Siasa za maigizo hazifuti damu, heshima hainunuliwi kwa vikao vya ikulu

Nicolas J Clinton Gabone

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2014
Posts
897
Reaction score
559
SIASA ZA MAIGIZO HAZIFUTI DAMU, HESHIMA HAINUNULIWI KWA VIKAO VYA IKULU

Nianze na nukuu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere "Mtu mwenye akili akikuambia jambo la kipumbavu, na wewe ukijua ni la kipumbavu ukamkubalia, anakudharau."

Kauli hii ya Mwalimu Nyerere siyo ya kutafakari kwa historia pekee, ni kioo cha kupimia matukio na hali yetu ya leo. Mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vya Tanzania kuna taarifa zinazoeleza kuwa Mwenyekiti wa CCM amekutana Ikulu na viongozi wa vyama vya siasa kwa kile kinachoelezwa kuwa ni mazungumzo ya maridhiano na Katiba mpya, Mwenyekiti wa CCM yeye anasema siyo Katiba mpya bali ni maboresho, Makamu wa Rais anasema tupambane tupate Katiba mpya!

Nikajiuliza, Je, kweli yalikuwa mazungumzo au ni jina zuri lililobandikwa kwenye jambo tofauti?
Mazungumzo yanaanza pale ambapo pande zote zinaingia zikiwa huru kuzungumza, kusikilizana na kuathiriana na hoja za kila mmoja. Lakini upande mmoja unapoitisha, ukaamua mahali, ukadhibiti mazingira na mwelekeo wa kikao, je, bado tunaweza kuyaita mazungumzo ua maagizo ya Mwenyekiti wa CCM? Au ni hotuba iliyosikilizwa kwa heshima ya mamlaka na umma ukaletewa vipande vya hotuba hiyo.

Hoja yangu kubwa hapa siyo nani alialikwa, bali ni maridhiano ya nini, na kati ya nani?

Maridhiano hayawezi kujengwa juu ya ukimya kuhusu kilichosababisha mgogoro wa kisiasa. Hayajengwi kwa kupiga picha za pamoja wakati maswali ya msingi bado hayajajibiwa. Hayajengwi kwa tabasamu mbele ya kamera huku madai ya kesi za kubambika, utekaji na kupotea kwa wakosoaji wa serikali ya awamu ya 6 yakiendelea kuibua hofu kwa wananchi. Kama kweli dhamira ni kuponya Taifa, kwa nini chanzo cha majeraha kisitajwe? Kwa nini uwajibikaji uonekane kama adui wa maridhiano? Maridhiano yasiyoambatana na ukweli, haki na uwajibikaji yanazaa ukimya wa muda, siyo amani ya kudumu.

Kuna jambo jingine la kutafakari sana, kama CCM na uongozi wake wanaamini hawakukosea, kwa nini wanazungumzia maridhiano? Lakini kama wanajua kuna mambo yaliyolikosesha Taifa utulivu, kwa nini hatua za kurejesha haki zisiwe za kwanza kabla ya kutafuta picha ya umoja na kuihadaa Dunia pamoja na shinikizo la mataifa ya kigeni?. Na kama wao wenyewe wanafahamu historia inayowazunguka, wanawatazamaje wale wanaokwenda kuwapa uhalali bila kwanza kudai majibu ya maswali ya wananchi?

Binadamu ana tabia moja isiyobadilika kamwe, ukijua umefanya kosa, halafu akatokea mtu akakusafishia njia bila kukuhoji wala kukuwajibisha, mara nyingi hawezi kukuheshimu kwa dhati. Au anaanza kuona kwamba anaweza kukubali chochote unachomweleza. Hapo ndipo maneno ya Mwalimu Nyerere yanapata uzito wake. Kukubaliana na jambo unalojua halina msingi hakumshawishi aliyelisema kuwa yuko sahihi, mara nyingi humshawishi kwamba anaweza kukuaminisha lolote na ukakubali bila kuhoji, muda mwingine njaa zako tu ziko kichwani, ubinafsi na kukosa hali ya UTU.

