Uchaguzi 2020 Siasa za Lissu ni hatari kwa usalama wa CCM

Uchaguzi 2020 Siasa za Lissu ni hatari kwa usalama wa CCM

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2016
Posts
4,701
Reaction score
11,920
Waswahili wanasema kumtawala mpumbavu au mjinga ni rahisi sana, lakini kumtawala mwerevu ni kazi ngumu sana.

Kikwete alimuelewa Lisu na mimi nimemuelewa, alisema "ni kheri Dkt. Slaa awe Rais kuliko Lissu kuwa mbunge"

Sasa hivi sio tena mbunge bali ni mgombea wa Urais kupitia CHADEMA.

Siasa za Lissu zinalenga ktk kuelimisha wananchi kuhusu haki zao huku akitumia kipaji chake cha ushawishi kuwaelimisha wananchi kuhusu uhuru na katiba (kuna wananchi hawajui katiba ni kitu gani ila yeye anawaelimisha)

Hizi siasa ni hatari kuliko siasa za Mrema, Slaa au Lowassa.

Lissu anawaelimisha watu na wanaelimika, ndio maana sera yake ni UHURU NA MAENDELEO YA WATU (amejikita zaidi kwenye uhuru na katiba mpya).

CCM tumieni akili msitumie matamasha kujitathimini.
 
Mpaka sasa hivi nawaza nakosa jibu japo sio kwenye uzi huu. Hivi Job Yustino Ndugai na Tundu Lissu ni nani mnyama wa porini? Hivi Ndugai hajui watanzania tunamuona yeye ni zaidi ya mnyama wa porini? Tena kamzidi hata shetani. Naandika kwa hasira naomba mnisamehe.
 
Kitendo cha kumnyima Lissu hela ya matibabu ili afe ni uhayawani wa kiwango cha juu sana.
 
Lissu ana hatari gani? Kuropoka matusi ndio hatari ?

Mgombea hatari alikuwa Dr Slaa alikuwa anaelimisha

Huyu Lissu amewekeza kwenye matusi
Tumeuchukua ushauri, tutauhifadhi na kuufanyia kazi.
 
Mpaka sasa hivi nawaza nakosa jibu japo sio kwenye uzi huu. Hivi Job Yustino Ndugai na Tundu Lissu ni nani mnyama wa porini? Hivi Ndugai hajui watanzania tunamuona yeye ni zaidi ya mnyama wa porini? Tena kamzidi hata shetani. Naandika kwa hasira naomba mnisamehe.
Job ndugai kasomea mambo ya wildlife management ndio maana mifano yake mingi ni ya wanyamapori
 
Mpaka sasa hivi nawaza nakosa jibu japo sio kwenye uzi huu. Hivi Job Yustino Ndugai na Tundu Lissu ni nani mnyama wa porini? Hivi Ndugai hajui watanzania tunamuona yeye ni zaidi ya mnyama wa porini? Tena kamzidi hata shetani. Naandika kwa hasira naomba mnisamehe.
Umenikumbusha mgonjwa ghali zaidi duniani aliyeteketeza 27bilion kwa miezi mitatu kujitibia
 
Kipimo kwamba watanzania wamemuelewa na katiba na Sheria zake, subiri 28 Oct !
Ukiona kapigwa chini , tena kwa mbali basi just watanzania hawataki porojo
 
Lissu ana hatari gani? Kuropoka matusi ndio hatari ?

Mgombea hatari alikuwa Dr Slaa alikuwa anaelimisha

Huyu Lissu amewekeza kwenye matusi
Unakuwaga "farashuu" sana weye! Hivi ulisoma shule za wenye mtindio wa akili? Ukiambiwa utaje matusi unayajua kweli? Au ukiona neno linakupa uchungu wa kujifungua mtoto ndiyo unaita matusi? Jitafakari!😂😂😂😂😂
 
Waswahili wanasema kumtawala mpumbavu au mjinga ni rahisi sana, lakini kumtawala mwerevu ni kazi ngumu sana.

Kikwete alimuelewa Lisu na mimi nimemuelewa, alisema "ni kheri Dr slaa awe raisi kuliko Lisu kuwa mbunge"

Sasa hivi sio tena mbunge bali ni mgombea wa uraisi kupitia CHADEMA.

Siasa za Lisu zinalenga ktk kuelimisha wananchi kuhusu haki zao huku akitumia kipaji chake cha ushawishi kuwaelimisha wananchi kuhusu uhuru na katiba (kuna wananchi hawajui katiba ni kitu gani ila yeye anawaelimisha)

Hizi siasa ni hatari kuliko siasa za Mrema, Slaa au Lowassa.

Lisu anawaelimisha watu na wanaelimika, ndio maana sera yake ni UHURU NA MAENDELEO YA WATU (amejikita zaidi kwenye uhuru na katiba mpya).

CCM tumieni akili msitumie matamasha kujitathimini.
Ni yeye !
 
Attachments

  • Muda huu Iringa katika mkutano wa kampeni wa mgombea urais wa JMT kupitia CHADEM ( 352 X 640 ).mp4
    1.6 MB
Lissu ana akili nyingi sana yani..... Sio wa sayari hii ni zawadi kutoka kwa Mungu
 
Hapa ndipo CHADEMA tunafeli! Yaani siku nzima hakuna live stream kwenye youtube? Na Sisi hatuna vijana wasomi wa mambo ya IT?
Hili ni kosa kubwa lakini juzi umemsikia TCRA lazim waombe kibali. Lakini hata hivyo Tundu Lissu anajiuza .....kizuri chajiuza bwana, kibaya lazima kijitangaze kwanza
 
Back
Top Bottom