Siasa safi imekosekana Jimbo langu la Iramba!

Siasa safi imekosekana Jimbo langu la Iramba!

Mnambua

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2020
Posts
246
Reaction score
233
Mwaka huu ni wa Uchaguzi Mkuu ambao kwa jimbo letu la Iramba tunategemea kumpata Mbunge na Madiwani ambao wataifanya Iramba yetu ijipambanue na kuanza kurudi katika enzi za kuwa Wilaya bora Mkoa wa Singida. Kwa sasa Iramba sio bora tena.

Inazidiwa na watani zetu na inavyoelekea hata Manyoni nayo itatuacha sasahivi kwani zao la korosho linaenda kuwapaisha miaka michache ijayo. Kwa nini Iramba yetu inadidimia? Nitaeleza mambo kadhaa yanayoifanya ishuke na izidi kushuka.

Changamoto kubwa tuliyonayo Iramba ni kukosa siasa safi ambayo imezalisha mambo kadhaa ambayo yanaibainisha Iramba wazi kabisa kuwa Iramba haiwezi kuendelea. Uongozi wa kisiasa kiwilaya mara nyingi unaangalia zaidi Mbunge wa Wilay husika, Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji na Baraza la Madiwani.

Hawa ndiyo wanaweza kuionesha wilaya inafanya vizuri. Kwa upande wa Wakuu wa Wilaya ukweli tangu aondoke yule Dkt Yahaya Nawanda Iramba haijawahi kuwa na Mkuu wa Wilaya ambaye ni mbunifu na mwenye fikra chanya kwa wilaya yetu. Kwa upande wa Wakurugenzi watendaji ndiyo hata usiseme. Hatuna Mkurugenzi Mtendaji ambaye amewahi kuja na ubunifu wa jambo gani aifanyie Iramba zaidi ya wote kuja kujineemesha kwa posho tu. Ndiyo maana hata madai ambayo ni malimbikizo kwa watendaji wa wilaya hii ni makubwa sana.

Kwa upande wa Baraza la Madiwani na Mbunge - kuanzia Mwenyekiti wa Halmashauri hamna hata mmoja ambaye ni mzuri na mwenye uchungu wa Iramba. Hawa wote hawaongei lugha moja na wote wapo katika kujikweza kwa nafasi zao. Wanapigania kuwa na nafasi, yaani vyeo, kuliko wanavyofikiri waifanyie nini Iramba. Wanyiramba wana tamaa sana ya madaraka ndiyo maana hata Mbunge wao Dkt. Mwigulu kabla hata hajafanya vizuri kwenye nafasi ya ubunge kakurupuka kwenye kutaka Urais wa nchi. Hata sasa hicho kinamtesa.

Viongozi wa kisiasa Iramba wamekosa kabisa namna ya kuwaunganisha wananchi katika kuleta maendeleo yao. Imebaki ni wajungu tu - nani anafaa udiwani au ubunge ndiyo imekuwa agenda kubwa na inakosanisha watu. Hamna mtu ambaye anaonwa anafaa kwa wale wanaofaa zaidi ya hawa ambao ni madaraka mongers - Mbunge akikuta watu wanakunywa pombe kilabuni anawaongezea pombe ili wamwone mkarimu.

Mbunge akikuktwa na mzazi maskini anataka fedha ya kumnunulia mwanae wa sekondari sare ya shule anatoa fedha haraka haraka na kumsisitiza asiache kumchagua na mwaka huu. Mbunge haangalii namna ya kumbadili mzazi au kuibadili Iramba kwa ujumla iwe na hali ya kujimudu kiuchumi. Mbunge anatamani Iramba iendelee kuwa dhaifu kiuchumi ili wananchi wake wawe wanyonge tu siku zote - anajiandaa kuwapelekea sare za CCM na wala sio kuwapelekea maendeleo.

Viongozi hawa wanakwepa sana kuunganisha nguvu za pamoja za wazawa wa Iramba wenye uwezo kiuchumi, walioelimika vizuri na wenye nafasi Serikalini ili kuweza kuangalia namna ya kuibadili Iramba. Hawa watu wangepata Maratibu wa kuwaweka pamoja si ajabu leo Iramba ingekuwa hata na Benki yake ya Maendeleo. Imebaki malumbano tu kati ya Dkt. Mwigulu na Prof. Kitila. Hawa wote hawafai kwa sababu wapo kwenye siasa za kitaifa zaidi. Tena Prof. Mkumbo ndiyo bure kabisa kwa sababu always anafanya mambo yake kwa kujipendekeza na ni mbahili kupita Dkt. Mwigulu - though wote ni wabahili.

Watu wazuri Iramba wanaogopa hata kugombea nafasi kwa sababu ya kuogopa tabia ya WanaiRamba kuoneana wivu na kunafikiana katika nafasi za uongozi. Kuna siku niliongea na ndugu yangu aliyepo Uingereza ambaye alinitangulia kusoma pale Moshi Tech - Tomaso Neligwa akaniambaia anatamani kuifanyaia kitu Iramba lakini anasita kujitokeza kwenye mazingira ambayo anaweza kuonewa wivu na kunafikiwa na WanaIramba wenye chuki binafsi kwa watu.