Ndiyo maana viongozi wa vyama vinavyojipeleka kwa CCM katika mazingira ya sasa wanapaswa kujiuliza siyo namna wanavyoonekana mbele ya kamera, bali namna wanavyotafsiriwa nyuma ya pazia. Katika siasa, unaweza kupewa kiti cha mbele, ukasalimiwa kwa heshima na kupigwa picha nyingi, lakini moyoni mwa mwenye mamlaka ukaendelea kutazamwa kwa dharau. Maisha yanatufundisha jambo moja heshima ya kisiasa haipatikani kwa ukaribu na dola inapatikana kwa uaminifu kwa dhamira na ukweli hauhitaji mapambo ili ubaki kuwa ukweli.

Vyama vya siasa, hususani vile vilivyoitwa Ikulu na kuhutubiwa na Mwenyekiti wa CCM, vinapaswa kujifunza kuwa na viongozi wanaoanza kwa kuhoji uhalali kabla ya kusikiliza hotuba. Kabla ya maridhiano, swali la kwanza halipaswi kuwa tukutane lini?, bali haki na uwajibikaji viko wapi?

Nani anawajibika kwa damu ya Watanzania waliopoteza maisha wakati wa uchaguzi wa Oktoba 29? Kwa nini suala hilo lisitangulie kabla ya vikao vya picha za pamoja? Kwa nini vyama vya siasa viitwe kusikiliza maelekezo badala ya kushiriki mjadala unaoweka maslahi ya Taifa ya muda mrefu na kila upande kwenye mizani ya hoja?

Tangu lini Mwenyekiti wa CCM akawa Mwenyekiti wa vyama vyote vya siasa Nchini? Kama kila jambo la kisiasa linaanzia kwake, yeye ndiye anayeita, anayeandaa ajenda, anayeongoza kikao na wengine wanaitika, je, uhuru wa vyama uko wapi? au demokrasia ya mlinganyo wa fikra iko wapi kama viongozi wa vyama siasa wanaitwa Ikulu na kushurtuishwa kusikiliza mawazo ya Mwenyekiti wa CCM pekee? Au vyama hivyo havina viongozi wenye ujasiri wa kuuliza maswali magumu? Je, jukumu lao ni kumlinda Rais dhidi ya maswali ya wananchi, au ni kuwalinda wananchi dhidi ya matumizi mabaya ya mamlaka? Na wanatoka kwenye kikoa wanapongezana na kutabasamu huku mikono yao ikibeba bahasha za kaki zilizo jaa kodi ya wananchi hao hao wanaokandamizwa, kutekwa, kuuliwa na kuswekwa ndani kwenye vituo vya polisi kwa madai ya ugaidi, uhaini na ukosoaji dhidi ya serikali ya sasa. Kwa hiyo tusema serikali ya sasa inatokea mbinguni haifanyi makosa?

Kinachoumiza zaidi ni kuona hata viongozi wa vyama vinavyojijengea taswira ya kusimamia mageuzi wakitabasamu mbele ya kamera kana kwamba Taifa halijapitia majeraha makubwa. Tabasamu la kisiasa haliwezi kufuta machozi ya familia zilizopoteza wapendwa wao. Picha za pamoja haziwezi kuzika wajibu wa kuwajibisha waliohusika. Upinzani usipokuwa sauti ya wanaoumizwa, unabaki kivuli cha watawala. Na kiongozi wa upinzani anayeshindwa kuzuia tamaa ya kuketi mezani pa mwenye mamlaka, huishia kutetea maslahi ya meza kuliko maslahi ya wananchi. Mwenyekiti wa CCM hawezi kuwa msimamizi wa Chama chake, awe msimamizi wa dola, halafu tena ajiwekee nafasi ya kuwa mkusanyaji wa vyama vyote vya siasa Ikulu, wakati serikali anayoiongoza bado inadaiwa na wananchi majibu kuhusu vifo vya raia wa Oktoba 29. Huo siyo mjadala wa demokrasia, huo ni mpangilio unaopaswa kuhojiwa kwa nguvu zote. Taifa halihitaji viongozi vya vya siasa wanaozoea kuitwa Ikulu mara kwa mara. Linahitaji viongozi wanaoweza kusimama, kuhoji, kudai ukweli na kuwajibisha mamlaka bila kuyumbishwa na viti, picha za pamoja au posho za kila mara.

