Fredrick Nwaka
Member
- Jul 8, 2013
- 53
- 75
Na
Fredrick Nwaka
Tanzania ni nchi inayosifiwa Afrika na duniani kote kwa utulivu wa kisiasa, ikilinganishwa na mataifa jirani kama Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Msumbiji na DRC ambazo zote zimepitia majaribu makubwa ya kisiasa ambayo kama kusingechukuliwa hatua za makusudi kumaliza majaribu hayo huenda nchi hizo zingekuwa zimesambaratika. Sote tunakumbuka ghasia za kisiasa zilizotokea nchini Kenya baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007 na mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994.
Utulivu wa kisiasa nchini umechangiwa na mambo mbalimbali lakini kubwa ni utashi wa viongozi wakuu wa taifa. Utashi ulioanzia kwa waasisi wa Muungano, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Sheikh Abeid Aman Karume ambao walijenga msingi imara ambao umeendelea kuheshimiwa na viongozi waliofuata.
Muungano wetu ambao uliunganisha yaliyokuwa mataifa huru, Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar na kuunda taifa moja, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania April 26, 1964 umekuwa mojawapo ya tunu muhimu kwa umoja, usalama, ulinzi, utulivu na maslahi ya dola ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Kwa kutambua umuhimu wa Muungano mambo 22 yamewekwa kuwa mambo ya Muungano huku jambo la kwanza likiwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mambo mengine ni pamoja na ulinzi na usalama, uhamiaji, utumishi katika Jamhuri ya Muungano na uandikishwaji wa vyama vya siasa.
Hivi karibuni kumetokea baadhi ya wanasiasa ambao ama kwa kujua au kwa kutokujua wameamua kutoa kauli ambazo zinatikisa na kuutweza Muungano.
Makamu mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA – Bara, Tundu Antiphas Lissu akihutubia mkutano wa kisiasa wilayani Babati mkoani Manyara amemshambulia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa misingi ya kikanda.
Amesema namnukuu, “Huyu Rais Mzanzibar sio Mtanganyika, kwa sababu ya miaka 60 ya Muungano huyu Mzanzibari akatoka anakotoka kuja kuvuruga watu huku. Usingekuwa Muungano asingethubutu kufanya hivyo kwa sababu asingekuwa Rais wetu”.
Matamshi haya ya kiongozi wa juu wa CHADEMA yamejaa chuki, kejeli, ubaguzi na yana dhamira ya kuzua mtafaruku usio na tija ndani ya taifa. Nilitarajia hadi sasa CHADEMA ijitokeze hadharani na kujitenga na kauli za kiongozi wake lakini imekuwa kimya. Viongozi wenzake na wafuasi wao wamebariki matamshi hayo?
Tangu alipoingia madarakani Machi 19, 2021 Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amefanya mambo ambayo hayakuwezekana kabla ya hapo. Amefungua shughuli za kisiasa kwa kuruhusu vyama vya siasa kufanya mikutano ya ndani na hadhara bila kubugudhiwa, baadhi ya wanasiasa waliokuwa wameikimbia nchi akiwemo Tundu Lissu mwenyewe wamerejea nchini bila masharti yoyote, amefungulia vyombo vya habari vilivyokuwa vimefungwa kwa sababu mbalimbali, serikali yake imeimarisha uhuru wa kujieleza na kadhalika.
Uhuru wa kujieleza anaoutumia Tundu Lissu umo kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya muungano ambayo imeainisha muundo wa serikali na mamlaka yake, pia katiba hiyo imeweka mipaka na imekataza aina yoyote ya ubaguzi kwa misingi ya dini, jinsi, kabila na kanda atokayo mtu.
Inawezekana vipi kwa Lissu na wenzake kukiuka katiba ya nchi kwa kueneza chuki na ubaguzi kwa misingi ya kikanda huku wakinyamaziwa? Inawezekana vipi kiongozi wa kisiasa ambayo anataka chama chake kushinda uchaguzi kuwagawa wananchi kwa misingi ya maeneo watokayo? Je, ni ujumbe gani anaoutuma kwa watanzania ikiwa chama chake kitapata fursa ya kushika serikali? Bahati nzuri asilimia 77 ya watanzania walizaliwa baada ya Muungano na wengi wao wamepuuza matamshi yake.
Utashi wa kisiasa aliouonesha Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutumia falsafa ya R4 yaani ustahimilivu, mabadiliko, kuvumiliana na kujenga upya uwe nguzo kwa wanasiasa kufanya siasa kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za nchi na si kwa misingi ya ubaguzi na chuki.
Mwingine ni Mbunge wa Jimbo la Konde kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Mohammed Said Issa amesikika bungeni akisema urejeshwe utaratibu wa watu kutoka Tanzania Bara kuingia Zanzibar kwa pasipoti akidai kuwa visiwa hivyo vinazidiwa na idadi ya watu. Alizungumza hayo alipokuwa akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais kwa mwaka wa Fedha 2024/25 na kusema lengo liwe kuvilinda visiwa hivyo.
Huku ni kuturudisha nyuma, haiwezekani miaka 60 baada ya Muungano tuanze kufikiria mambo ambayo yatatugawa badala ya kutuunganisha. Hoja ya kuvilinda Visiwa vya Zanzibar ina mantiki na muungano wetu umeilinda mipaka yote ya Nchi yetu kwa miaka yote 60 ya Muungano.
Ni vyema vyama vya siasa na wanasiasa wakachunga ndimi zao. Madaraka na uongozi wa nchi haupatikani kwa kubagua watu wa eneo, kabila au dini fulani. Wanasiasa watambue kuwa hawako juu ya Katiba ya Nchi na wasitumie kichaka cha udini, ukanda na ukabila kuwagawa Watanzania.
Fredrick Nwaka ni mwandishi wa habari wa Shirika la Utangazaji Tanzania, TBC, anapatikana kwa barua pepe
fredrick.nwaka@tbc.go.tz