Siasa za kimtandao (Oligarchy/ Plutocracy): Historia inayojirudia Tanzania

Siasa za kimtandao (Oligarchy/ Plutocracy): Historia inayojirudia Tanzania

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
5,628
Reaction score
6,411
Kulingana na Jeffrey Winter (2011) katika kitabu chake cha siasa za kimtandao(Oligarchy) anasema " Mfumo wa siasa za kimtandao unajengwa na mtandao wa wasomi wa kiuchumi wanaotumia ukwasi wao kulinda mali zao na kushawishi maamuzi ya Serikali.

Maelezo hayo yaliyotolewa na Jeffrey yanatupa tafsiri kuwa mtandao hujiimarisha kwa kujenga ushawishi unaoweza kuingilia maamuzi ya Serikali ili kulinda maslahi ya wanamtandao.

Historia inaonesha siasa za aina hii hazijaanza Nchini au miaka ya hapa karibuni ila zina mizizi mikongwe sana kwani maandishi ya kale yanaonesha tangu Roma ya Kale mpaka makampuni makubwa ya kimataifa tunayoyaona leo yamekuwa yakiutumia mtindo huu ambao umekuwa ukijenga ushawishi na kujibadilisha kimfumo kutoka kwenye nguvu za kijeshi hadi matumizi ya sheria, fedha na teknolojia.

Maelezo ya Aristotle yalikazia kuwa mfumo huu una tabia ya wenye mali kutawala kwa manufaa yao wenyewe bila kujali masikini. Hapa inaonesha kuwa suala la maslahi mapana ya Umma kuwa sadaka ya maslahi ya watu binafsi.

Katika Roma ya Kale Maseneta matajiri walidhibiti ardhi, Sheria na Mahakama huku wakitumia mikopo mikubwa kama zana ya kutawala kiuchumi na kisiasa wananchi wa kawaida.

Kwa Tanzania historia inaonesha miaka yac1970's navmwanzoni sana mwa miaka ya 1980's wakati siasa ya Ujamaa na kujitegemea ikipigiwa chapuo viashiria vya nguvu za siasa za mkondo huu vilijidhihirisha kupitia kauli iliyotilewa na Mfanyabiashara mmoja tajiri (Mzungu) ambaye ni raia wa Ugiriki aliposema "Serikali yote ya Tanzania nimeiweka mfukoni mwangu".

Hili linatupa kufahamu kuwa kinachoonekana ni kama ncha tu ya barafu inayoelea baharini (tip of an iceberg).
 
Historia inaonesha siasa za aina hii hazijaanza Nchini au miaka ya hapa karibuni ila zina mizizi mikongwe sana
Ndugu mtoa mada, tambua kuwa the only clear road ya kupeleka nchi katika oligarchy ni kitu kiitwacho MARXISM, njia ambayo nyerere aliita UJAMAA, marxism ni nzuri katika makaratasi ila kiuhalisia ni system inayotengeneza deep state gangs kwa maana katiba inawaruhusu wao kutokuwa questioned.

So haya yote ni kutokana na utapeli wa ujamaa uliolindwa na katiba mbovu.
 
Ndugu mtoa mada, tambua kuwa the only clear road ya kupeleka nchi katika oligarchy ni kitu kiitwacho MARXISM, njia ambayo nyerere aliita UJAMAA, marxism ni nzuri katika makaratasi ila kiuhalisia ni system inayotengeneza deep state gangs kwa maana katiba inawaruhusu wao kutokuwa questioned.

So haya yote ni kutokana na utapeli wa ujamaa uliolindwa na katiba mbovu.
Unaweza kufafanua kidogo nahisi kuna mengi siyaelewi kuhusu ujamaa
 
Unaweza kufafanua kidogo nahisi kuna mengi siyaelewi kuhusu ujamaa
Okey

Nyerere alikuwa muhumini wa system za uongozi ilioitwa COMMUNISM, ambayo kwa wakati ule vinara wa communism walikuwa niurusi, china na north korea.

Na wakati ule russia ali invest sana kusambaza ukomonosti,

Sasa communism ni zao la marxism, marxism ni ideoology iliopendekezwa waandishi nguli wawili kutoka ujerumani.

So kwa upande wa nyerere hakuingia deep in communism ila akazama kwa mtoto wake aitwae socialism (ujamaa)

So, ujamaa, marxism, communism ni vitu ambavyo ukivisoma unaona perfection katika kutengeneza uchumii sawa na haki sawa ila kiukweli katika practictability ni systems ambazo zinauza nchi kwa jamaa tawala ambacho ndicho kitakacho control uchumi na rasilimali.

Sasa ili wannachi aweze kupiga hatua zaidi ya limitation ambazo amewekea ndip ile anaonga deep state gangs tofauti na hapo utabaki na umasikini wa kulazimishwa maana wote mnatakiwa muwe sawa.

Ndio maana nyererw alipigana na rushwa kwa maana aliona kwa sytem yake ya uongozi lazima rushwq itawale maana watu hawana uhuru wa kiuchumi kama ilivyo IMPERIALISM.

So chama kinakuwa na nguvu ambazo out of control na kutengeeneza system za upigaji maana hakuna wa kuwauliza chochote.
 
Back
Top Bottom