Siasa za matusi hazina mashiko, siasa ni kujenga hoja

Moto wa volcano

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2018
Posts
1,148
Reaction score
2,815
Siasa sio uadui ni ushindani na hamasa ya kuchochea maendeleo, inashangaza kuona mwanasiasa anazungumza jukwaani mpaka mishipa inataka kupasuka. Siasa ni ushindani wa hoja . Kutumia lugha ya matusi kunafifisha jumbe uliyokusudia kwa jamii

Kutoka kwa Raia mwema nisiyefungamana na chama chochote Moto wa volcano
 
We mwenyewe tukikwambia umekosea unahisi umetukanwa.

Tatizo lina kuja ni kwamba ukweli au kukoselewa ni tusi. Je ukitukanwa utasema ni nini?
 
Tuwe wakweli bwana , wewe na mimi tunafahamu yanayoendelea jukwaani kwa wanasiasa wengi, tunashuudia majibizano ya maneno makali yasiyo na lugha ya staha kitu ambacho sio kizuri
 
Kuliweka neno kwenye kundi la matusi bado inategemea eneo,mpokeaji,mtoaji na tafsiri ya wakati.
 
Ikitokea wewe umetukanwa utalipokeaje ?

Naimani moyoni hautafurahia , kwahiyo busara ni vizuri itumike kutambua hata unayemtusi licha ya cheo chake au nafasi yake ya kisiasa na yeye ni binadamu ana roho ya nyama sio vizuri kukwazana
 
Back
Top Bottom