Siasa tunazoziona leo KENYA ni zilezile za Kikwete na Lowassa

nashicha

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2021
Posts
279
Reaction score
524
Siasa tunazoziona leo KENYA ni zilezile za Kikwete na LOWASSA Rutto alikuwa maarufu zaidi ya Kenyatta kwenye Siasa lakini akaombwa amsaidie ili apate miaka kumi na KENYATTA aje amsaidie nae kupata URAIS

Lakini leo hii Kenyatta anamgeuka na kumuunga mkono ODINGA HUKU AKISAHAU KWAMBA RUTO ALITUMIA NGUVU SANA NA PESA NYINGI KUMFANYIA KAMPENI HII NI SAWA na KIKWETE alivyomfanyia LOWASSA

MAANA aliyekuwa maarufu zaidi alikuwa Lowassa ila akakubali kurudi nyuma wakati huo wakiitwa BOYZ II MEN na kutumia nguvu nyingi sana akijua baada ya KIKWETE angefuata

Lakinj kwa roho ileile ya Kenyatta kikwete akamkataa lowassa na kumtaka MEMBE ugomvi wao ulizaa mpasuko ccm kama sio wazee chama kilitaka kumfia kikwete lakini zao lake tulikuja kupata VIONGOZI WASIOELEWEKA KATIKA NCHI YETU KINA BASHIRU KINA POLEPOLE KINA SABAYA KINA MAKONDA NA KUBWA ZAIDI TUKAPATA KIONGOZI DIKTETA

LAKINI KWA KENYA CHA TAWALA CHA JUBILEE KIMEKUFA BAADA YA KUWAPATA KINA MURATHE TUJU NA WENGINEO KUNA CHAKUJIFUNZA HAPA HASA KWA WANASIASA KUWA UNAFKI UNAWEZA KULITUMBUKIZA TAIFA KATIKA MACHAFUKO MAKUBWA SANA KENYA SASAHIVI RAIS NA MAKAMU WAKE HATA KUSALIMIA HAWASALIMIANI

LEO HII KIKWETE NA LOWASSA HATA KUKARIBISHANA NA WATOTO WAO KULA PAMOJA HAIWEZEKANI TENA
 
Ya Ngoswe mwachie Ngoswe! Wakati mwingine unaweza kuadhani kuwa mtu fulani ana uwezo sana ila ukishaanza kufanya naye kazi kwa karibu ndipo unagundua kuwa ni mtupu na kuji;laumu kuwa kwa nini ulimteaua! Ya Ngoswe mwachie Ngoswe!
 
Rutto alikuwa na ushawishi tu, ila hakuwa na fedha nyingi by then, sijui unaelewa tofauti, Rutto ameanza kupata fedha baada ya kuiba sana akiwa Makamu wa Rais, Lowassa ni kitu kingine. Lowassa is the tycoon.

Sema Uhuru Kenyatta ni tajiri zaidi ya Lowassa na nani tajiri wa pili nchini Kenya, yaani Baada ya Moi & Family, familia ya Uhuru Kenyatta inashika utajiri namba 2 nchini Kenya. Alafu inafuata Nicolaus Biwott, alafu Mhindi yule mwenye Bidco Refineries.

DP Rutto kwa sasa baada ya kupata uDP ndio katajirika sana, ila bado hamfikii Lowassa
 
Kinachoonekana baina ya Uhuru na Ruto ni kukosekana kuaminiana. Uhuru hana imani na Ruto anamuona kama mtu hatari anayeweza kumbadilikia akishakaa kwenye kiti na kumtia misukosuko.

Na ktk kukabiliana na hilo ndipo amemgeukia Odinga mwana wa Jaramogi. Huyu anamuamini kuliko Ruto. Hawa wote wawili wametokea kwenye familia kubwa mbili Kenya zenye majina ambayo yameendesha siasa za Kenya toka Uhuru hadi sasa. Na kwa hali inavyokwrnda Uhuru ndo anaenda kushinda ktk hili dhidi ya Ruto.
 
Rutto alikuwa na ushawishi tu, ila hakuwa na fedha, sijui unaelewa tofauti, Rutto ameanza kupata fedha baada ya kuiba sana akiwa Makamu wa Rais, Lowassa ni kitu kingine. Lowassa is the tycoon.
Sidhani kama Lowasa anamkuta Ruto kwa utajiri na uwekezaji that is a fact
 
Rutto alikuwa na ushawishi tu, ila hakuwa na fedha, sijui unaelewa tofauti, Rutto ameanza kupata fedha baada ya kuiba sana akiwa Makamu wa Rais, Lowassa ni kitu kingine. Lowassa is the tycoon.
Ruto alikuwa na kila kitu,Ruto anajulikana Kama self made king.Alishakuwa na vyeo vingi.Alishakuwa makamu wa rais miaka ya mwisho ya Mzee Moi.Rutto alikuwa taniri balaaa.
 
kuna nyakati kikwete hujutia sana kumtosa lowassa maana waliempa dhamana aliwapeka mpera mpera kweli kweli
 
Aliyenzisha kundi la mtandao ndiye aliyelivunja kundi la mtandano, shamba la bwana kheri mbuzi wa bwana kheri..

