Siasa tunazoziona leo KENYA ni zilezile za Kikwete na Lowassa

Ruto haamini anachokiona. Ila kaamua kusonga mbele bila kuungwa mkono na Kenyata. Ila Kenyata ndo ataamua nani awe Rais.
 
Kichwa yako hovyo Sana, eleza mwanasiasa wa Tanzania aliyetajirika kwa kupitia siasa, tueleze anamiliki utajiri kiasi gani na amewekeza katika nini?, Weka ushahidi.
 

msamehe tu, wengi siasa wamezianza jana..

sidhani kama anajua 1995 pale chimwaga bila ya JKN kupindua meza JK alibeba ndoo na BWM tungemsikia tu kwenye bomba.... Hekima za JKN na usikivu wa JK vilileta utulivu..

Wengi hawajui kama JK alilelewa kwenye chama na ni mmoja wa vijana ambao JKN alikuwa akiwakuza na kuwaamini pia akiwemo Seif Sharif Hamad...Kiukweli umaarufu na ushawishi wa JK ulikuwa mkubwa sana 1995 and up, ndani ya chama na mtaani pia..nafikiri ni nyota tu na aina ya maisha ya JK aka mzee wa saigon.
 
Ruto haamini anachokiona. Ila kaamua kusonga mbele bila kuungwa mkono na Kenyata. Ila Kenyata ndo ataamua nani awe Rais.
Labda apewe tu....lakini wananchi wakikomaa...Asee Ruto anao watu acha kabisa....kuna uwezekano raila kusalitiwa....Kenyatta hana ushawishi kabisa dada....oka yenyewe mpaka sasa hawamweshimu
 
Kama uhuru atajaribu kupora ushindi wa Ruto na kumpa Raila 2022 yatatotokea ya 2007,Ruto sio mwanasiasa mjinga kama hawa wetu,ni mtu Mwenye nguvu ya ushawishi kuliko yeyote kenya kwa sasa.
Hajawahi shindwa,yeye ndio aliyefanya Raila kuwa PM na Kenyatta kuwa president kwa miaka 10 ,kinamzuia nini yeye kuwa president?
 
2022 battle itakuwa tough sana lakini Ruto atashinda tena kwa margin kubwa tu.
 
Atakosa kura za wa kikuyu.
 
Wewe ni mtanzania au mkenya?, jaribu kuwa makini katika kuzungumza siasa za Kenya, sio vizuri kuegemea upande mmoja kwenye siasa za nchi Jirani.
 
Wewe ni mtanzania au mkenya?, jaribu kuwa makini katika kuzungumza siasa za Kenya, sio vizuri kuegemea upande mmoja kwenye siasa za nchi Jirani.
Kuzungumza vizuri vipi tena....analysis zinaonesha kama mwamba alivyoeleza....ingia YouTube uone utaelewa
 
Yaani kikuyus wampigie kura mluo? Serious
Au 2022 kutakuwa na candidate mwingine Mwenye nguvu tofauti na WSR vs RAO?
Mbona walimpigia Raila kipindi yupo pamoja na Uhuru Kenyata vs Mwai Kibaki ?Sema Kibaki akaiba Urais. Uhuru Kenyata akimuunga mkono Raila Odinga kazi kwisha. Wakikiyu wanafuata maneno ya Uhuru Kenyata.
 
Ruto kajisahau sana kiasi hana heshima kwa rais wake na kuanza kumtweeza mbele za watu.

Nakuhakikishia Ruto urais mwaka 2022 atausikia kupitia radio citizen tu .
Hata Lowassa kwny kampeni 2015 alikua anasema huyu rafiki yangu(JK) uchumi ameuvuruga hajavuruga? Alikua anamtweza rafiki ndio maana pengine urais aliusikia kupitia ITV.
 
Ruto hadi jana ana miliki chopa 5 mali yake halali.

Na sioni kwa sasa kama bado anao mvuto baada ya kuanza kumshambulia rais Uhuru.
Aisee mbona chopa Ni Bei ya kawaida tu kwa madogo?Hicho sio kitu Cha kujitambia mbele ya madon.
 
πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„ JK hakuwahi kumpenda ticha hata siku 1 hata kumuita Baba wa Taifa aligoma kabisa kabisa,anaishia tu kumuita Mwl πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„.
 
Hata Lowassa kwny kampeni 2015 alikua anasema huyu rafiki yangu(JK) uchumi ameuvuruga hajavuruga? Alikua anamtweza rafiki ndio maana pengine urais aliusikia kupitia ITV.
Kwahiyo unakubali kuwa Ruto ataangukia pua this time?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…