Siasa za El nino : Hapo ulipo kuna mvua ,jua kali au upepo ?

Huku ni jua kali mixer joto halafu mavingu mbaali
 
Tanga imepiga asubuhi sana,muda huu jua linalipiza kisasi.
 
Ndipo uelewe kwanini watu wanahifadhi vyakula na serikali haijafungua mipaka ,mikoa kama saba watapata athari za mvua lkn matokeo mingine elewa elnino sio mvua pekee ,kwa nyanda za juu kusini wanaweza kuthiriwa na ukame,au mafuriko.
Kama una mtu wa makamo muulize kilichotokea 98 !
 
Eemm namimi nieleweshe mkuu kwaivo hata ukame unaweza kuitwa elnino
El Niño ni mfumo wa mabadiliko ya hali ya hewa ya asili unaosababishwa na kuongezeka kwa joto la maji ya bahari kuliko kawaida katika eneo la kati na mashariki mwa Bahari ya Pasifiki ya Kitropiki.
Athari za zaweza kuwa:
○Mvua kubwa kupita kiasi
○Upepo mkali kupita kiasi
○Joto kali kupita kiasi/ukame/moto wa nyika
○Mabadiliko ya majira/tabia nchi n.k
○magonjwa kama kichocho,kipindupindu,maleria n.k
○Uharibifu wa miundombinu kama barabara,madaraja,nyumba n.k(uharibifu huu unaweza kusababishwa na mvua au upepo)
 
wakati wa Nuhu,
ubishi na madharao dhidi ya maonyo na tahadhari yalipindukia.

huenda,
athari za Elnino hii ya mwaka huu 2026 zikavunja record ya 1998 kwa athari na madhara.
Na Elnino hii haihitaji mvua, vimbunga, jua kali na ukame wa zaidi ya mwezi moja, ni wiki3 tu kila moja anaweza kupiga mayowe hadi sauti ikatike yenyewe 🐒
 
Ni bora kusema "Mungu Yupo" na ukifa ukakuta hayupo, hakuna noma na ukimkuta mnaelewana maana ulimkubali.

Msala ni pale unasema "Mungu Hayupo" halafu ukifa unamkuta Mwamba yupo anakucheki!

Ni bora kuwe na Maandalizi kuwa El Nino ipo. Isipokuwepo, poa. Ni jambo jema na balaa limetuhepuka kuliko kusema hakuna El Nino haipo halafu ikaja hatujajiandaa!

Kwa Maandalizi haya El Nino binafsi naipongeza sana Serikali!
 
Tulia wewe kapuku chawa
 
Na jinsi Wabongo tulivyo wapumbavu, mvua kidogo tuu Utasikia El Nino ishaanza ahh nakereka kinoma nikisikia huo upuuzi

Waliopiga yale mabilioni wakisikia hvy wanafurahi wanaona Hawa manyumbu washaingia mkenge
 
Broo umekariri elnino sio mvua pekee bali hata ukame ,upepo mkali(vimbunga ,tsunami), au hata mafuriko ,hali ya ukame yaweza tokea pale ambapo majira ya mvua yatahama au yasiwepo kabisa .
Ukame siyo Elnino. Ni La nina. Elnino ni mvua, wewe ndo umekariri
 
Jinsi mamlaka husika wanavyotoa habari ni kama tinatishana,inapaswa water eliminate vizuri
 
Mungu atusaidie isiwe kweli ila kuna kitu nimeona I hope hakihusiani na hizi mvua labda ni mawazo tu sababu inaongelewa sana ila kama kinahusiana hizi mvua nahisi zitakuwa mbaya yatakuwa mafuriko mabaya kuwahi kutokea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…