Unaweza kuwa na hela lakini usiwe mjanja na mwenye akili na maarifa ya kimtaa, Hivi vitu EL hana na JK anavyo...JK aliamua kujali maslahi ya nchi na kumuangusha swaiba wake..
Mwanzoni wote walitegemeana, mmoja alitaka kutumia umaarufu na ushawishi wa mwenzie ndani ya chama na kukubalika kwake mtaani amfanye ngazi na mwingine alitegemea mipango ya upatikanaji wa hela na hela akawa rais..
 
Kinachoonekana baina ya Uhuru na Ruto ni kukosekana kuaminiana. Uhuru hana imani na Ruto anamuona kama mtu hatari anayeweza kumbadilikia akishakaa kwenye kiti na kumtia misukosuko.

Na ktk kukabiliana na hilo ndipo amemgeukia Odinga mwana wa Jaramogi. Huyu anamuamini kuliko Ruto. Hawa wote wawili wametokea kwenye familia kubwa mbili Kenya zenye majina ambayo yameendesha siasa za Kenya toka Uhuru hadi sasa. Na kwa hali inavyokwrnda Uhuru ndo anaenda kushinda ktk hili dhidi ya Ruto.

Kuna wakati inakupasa uangalie maslahi ya nchi kwanza na kuweka uswaiba pembeni....kwa siasa za Kenya zilivyo.....inapaswa waluo wapozwe kwa kupewa nchi kujaribu kuneutralize ukabila wa wakalengin na Wakikuyu...
 
Tofauti ya wanasiasa wa Kenya na Tanzania, wanasiasa wengi wa Tanzania wanapata hela na kuwa matajiri wakiwa tayari kwenye siasa na kupitia hiyo siasa kwa maana ya madili, wanasiasa wa Kenya wengi wao wanaingia kwenye siasa tayari wakiwa matajiri na wanainvestment nyingi....na huo mfumo ndio unafanya siasa za Tanzania kuwa za hovyo..
 
Siasa tunazoziona leo KENYA ni zilezile za Kikwete na LOWASSA Rutto alikuwa maarufu zaidi ya Kenyatta kwenye Siasa lakini akaombwa amsaidie ili apate miaka kumi na KENYATTA aje amsaidie nae kupata URAIS

Lakini leo hii Kenyatta anamgeuka na kumuunga mkono ODINGA HUKU AKISAHAU KWAMBA RUTO ALITUMIA NGUVU SANA NA PESA NYINGI KUMFANYIA KAMPENI HII NI SAWA na KIKWETE alivyomfanyia LOWASSA

MAANA aliyekuwa maarufu zaidi alikuwa Lowassa ila akakubali kurudi nyuma wakati huo wakiitwa BOYZ II MEN na kutumia nguvu nyingi sana akijua baada ya KIKWETE angefuata

Lakinj kwa roho ileile ya Kenyatta kikwete akamkataa lowassa na kumtaka MEMBE ugomvi wao ulizaa mpasuko ccm kama sio wazee chama kilitaka kumfia kikwete lakini zao lake tulikuja kupata VIONGOZI WASIOELEWEKA KATIKA NCHI YETU KINA BASHIRU KINA POLEPOLE KINA SABAYA KINA MAKONDA NA KUBWA ZAIDI TUKAPATA KIONGOZI DIKTETA

LAKINI KWA KENYA CHA TAWALA CHA JUBILEE KIMEKUFA BAADA YA KUWAPATA KINA MURATHE TUJU NA WENGINEO KUNA CHAKUJIFUNZA HAPA HASA KWA WANASIASA KUWA UNAFKI UNAWEZA KULITUMBUKIZA TAIFA KATIKA MACHAFUKO MAKUBWA SANA KENYA SASAHIVI RAIS NA MAKAMU WAKE HATA KUSALIMIA HAWASALIMIANI

LEO HII KIKWETE NA LOWASSA HATA KUKARIBISHANA NA WATOTO WAO KULA PAMOJA HAIWEZEKANI TENA
Ruto kajisahau sana kiasi hana heshima kwa rais wake na kuanza kumtweeza mbele za watu.

Nakuhakikishia Ruto urais mwaka 2022 atausikia kupitia radio citizen tu .
 
