Siasa ya chikichi vs korosho mkoani Kigoma

Siasa ya chikichi vs korosho mkoani Kigoma

Tangantika

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2018
Posts
5,586
Reaction score
7,087
Wasalamu bandugu.

Naomba Leo niongee kidogo kuhusu zao la chikichi mkoani kigoma. Watanzania wote tunafahamu kuwa Chikichi inastawi zaidi kigoma na mikoa ya pembezoni mwake.

Ukweli ni kwamba zao hili halijaleta tija/maendeleo makubwa kama linavyovuma, hii inatokana na sababu nying ambazo sio lengo kuzijadili hapa.

Jambo kubwa nalotaka tujadili ni jinsi viongozi wanavyopigia chapuo watu walime kwa wingi sana zao hili(Ni jambo zuri) ila kuna maswali mengi ya kujichikichi!.Kwa nini viongozi wamelishikilia watu walime sana chikichi,lengo ni nini?

2. Wameboresha nini kwa mazao yanayovunwa sasa kabla ya kupanda miti mingi zaidi?

3. Upandaji wa chikichi ni mpango wa kisera au mhemko/ utashi wa viongozi w juu

4. Zao chikichi limefanyiwa tafiti za kutosha?

7. Kuna mkakati gani uliondaliwa wa kuwasaidia wakulima au ni kuwagawia tu miche kushne

8. Kwa nini viongozi wanasiasa wapigie chapuo chikichi na kuacha ,Kahawa,miti ya mbao,tangawizi,alizeti,miwa,ndizi,mifugo nk.Kigoma inastawi mazao mengi ya biashara.

9. Kuna mkakati gani wa kiviwanda wa kuchakata mazao ya chikichi

11. Mafuta kama zao kuu la chikichi yanapendwa na watanzania?

Maswali ni mengi sana.
Nilipotembelea kigoma,niliongea na wazee kuhusu mwenendo wakilimo cha biashara.Nilichogundua ni kwamba wakulima wengine hawaliungi mkono wazo la kupanda chikichi bali wameamua kupanda KOROSHO.

Wanasema kwamba Chikichi inapigiwa chapuo kuwapumbaza wasipande KOROSHO,kwanini?

Wanasema kwamba "KIONGOZI" anaewahamasisha kupanda chikichi kwao kuna KOROSHO nyingi hivyo basi hataki ushindani utokee unaoweza kushusha bei ya KOROSHO na ukanda wake hauna mazao mengine ya kudumu kama kigoma, hivyo basi anatumia nguvu nyingi na mamlaka kuhakikisha kigoma wanapandaCHIKICHI na hawapandi KOROSHO(sijui kweli!!!) ili uzalishaji wa korosho uwe chini na wanunuzi hawatavutiwa kwenda huko('mhiiii!!! is it true wazee? )watu wanajua kufukunyua.

Hawa wazee wanajiuliza mbona wilaya nyingi tu Tanzania zinahali inayoruhusu Chikichi kustawi ila amekazania tu kigoma!!! watu wa kigoma nao maswali maswali tu

Wanasema mkuranga,morogoro,mbeya katavi tabora chikichi inakubali.Halafu anahimiza tu kupanda bila kujali wapi panastawi zaidi na wapi hapastawi,yani yeye ni panda tu,panda tu, sio kigoma yote inastawi chikichi.Aisee hawa wazee noma.

Naomba niishie kwanza hapa nitaiendeleza sitaki niwachoshe sana
 
Back
Top Bottom