Imeandaliwa na,
Nicolas Jovin Clinton Gabone.
Bukoba, Kamachumu.
31 Julai 2026.
 
Aisee inashangaza sana 😢 inakuwaje kile kikao cha Mwenyekiti na raisi na wale viongozi wa vyama vya siasa ?

Haki hakuna , uwajibikaji hakuna ? Viongozi wengine wa serikali wana madharau kwa raia hasa yule aliyetuita vijana tunaoingiza 30,000 tusubiri kuolewa mimi hata sielewi nini kinaendelea mambo yapo hovyo hovyo.

Watanzania wengi wameumizwa, watu wana madai ya haki na uwajibikaji halafu hao viongozi wa vyama vya siasa ñao walienda ikulu kama mazuzu tu. Mpaka sasa inatakiwa hili jambo liwe na mjadala wa kitaifa. Yaani ni uongo ulaghai na utapeli tu ndio ninachokiona mimi.
 
Makala nzuri na iliyojaa facts za kufikirisha na kusaidia kuinua ufahamu wa mtu...

Nimechukua vipande vya baadhi ya maeneo muhimu uliyoyaandika nami nayaweka hapa chini 👇🏻👇🏻👇🏻kama nukuu za kuwasaidia wavivu wa kusoma makala ndefu ingalau wazione hizi facts ziamushe ufahamu wao..
 
".....Hoja yangu kubwa hapa siyo nani alialikwa, bali ni maridhiano ya nini, na kati ya nani?

Maridhiano hayawezi kujengwa juu ya ukimya kuhusu kilichosababisha mgogoro wa kisiasa. Hayajengwi kwa kupiga picha za pamoja wakati maswali ya msingi bado hayajajibiwa. Hayajengwi kwa tabasamu mbele ya kamera huku madai ya kesi za kubambika, utekaji na kupotea kwa wakosoaji wa serikali ya awamu ya 6 yakiendelea kuibua hofu kwa wananchi. Kama kweli dhamira ni kuponya Taifa, kwa nini chanzo cha majeraha kisitajwe? Kwa nini uwajibikaji uonekane kama adui wa maridhiano? Maridhiano yasiyoambatana na ukweli, haki na uwajibikaji yanazaa ukimya wa muda, siyo amani ya kudumu...."
 
"........Kuna jambo jingine la kutafakari sana, kama CCM na uongozi wake wanaamini hawakukosea, kwa nini wanazungumzia maridhiano?

Lakini kama wanajua kuna mambo yaliyolikosesha Taifa utulivu, kwa nini hatua za kurejesha haki zisiwe za kwanza kabla ya kutafuta picha ya umoja na kuihadaa Dunia pamoja na shinikizo la mataifa ya kigeni?

Na kama wao wenyewe wanafahamu historia inayowazunguka, wanawatazamaje wale wanaokwenda kuwapa uhalali bila kwanza kudai majibu ya maswali ya wananchi....?"
 
Bandiko reefu ila ni kwakuwa Chadema hamkushiriki kwa ukaidi wenu.

Mara hii tu mmeshasahau Juice za ikulu enzi za JK??
 
Hapa ndo ukapiga nyundo ya hatari kwa vyama kama CHAUMA, CUF, ACT WAZALENDO, ADA TADEA, TLP, NCCR MAGEUZI, na vingine ambavyo hata havijulikani viko wapi na ofisi zao...

"......Tangu lini Mwenyekiti wa CCM akawa Mwenyekiti wa vyama vyote vya siasa Nchini?

Kama kila jambo la kisiasa linaanzia kwake, yeye ndiye anayeita, anayeandaa ajenda, anayeongoza kikao na wengine wanaitika, je, uhuru wa vyama uko wapi?

Au demokrasia ya mlinganyo wa fikra iko wapi kama viongozi wa vyama siasa wanaitwa Ikulu na kushurtuishwa kusikiliza mawazo ya Mwenyekiti wa CCM pekee?

Au vyama hivyo havina viongozi wenye ujasiri wa kuuliza maswali magumu?

Je, jukumu lao ni kumlinda Rais dhidi ya maswali ya wananchi, au ni kuwalinda wananchi dhidi ya matumizi mabaya ya mamlaka?