Rutto alikuwa na ushawishi tu, ila hakuwa na fedha, sijui unaelewa tofauti, Rutto ameanza kupata fedha baada ya kuiba sana akiwa Makamu wa Rais, Lowassa ni kitu kingine. Lowassa is the tycoon.
Ruto hadi jana ana miliki chopa 5 mali yake halali.

Na sioni kwa sasa kama bado anao mvuto baada ya kuanza kumshambulia rais Uhuru.
 
Kinachoonekana baina ya Uhuru na Ruto ni kukosekana kuaminiana. Uhuru hana imani na Ruto anamuona kama mtu hatari anayeweza kumbadilikia akishakaa kwenye kiti na kumtia misukosuko.

Na ktk kukabiliana na hilo ndipo amemgeukia Odinga mwana wa Jaramogi. Huyu anamuamini kuliko Ruto. Hawa wote wawili wametokea kwenye familia kubwa mbili Kenya zenye majina ambayo yameendesha siasa za Kenya toka Uhuru hadi sasa. Na kwa hali inavyokwrnda Uhuru ndo anaenda kushinda ktk hili dhidi ya Ruto.
Nakubaliana na wewe kwa 100% na tayari naona kwa mara ya kwanza Raila Odinga anaenda kushinda urais wa kenya tena kiulaini sana
 
Siasa tunazoziona leo KENYA ni zilezile za Kikwete na LOWASSA Rutto alikuwa maarufu zaidi ya Kenyatta kwenye Siasa lakini akaombwa amsaidie ili apate miaka kumi na KENYATTA aje amsaidie nae kupata URAIS

Lakini leo hii Kenyatta anamgeuka na kumuunga mkono ODINGA HUKU AKISAHAU KWAMBA RUTO ALITUMIA NGUVU SANA NA PESA NYINGI KUMFANYIA KAMPENI HII NI SAWA na KIKWETE alivyomfanyia LOWASSA

MAANA aliyekuwa maarufu zaidi alikuwa Lowassa ila akakubali kurudi nyuma.

Una umri gani?

Ni kweli 2015 Lowassa alimzidi Kikwete umaarufu? Kikwete huyuhuyu aliyeamua kusamehe kumwachia Mkapa kumridhisha Nyerere 1995 alizidiwa nini na Lowassa? Alichofanya Kikwete 2005 ni kuimarisha coalition yake ndani ya Chama dhidi ya wagombea wengine na Lowassa asingeweza kumsumbua Kikwete mwaka ule 2005 mzee wa Msoga alishaunda chaini 10yrs back.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Kuna wakati inakupasa uangalie maslahi ya nchi kwanza na kuweka uswaiba pembeni....kwa siasa za Kenya zilivyo.....inapaswa waluo wapozwe kwa kupewa nchi kujaribu kuneutralize ukabila wa wakalengin na Wakikuyu...
Nani kakudangsnya huyo? Mkikuyu hasingependa kamwe on earth Mluo achukue nchi hii imetokea kwa vile Ruto haeleweki. Mkikuyu anamemwsmini Mkalenjini tangu enzi ila sio Mluo. Ila katika mazingira yaliyopo kwa wakati huu sasa ni ishu ya familia 2 to decide the future of the nation. Wakikuyu wengi hawapendi ila Mwigai mwana wa Jomo anao ushawishi miongoni mwa Wakikuyu wengi kwa sasa. KANU wanataka kumleta Gideon Moi Mkalenjini mwenzie na Ruto lakini haisaidii Mwigai hamjui vizuri Moi. Kwa Odinga anaiona future yake iko secure zaidi.
 
Nimeupuuza uzi na kuacha kuendelea kusoma zaidi pale tu uliposema eti Lowasa alikuwa maarufu zaidi ya Kikwete,hii sio kweli ukweli ni kwamba kati 1995 hadi 2005 wakati Kikwete anachaguliwa kuwa Rais alikuwa maarufu zaidi ya Lowasa labda ungesema umaarufu wa Kikwete ulipungua baada kuingia kwenye utawala.
 
Nani kakudangsnya huyo? Mkikuyu hasingependa kamwe on earth Mluo achukue nchi hii imetokea kwa vile Ruto haeleweki. Mkikuyu anamemwsmini Mkalenjini tangu enzi ila sio Mluo. Ila katika mazingira yaliyopo kwa wakati huu sasa ni ishu ya familia 2 to decide the future of the nation. Wakikuyu wengi hawapendi ila Mwigai mwana wa Jomo anao ushawishi miongoni mwa Wakikuyu wengi kwa sasa. KANU wanataka kumleta Gideon Moi Mkalenjini mwenzie na Ruto lakini haisaidii Mwigai hamjui vizuri Moi. Kwa Odinga anaiona future yake iko secure zaidi.

ndio maana nikakwambia kwa maslahi ya nchi, ita better Luo wakapozwa kwa Odinga kupewa..
 
Back
Top Bottom