Hehehe! Eti Kenya utatiwa ndani kwa kumwamkua waziri, jameni Watanzania huwa mumeaminishwa mambo ya kiajabu ajabu ya Kikenya. Kuna wakati huwa nikiwa Tanzania halafu nawaskliza vijiweni mkiijadili Kenya bila kunishtukia kwamba mimi Mkenya, yaani vioja, sijui nani kawahubiria na kuwaaminisha hayo yote huwa nawaskia mkiyasema kuhusu Kenya na Wakenya.
Anyway, ukirejelea mada, kwenye masuala ya ufisadi, hamna sehemu nimesema kwamba Kenya hakuna ufisadi. Upo tena maeneo mengi, pamoja na kwamba tumewekeza sana kwenye mifumo. Fahamu kwamba Kenya ilianza kibepari, watu walijua hela tangu hapo awali na rais muasisi wa taifa letu kaendekeza ufisadi na ukabila. Hivyo sio kazi rahisi kuufuta huo mfumo wote, ni hatua kwa hatua. Lakini Tanzania, mlianza kiujamaa, ambapo mfumo wenyewe unapunguza tamaa ila unalemaza uwezo wa watu kutumia akili na kujituma. Wanakua wazembe na kutegemeana bila kuloa jasho, ikawafanya muwe maskini sana hadi mnakuja kubadilisha wakati Nyerere ananyanyua miko na kuachia, mlikua mumeisha kabisa, umaskini ulikua umewatafuna.
Tatizo sasa mliingia kwenye mfumo wa ubepari bila kujifunza kwa hatua, mkaanza kwa pupa, mafisadi mkaanza kuitafuna nchi, vitalu vya madini vikaanza kubaki mahandaki. Mkaanza kutafuna kila kitu kwa pupa, hadi inatajwa eti mnasafirisha meno ya tembo na twiga kwa ndege ya rais. Yaani ikawa yote ruksa, kula huku kula kule, wengine wanawatambia wenzao eti hela ya mboga, mara chenji, mara nyoka mwenye makengeza. Yaani vituko vya wizi kweli kweli, na kila wananchi wakihoji wanawekewa hotuba za Nyerere halafu wanabaki kimya.
Halafu unasema mamilioni waliyogawana wabunge wa CCM kwamba ni propaganda za upinzani, sasa mbona hata katibu wa CCM Bunge mwenyewe alikiri, hebu fuata hii link uone wenzio ambao hawakupata mgao wanavyolalamika
Wabunge wa CCM wagawana hela za CCM, Je wanachama tutagawiwa lini?