Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,186
- 7,492
Ndugu zangu, kuna tatizo lipo lakini ni kama kila mtu anajaribu kulifumbia macho wakati katika hatua yake ya juu kabisa itakuwa ni hasara ya watu wote.
Katika mazingira mbali mbali unakuta mtu anatetea kitu si kwa sababu kitu hicho ni sahihi bali kwa sababu kulingana na upande aliopo kwa wakati husika kitu hicho kinamnufaisha, au kinanufaisha watu wa kundi lake au kinawaumiza wengine. Hii inaweza kuwa katika level ya mtu, level ya vyama au makundi flani flani hivi.
Aidha, kuna watu wanapinga vitu, si kwa sababu vitu wanavyopinga ni vibaya kwa uhalisia wake bali kwa sababu vitu husika vikifanyika kwa usahihi au kwa haki; anayepinga anaona watanufaika wengine ‘wao’ na kinyume chake.
Kwa hiyo kabla mtu hajatetea au kupinga kitu, badala ya kujiuliza ‘ je! hii ni haki?’ au ‘je! Hii sio dhulma’ hijiuliza mimi nitanufaikaje? Kundi langu litanufaikaje? Siwezi kuwanufaisha wao bila kutarajia kweli? Lakini wanaoumia si wao sasa mimi nipate tabu ya nini? Na mtiririko huo wa fikra unaendelea…… bila kujua kuwa kitu ambacho ni sahihi ni sahihi tu na ambacho si sahihi si sahihi tu.
Ushahidi wa mambo haya ni pale unapoona mtu akiwa katika mazingira 'A' anaunga mkono jambo (Ikiwa ananufaika, au angalau haathiriki kwa wakati huo wakati wenzake wanaumia), na mtu huyo huyo akiwa katika mazingira 'B' ( hanufaiki au pengine anaumia wakati wenzake wananufaika) anapinga jambo lile lile na kinyume chake.
Mwishowe hali hii inasababisha tunakuwa hatuna ‘objective truth’ na hatuna ‘objective justice’. Kwa hiyo tunajikuta tunazunguka katika mhimili wa unafiki kiasi kwamba hakuna anayethubutu kuongea ukweli kama ulivyo.
Katika mazingira hayo, hakuna namna tunaweza kujenga jamii adili, tutakuwa tunajidanganya tu na madhara yake yatamgusa kila mmoja wetu. Labda muda tu ndio huweza kutofautiana kati ya mtu na mtu.
Ni vyema tukajilazimisha kutetea vitu kwa kuwa ni vya haki na muhimu na kukemea vitu kwa kuwa ni dhulma au sio sahihi bila kujali nani yuko wapi au nani ananufaika au kuumia. Kwa kufanya hivyo, ndio tunajenga nchi yenye uadilifu wa kweli ambapo ndio msingi mkuu wa kufanikiwa kama taifa. Kinyume chake ni vigumu kupata maendeleo ya kweli kwa kuwa tutakuwa hatuambiani ukweli na tutakuwa hatuaminiani.