwa mzigo, ukimaanisha hakuwa na thamani hapo kwenu, sasa nakushangaa kwanini unauhurumia huo mzigo? Wacha unafiki.
 
Pole sana kwa hayo yaliyomkuta mdogo wako. Kama ni binti basi kwa huo ukata usishangae ukipata bwana haraka na kutandikwa mimba chap chap. Na kama ni kijana wa kiume hilo usiwaze sana, atapambana kiume hata kuopoa single mother mmoja ambaye ni teacher mwenzake amtunze fresh.
Asante boss
Unathubutu kuandika mtoto wa baba yako mkubwa alikuwa mzigo, ukimaanisha hakuwa na thamani hapo kwenu, sasa nakushangaa kwanini unauhurumia huo mzigo? wacha unafiki.
Bila shaka umeshiba kande la huko upareni.Ukisafisha tumbo akili itakaa sawa utaandika kwa utulivu.
 
Hope kila mmoja ameshiba pilau...
Kuwa mwajiriwa mpya kuna mambo mengi bro pengine alichelewa kuripoti akakuta tayari halmashauri wameshatuma payroll inakuwa vigumu yeye kuupata huo mshahara wa mwezi husika , hivyo mshahara wake utakuwa ni limbikizo anaweza akalipwa mwezi unaofuata double salary hvyo mwelekeze awe mvumilivu na afuate maelekezo ya wataalamu hasa kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni[emoji120][emoji120][emoji120]
 
🤣🤣🤣🤣Asante boss
 
Sasa hapo siasa ni ipi?

Kwanza lazima uelewe kuna ambao walichelewa kuripoti na hivyo kusababisha taarifa zao kuchelewa kufanyiwa kazi. Hawa hawawezi kupata salary ya Dec.

Muhimu amepata ajira, elewa tu atapata mshahara wake na kuhusu madai ya fedha za kujikimu kuna watu wana miaka zaidi ya 3 tangu waajiriwe hawajaipata hiyo fedha.

Serikalini kitu kikubwa upate salary yako tu.
Je, waliowahi kuripoti wamepata?
 
Kuwa mwajiriwa mpya kuna mambo mengi bro pengine alichelewa kuripoti akakuta tayari halmashauri wameshatuma payroll inakuwa vigumu yeye kuupata huo mshahara wa mwezi husika , hivyo mshahara wake utakuwa ni limbikizo anaweza akalipwa mwezi unaofuata double salary hvyo mwelekeze awe mvumilivu na afuate maelekezo ya wataalamu hasa kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni[emoji120][emoji120][emoji120]
Sikiliza weweeeeee....

Sisi ndio wataalamu[emoji1][emoji1][emoji1]
 
Back
Top Bottom