JF Member
JF-Expert Member
- Dec 14, 2014
- 7,914
- 10,793
Amini naawaambieni mambo ni Magumu mno huku kitaa lakini tuliozoea kutusemea wameshalamba asali na hawajui wafanye nini. Wametugeuka sasa wanaona kazi zetu za bodaboda na uvuvi ni za hovyo.
Bei za vitu zimepanda sana na Serikali imelala. Wapambe wanahakikisha Rais hajui mambo ya nchi. Wanchofanya ni kumpandisha ndege kwenda kuomba/kukopa pesa.
Siasa za namna hii zinalifirisi taifa, wakubwa wote wanalamba asali tu. Biashara pia ni ngumu sana. korosho nayo iko kwenye hifadhi hakuna soko. Parachichi nazo zimedoda.
Ni wakati sasa wananchi tujitenge na wanasiasa tufuate mambo yetu. Wakiita mikutano wasitukute.