Na wanatoka kwenye kikoa wanapongezana na kutabasamu huku mikono yao ikibeba bahasha za kaki zilizo jaa kodi ya wananchi hao hao wanaokandamizwa, kutekwa, kuuliwa na kuswekwa ndani kwenye vituo vya polisi kwa madai ya ugaidi, uhaini na ukosoaji dhidi ya serikali ya sasa.

Kwa hiyo tuseme serikali ya sasa inatokea mbinguni haifanyi makosa, au siyo.....?"
 
Kwa kifupi sana ni kuwa, njaa za tumboni ndizo zinasumbua hawa viongozi wa vyama hivi...

Walienda kuchukua pesa tu hizo ulizosema "bahasha za khaki"

Lakini deep inside their hearts, wanajua kabisa wanachokifanya ni makosa na ni kusaliti wananchi walioumizwa na kuuliwa ndugu zao...

Iko hivi: Wamechukua pesa za damu na damu ya waliouwawa 29/10 itawatafuna wao pia na vyama vyao...

Biblia Neno la Mungu linasema hivi;

"....Astahimiliye shida, majaribu na mahangaiko hadi mwisho ndiye atakayepona na kuokoka..."

Hiyo👆🏻ndiyo siri ya ushindi wa Tundu Lissu hadi leo. Amesimama ktk mstari wa haki na Mungu ni haki. Haki inamlinda na kumponya ktk kila hatua ya jaribu analopitia/pitishwa...

Nawapongeza CHADEMA kwa dhati kabisa kwa kukataa kushiriki uchafu huu, kwa kuendelea kusimama ktika msimamo wa haki pamoja na kupitia ktk shida na dhoruba kali ikiwemo kutishiwa kuuwawa, vifungo na wengine kuuwawa, kutekwa, kupotezwa na kufanyiwa kila aina ya unyama na unyanyasaji....

Nawahakikishia kuwa HAKIKA MUNGU HAJAWAACHA NA HAJAWATUPA, YU PAMOJA NANYI NA YU PAMOJA NA WANA WA NCHI YA TANGANYIKA. NYIE MUNGU AMEWAPONYA NA AMESHAWAKOA NA KUIKOA TANGANYIKA...

CHADEMA na wananchi wa Tanganyika nawatia moyo kwa kuwa ahadi ya Mungu yehova inasema hivi katika Neno lake Mungu - yaani Biblia 👇🏻

Isaya 43:2-4 SUV
"......Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza. Maana mimi ni BWANA, Mungu wako; Mtakatifu wa Israeli, mwokozi wako, nimetoa Misri kuwa ukombozi wako; nimetoa Kushi na Seba kwa ajili yako. Kwa kuwa ulikuwa wa thamani machoni pangu, na mwenye kuheshimiwa, nami nimekupenda; kwa sababu hiyo nitatoa watu kwa ajili yako; na kabila za watu kwa ajili ya maisha yako....

Simameni imara, msiogope Mungu wa mbinguni yu pamoja nasi​
 
SIASA ZA MAIGIZO HAZIFUTI DAMU, HESHIMA HAINUNULIWI KWA VIKAO VYA IKULU

Nianze na nukuu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere "Mtu mwenye akili akikuambia jambo la kipumbavu, na wewe ukijua ni la kipumbavu ukamkubalia, anakudharau."

Kauli hii ya Mwalimu Nyerere siyo ya kutafakari kwa historia pekee, ni kioo cha kupimia matukio na hali yetu ya leo. Mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vya Tanzania kuna taarifa zinazoeleza kuwa Mwenyekiti wa CCM amekutana Ikulu na viongozi wa vyama vya siasa kwa kile kinachoelezwa kuwa ni mazungumzo ya maridhiano na Katiba mpya, Mwenyekiti wa CCM yeye anasema siyo Katiba mpya bali ni maboresho, Makamu wa Rais anasema tupambane tupate Katiba mpya!

Nikajiuliza, Je, kweli yalikuwa mazungumzo au ni jina zuri lililobandikwa kwenye jambo tofauti?
Mazungumzo yanaanza pale ambapo pande zote zinaingia zikiwa huru kuzungumza, kusikilizana na kuathiriana na hoja za kila mmoja. Lakini upande mmoja unapoitisha, ukaamua mahali, ukadhibiti mazingira na mwelekeo wa kikao, je, bado tunaweza kuyaita mazungumzo ua maagizo ya Mwenyekiti wa CCM? Au ni hotuba iliyosikilizwa kwa heshima ya mamlaka na umma ukaletewa vipande vya hotuba hiyo.

