Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Habari za Jumapili Wanabodi,
Kati ya maeneo ambayo inawezekana Tanzania hatujaweza kuyatumia vizuri kunufaika kiuchumi basi ni hili eneo la Siasa ya kutofungamana na Upande Wowote
Sote tumeona jirani yetu Kenya anavyonufaika na msimamo wake wa wazi wa kuegemea upande wa Magharibi (West) ambapo kwa sasa makampuni makubwa ya Ulaya na Marekani yanafungua Ofisi zake za Afrika nchini Kenya mfano Benki ya JP Morgan, Microsoft, BBC, Google na mengineyo mengi.
Tanzania tunajinasibu sana kuwa na siasa ya kutofungamana na upande wowote ila kiuhalisia tumeegemea sana China ambapo hata hivyo hatujatumia akili zetu vizuri kumfanya hata afungue makampuni yake makubwa nchini kwetu.
China ana benki kubwa kama HSCB ambayo ndiyo inasemwa kuweza kulinganishwa na Benki ya Marekani ya JP Morgan. Ila hadi sasa hatujaweza hata kuwashawishi wafungue tawi lake kwa Afrika hapa Tanzania.
Kwa urusi wanafanya biashara kubwa sana ya Gesi ulaya ila kwetu sisi kila siku tunaagiza mafuta, hatujaweza hata kumshawishi Mrusi kutengeneza mtandao wa usambazaji wa Gesi kwa Tanzania ili tuwe na matumizi ya gesi nchini mwetu na kuondokana na utegemezi wa mafuta kutoka nje ya Tanzania.
Nilitegemea kwa msimamo wetu wa kutofungamana na upande wowote Nchi yetu ndo ingekuwa kinara wa uwekezaji wa mataifa ya Ulaya, Marekani, Urusi na China.
Nilitegemea Makampuni ya Marekani, China, Ulaya na Urusi ndo yangekuwa na uwekezaji mkubwa hapa Tanzania kuliko nchi nyingine yeyote ile kwa sababu sie hatuna upande na tunawakaribisha wote.
Rai yangu kwa think tank wa Tanzania. Acheni kuwaza ndani ya boksi, anzeni kuwaza nje ya boksi. Tanzania inaweza kuwa Economic power kwa Afrika na Dunia endapo mtawaza vizuri na kuendekeza mambo mazito kwa uchumi wetu. Tanzania kulifanyia kazi hili wazo.
Tanzania ndiyo inapaswa kuwa centre ya uwekezaji mkubwa wa Magharibi na Mashariki kwa hapa Africa. Tumieni akili zenu kuwaza vyema kwa faida ya nchi kiuchumi kwa vizazi vingi vijavyo.
Lord Denning
Mwanza.