Siasa za hovyo sana za kuwafanya wapenzi wa mpira mazuzu

Cashman

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2018
Posts
3,017
Reaction score
5,294
Sikuwahi kujua kama viongozi wa hivi vilabu vikubwa wanawadharau kiasi hiki mashabiki wao.

Kitendo cha kumleta Manzoky ili kuwarubuni wapiga kura ni cha kusikitisha sana.
Ninakumbuka aliyewahi kuwa kiongozi wa Simba alivyowaita wapenzi wa Simba mbumbumbu.
Nahisi kila kiongozi huambiwa neno hilo anapokabidhiwa madaraka,ndio maana watu wanaweza kufanya siasa za kitoto au niite za kijinga sana ili tu wapate kura.

Ningekuwepo Leo,ningepiga kura ya hasira dhidi ya dharau kama hizi.
Hii ni dalili ya ubabaishaji mkubwa

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Unaweza ukadhani una akili kumbe wewe ni zuzu.
Nani kamleta Manzoki? Hujui

Uwepo wa Manzoki pale kuna mgombea atanufaika moja kwa moja? Hapana

Alipopewa nafasi ya kuongea kasema nini? Hujui.
Vipi Ibenge na yeye kaja kwa ajili kiongozi apate kura? Huna jibu.
Usikurupuke kujudge vitu na kutafuta wapi fulani kakosea., hii ni mbaya sana.
 
Sasa manzoki amekuja kufanya nini kama sio siasa? Hivi hujuI Ameletwa na nani kama sio kiongozi anaetetea nafasi yake!
 
Ndio vitu wanavyopenda Madunduka🤣🤣🤣🤣 ujinga ujinga tu
 
We kweli mbumbumbu original,hata kama huelewi hata macho yako hayaoni?
 
Mkuu unatetea ujinga, fullstop!

Mnaacha kumleta Manzoki wakati wa usajili aje acheze unamleta siku ya uchaguzi aongee kwenye kampeni, na wewe unaona ni sawa kabisa?
 
Mkuu unatetea ujinga, fullstop!

Mnaacha kumleta Manzoki wakati wa usajili aje acheze unamleta siku ya uchaguzi aongee kwenye kampeni, na wewe unaona ni sawa kabisa?
Sitetei ujinga, ila ukiniambia uwpo wa manzoki unamnufaisha nani na kwanini, ndio tutaelewana.
 
Kiukweli hasta Mimi mwenyewe nimeshangaa sana

Huyo kiongozi aliyefanya hivyo alitaliwa alimwe kichwa mapema sana
 

Nyie wenye akili timamu hata Kadi Huna, hata mpiran huendi, hata michango hutoi

Wale wenye akili ambazo ww unaona za kizuzu ndio hao wenye kadi hai, wanaenda uwanjani, na wanalipa michango

So waache waenjoy wanachokisikia ndio wanachokipenda
 
Mwenye kiti wetu msaafu Aden Rage alishasema wanasimba wote ni mbumbumbu, Sasa Mangungu anapitia mulemule[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Ila Simba tuna nini jamani? Mbona tunatia aibu kiasi hiki? Kuanzia uwanjani wachezaji ni wa hovyo hovyo sana makocha ndio usiseme hadi tunaazima kocha, huku kwenye uongozi Sasa ndio futuhi tupu[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Manzoki yupo anasimamia masanduku ya kura, kuweni watulivu jamaa kaja kama wale waangalizi wa uchaguzi wa kimataifa.
 
Aya mambo mbona kwenye mpira yapo sana, refer kisa cha Luis Figo na raisi wa sasa wa madrid florentino Perez wakati akigombea awamu yake ya kwanza.
 
Nyie wenye akili timamu hata Kadi Huna, hata mpiran huendi, hata michango hutoi

Wale wenye akili ambazo ww unaona za kizuzu ndio hao wenye kadi hai, wanaenda uwanjani, na wanalipa michango

So waache waenjoy wanachokisikia ndio wanachokipenda
Acha utoto wako,unadhani watu wote tunaishi Dar na hatuna majukumu yanayotubana?



Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…