Hoja yangu kubwa hapa siyo nani alialikwa, bali ni maridhiano ya nini, na kati ya nani?

Maridhiano hayawezi kujengwa juu ya ukimya kuhusu kilichosababisha mgogoro wa kisiasa. Hayajengwi kwa kupiga picha za pamoja wakati maswali ya msingi bado hayajajibiwa. Hayajengwi kwa tabasamu mbele ya kamera huku madai ya kesi za kubambika, utekaji na kupotea kwa wakosoaji wa serikali ya awamu ya 6 yakiendelea kuibua hofu kwa wananchi. Kama kweli dhamira ni kuponya Taifa, kwa nini chanzo cha majeraha kisitajwe? Kwa nini uwajibikaji uonekane kama adui wa maridhiano? Maridhiano yasiyoambatana na ukweli, haki na uwajibikaji yanazaa ukimya wa muda, siyo amani ya kudumu.

Kuna jambo jingine la kutafakari sana, kama CCM na uongozi wake wanaamini hawakukosea, kwa nini wanazungumzia maridhiano? Lakini kama wanajua kuna mambo yaliyolikosesha Taifa utulivu, kwa nini hatua za kurejesha haki zisiwe za kwanza kabla ya kutafuta picha ya umoja na kuihadaa Dunia pamoja na shinikizo la mataifa ya kigeni?. Na kama wao wenyewe wanafahamu historia inayowazunguka, wanawatazamaje wale wanaokwenda kuwapa uhalali bila kwanza kudai majibu ya maswali ya wananchi?

Binadamu ana tabia moja isiyobadilika kamwe, ukijua umefanya kosa, halafu akatokea mtu akakusafishia njia bila kukuhoji wala kukuwajibisha, mara nyingi hawezi kukuheshimu kwa dhati. Au anaanza kuona kwamba anaweza kukubali chochote unachomweleza. Hapo ndipo maneno ya Mwalimu Nyerere yanapata uzito wake. Kukubaliana na jambo unalojua halina msingi hakumshawishi aliyelisema kuwa yuko sahihi, mara nyingi humshawishi kwamba anaweza kukuaminisha lolote na ukakubali bila kuhoji, muda mwingine njaa zako tu ziko kichwani, ubinafsi na kukosa hali ya UTU.

Ndiyo maana viongozi wa vyama vinavyojipeleka kwa CCM katika mazingira ya sasa wanapaswa kujiuliza siyo namna wanavyoonekana mbele ya kamera, bali namna wanavyotafsiriwa nyuma ya pazia. Katika siasa, unaweza kupewa kiti cha mbele, ukasalimiwa kwa heshima na kupigwa picha nyingi, lakini moyoni mwa mwenye mamlaka ukaendelea kutazamwa kwa dharau. Maisha yanatufundisha jambo moja heshima ya kisiasa haipatikani kwa ukaribu na dola inapatikana kwa uaminifu kwa dhamira na ukweli hauhitaji mapambo ili ubaki kuwa ukweli.

Vyama vya siasa, hususani vile vilivyoitwa Ikulu na kuhutubiwa na Mwenyekiti wa CCM, vinapaswa kujifunza kuwa na viongozi wanaoanza kwa kuhoji uhalali kabla ya kusikiliza hotuba. Kabla ya maridhiano, swali la kwanza halipaswi kuwa tukutane lini?, bali haki na uwajibikaji viko wapi?

Nani anawajibika kwa damu ya Watanzania waliopoteza maisha wakati wa uchaguzi wa Oktoba 29? Kwa nini suala hilo lisitangulie kabla ya vikao vya picha za pamoja? Kwa nini vyama vya siasa viitwe kusikiliza maelekezo badala ya kushiriki mjadala unaoweka maslahi ya Taifa ya muda mrefu na kila upande kwenye mizani ya hoja?