Watu ambao ni wazuri na makini katika kuleta maendeleo ya Iramba kama William Shila wa Ulemo, Richard Mkumbo wa Kinampanda, Jumbe Katala wa Kisiriri, Zaipuna Yona wa Kisiriri, Timothy Lyanga wa Ndago, Brigedia Kitundu wa Ndago, Kitandu Ugula wa Kyengege, Kanali Kingu aliyekuwa Katibu Mkuu Mambo ya Ndani, Mapinduzi Urembo wa Ruruma na wengine ambao hawana tabia za kujivuna na kugombania madaraka kawa waliopita na waliopo.

Tangua enzi za Mbunge Leonard Shango mpaka leo hii wabunge wote hao wamekuwa ni watu wenye tamaa ya madaraka na waendesha chuki na figisu jimboni. Juma Kilimba aliingia kwenye ubunge sababu hiyo hiyo ya kuchukiana, vivyo vivyo hata Dkt. Mwigulu amabaye alionekana atawaunganisha WanaIramba lakini mapaka sasa kakakwama kwa sababu aliwafanya wananchi kama sehemu ya kukanyagia ili aufikie Urais.

Namalizia kuwa bila Iramba kupata mtu wa kuwaunganisha wawe wamoja Iramba itazidi kudidimia kwa sababu siku zote kwa kuingiza kwetu viongozi wasiofaa kuanzia madiwani na mbunge ndiyo tunakaribisha tabia ya kuletewa Wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya wasiofaa. Tufungue macho Iramba, tutafute watu wanaotufaa tuwashawishi wagombee uongozi, tuachane na hawa waliojawa na akili ya kujinufaisha wao kwa kupitia wapiga kura.
 
Kuwa , makini msije kuuwana kisa udiwani na Ubunge ,,,wewe umetumwa namkumbo hila Njaa itakumaliza mkuu , tafuta kazi ya halali siasa chafu zitakuuwa bure.
Wala! Nimejituma mwenyewe Mkuu! Prof. Kitila unamjua wewe? Hawezi hata kukunulia soda au pipi! Vijiji vyetu jirani sana na namjua toka nitoke!
 
Unauliza kwa Timu zilizoonesha nia ama?

Mbali ya maneno mengine mazuri uliyoongea na ushauru mujarabu ulioutoa, ni kweli huko Iramba hamna siasa safi,maana mwigulu ndio kioo cha wanasiasa toka Iramba. Huyo jamaa ni mtu wa siasa chafu sana, na hawezi kubadilika zaidi ya kumpiga chini ili mchague kweli mtu wa siasa safi.
 
Ndio hivyo mkuu
Tumewaambia tumewashindwa
Pale kitawaka tu hamna namna
Wanyiramba wanaumana
Hapana! Mimi mauongozi ya kisiasa najiona kabisa sitoshi - ni darasa la saba la zamani ingawa nilibahatika kuajiriwa na nilipona kuondoshwa kwa vyeti feki kwa sababu sikuficha kuwa mie ni la saba kaka!
 
tunawatakia kila la kheri kwenye huo mtifuano.
 
Hapana! Mimi mauongozi ya kisiasa najiona kabisa sitoshi - ni darasa la saba la zamani ingawa nilibahatika kuajiriwa na nilipona kuondoshwa kwa vyeti feki kwa sababu sikuficha kuwa mie ni la saba kaka!
Na Moshi Tech ulienda na Cheti Feki Cha Form Four!
 
Mwaka huu ni wa Uchaguzi Mkuu ambao kwa jimbo letu la Iramba.

... Wanyiramba wana tamaa sana ya madaraka ndiyo maana hata Mbunge wao Dkt. Mwigulu ...

Lengo kuu la ubunge ni mbunge ale, wala si kuleteana maendeleo.

Lile bunge lililo chini ya CCM hakuna hata siku moja litakuja kuwa bunge kwa maslahi ya wananchi.
 
Nlishakosa hamu na Iramba yetu, sijui kuna tatizo gani,miaka nenda rudi badala ya kwenda mbele tunarud nyuma
Sema wanyiramba nao sijui tukoje
Tunaishiaga kupewa kanga na kofia au yale matishet tunauza kura
Weiiii basi tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Tunashangaza sana. Ila tuache basi kulalamika mie nimependekeza tuangalie watu ambao wanaweza kututoa kimasomaso. Watani zetu WaNyaturu wanatupita sasahivi
 
Mbunge wa Iramba Magaribi mwaka huu ni Daudi Mjungu, kwa sasa ni Mratibu elimu kata old kiomboi. Nimenasa tetesi huyu kijana anajipanga kimyakimya na migogoro baina ya miamba inaweza kumpaisha kama ilivyotokea kwa Magufuli 2015. Subirini muda mtaamini.
 
Back
Top Bottom