Juzi ulileta mada ya kuwaponda wakenya, wakakushambulia nusu wakutowe macho. Leo umeleta mada ya kuwasifia, wamepotea.
Unaposema Kenya wanachagua mtu anaewaletea maendeleo, nadhani unaangalia siasa za Kenya juu juu. Kenya politics is exclusive, its for the elite people. Wanaofanikiwa kujikita kwenye siasa ni wenye pesa mifukoni, ni watu walijijengea makundi ya kumlida na kuhakikisha anashimda no matter what. Huwezi kufanya siasa Kenya ukiwa mikono mitupu. Wakati hali ni tofauti na Tanzania ambapo unaweza ukawa mtu wa hali ya kawaida au hata ya chini, lakini ukachagama mpaka ukawa Rais wa Tanzania.
Siasa za Kenya mnaziamgalia kwa jicho la husuda, lakini, hazilindi kila jamii, waturkana atapigamia cha Turkana tuu, wamombasa atapigania cha Mombasa tuu, hakuna kupigania taifa zima kwa pamoja. Wanakuwa wamoja pale tuu jina la Kenya linapopakwa matope, vinginevyo kila mtu kivyake.
Mbunge au governor kukaa muda mrefu sio kipimo cha kusema demokrasia ni ya kweli au sio ya kweli. Mbona nchi zilizokomaa kidemokrasia kama Marekani na Uwingereza Kuna wabunge wengi wamekuwa katika nafasi zao kwa miaka mingi tuu?? There's something called "safe seat" yani jimbo lisilo tetereka, wananchi wameridhika na mbunge wao au kiongozi wao.