Tangu lini Mwenyekiti wa CCM akawa Mwenyekiti wa vyama vyote vya siasa Nchini? Kama kila jambo la kisiasa linaanzia kwake, yeye ndiye anayeita, anayeandaa ajenda, anayeongoza kikao na wengine wanaitika, je, uhuru wa vyama uko wapi? au demokrasia ya mlinganyo wa fikra iko wapi kama viongozi wa vyama siasa wanaitwa Ikulu na kushurtuishwa kusikiliza mawazo ya Mwenyekiti wa CCM pekee? Au vyama hivyo havina viongozi wenye ujasiri wa kuuliza maswali magumu? Je, jukumu lao ni kumlinda Rais dhidi ya maswali ya wananchi, au ni kuwalinda wananchi dhidi ya matumizi mabaya ya mamlaka? Na wanatoka kwenye kikoa wanapongezana na kutabasamu huku mikono yao ikibeba bahasha za kaki zilizo jaa kodi ya wananchi hao hao wanaokandamizwa, kutekwa, kuuliwa na kuswekwa ndani kwenye vituo vya polisi kwa madai ya ugaidi, uhaini na ukosoaji dhidi ya serikali ya sasa. Kwa hiyo tusema serikali ya sasa inatokea mbinguni haifanyi makosa?

Kinachoumiza zaidi ni kuona hata viongozi wa vyama vinavyojijengea taswira ya kusimamia mageuzi wakitabasamu mbele ya kamera kana kwamba Taifa halijapitia majeraha makubwa. Tabasamu la kisiasa haliwezi kufuta machozi ya familia zilizopoteza wapendwa wao. Picha za pamoja haziwezi kuzika wajibu wa kuwajibisha waliohusika. Upinzani usipokuwa sauti ya wanaoumizwa, unabaki kivuli cha watawala. Na kiongozi wa upinzani anayeshindwa kuzuia tamaa ya kuketi mezani pa mwenye mamlaka, huishia kutetea maslahi ya meza kuliko maslahi ya wananchi. Mwenyekiti wa CCM hawezi kuwa msimamizi wa Chama chake, awe msimamizi wa dola, halafu tena ajiwekee nafasi ya kuwa mkusanyaji wa vyama vyote vya siasa Ikulu, wakati serikali anayoiongoza bado inadaiwa na wananchi majibu kuhusu vifo vya raia wa Oktoba 29. Huo siyo mjadala wa demokrasia, huo ni mpangilio unaopaswa kuhojiwa kwa nguvu zote. Taifa halihitaji viongozi vya vya siasa wanaozoea kuitwa Ikulu mara kwa mara. Linahitaji viongozi wanaoweza kusimama, kuhoji, kudai ukweli na kuwajibisha mamlaka bila kuyumbishwa na viti, picha za pamoja au posho za kila mara.

Imeandaliwa na,
Nicolas Jovin Clinton Gabone.
Bukoba, Kamachumu.
31 Julai 2026.
nchi ya kipumbavu sana hii
 
Hoja nzito sana mkuu, ila ungeficha id yako...kuna genge linalofaidika na mapungufu ya samuya liko vitani dhidi ya yeyote anayetaka kutia kitumbua chao mchanga!.
Hoja haipigwi RUNGU,

Ina shangaza mtu akutumie freedom of speech 💬 anapewa kesi ya UGAIDII

Nimejifunza mengi SANA Kuna muda watu Wana amua kua kimyaa TU.
 
Kuna jambo jingine la kutafakari sana, kama CCM na uongozi wake wanaamini hawakukosea, kwa nini wanazungumzia maridhiano? Lakini kama wanajua kuna mambo yaliyolikosesha Taifa utulivu, kwa nini hatua za kurejesha haki zisiwe za kwanza kabla ya kutafuta picha ya umoja na kuihadaa Dunia pamoja na shinikizo la mataifa ya kigeni?. Na kama wao wenyewe wanafahamu historia inayowazunguka, wanawatazamaje wale wanaokwenda kuwapa uhalali bila kwanza kudai majibu ya maswali ya wananchi?
Tuendelee kujadiriana kama hivi, na Mh Rais amesema anaendelea kusikiliA maoni na kutekeleza baadhi ya masharti ya Wenzao. Hii ni hatua nzuri angalau tunajadili mambo ya mstakabali wa Nchi
 
Back
Top Bottom