Siasa za mimi Vs wengine sisi Vs wao na hatma ya nchi yetu

Siasa za mimi Vs wengine sisi Vs wao na hatma ya nchi yetu

Mkuu, ni vyema hata kama mtu kakosea amma ukamuelewesha au kumshawishi lakini sio kumlaani au kumuombea mabaya.

Aidha, kama nilivyosema kuwa uadilifu ni kufanya vitu kwa namna ambayo ungetamani kila mtu awe anafanya, sasa fikiria kila mtu akimlaani yule ambaye anaona anakosea hauoni mwishowe tutalaaniana na kuombeana mabaya wote ikiwemo na wewe?

Halafu pia kumuombea mabaya kiongozi akiwa madarakani, ni sawa na kumuombea dereva wa basi apate ajali ukiwa ndani ya basi. Hata kama huyo dereva anakosea, wewe unakuwa umekosea zaidi.

Kwa hiyo nadhani tushawishiane in a positive way hii itatusaidia tuwe pazuri zaidi leo kuliko jana na kesho kuliko leo.
Bw. Aziz Allah ni mjuzi wa yote kwa imani ya DINI yangu tumehusiwa KUKEMEA mabaya ikiwa tushindwa KUYAPIGANIA na pale utakaposhindwa kuyakemea basi angalau UYAKASIRIKIE au yule muhusika mbaya UMSHITAKIE mbele ya mamlaka ya juu ambayo enzi kuu ya Allah Subhana Wataala na yeye ndie muamuzi na usipofanya moja katika hayo manne (KUPIGANIA au KUKEMEA au KUKASIRIKIA au KUSHITAKIA) basi wewe muonewaji ndio utapata dhambi

NB: Kuna hili la KUSAMEHE ambalo lenyewe linaingia kwenye kundi la KUSHITAKIA kwa maana ya kumuachia ALLAH kwa sababu hakuna Binadam mwenye mamlaka ya KUSAMEHE dhambi inayojumuisha maumivu ya watu wengi in case otherwise labda kama jamii nzima tumeumbwa kwa nafsi moja lakini bahati mbaya kila mtu ana nafsi yake aliyozaliwa nayo peke yake tofauti na mwingine "Allahu Yaalam"

*** Unaweza kusamehe wewe kama wewe endapo tu ulichotendewa maumivu yake yanakuhusu wewe binafsi na nafsi yako. But still Allah anaweza kumuadhabu licha ya wewe kumsamehe alie kukosea na ndio maana nasema hakuna binadamu mwenye mamlaka ya kusamehe isipokua Allah mwenyewe kwa sababu yeye ndie mjuzi wa kila jambo. Ndio maana siku zote huwa tunatumia usemi usemao "NAMUACHIA MUNGU" Nina imani usemi huu wewe umezaliwa umeukuta. Basi kuanzia leo fahamu usemi huu upo kwa mantiki hiyo hapo juu waliouanzisha wanajua hilo kwa msingi huo wa Binaadam kutokua na mamlaka ya KUSAMEHE

Lakini pia kumbuka kila shitaka lazima liwe na nia fulani, ni kama vile umeenda kumshitaki mtu Polisi lazima utakuwa na matarajio anayoyategemea kupata ambayo ni matokeo baada ya kuwasilisha shitaka lako, hivyo basi elewa kuwa mimi sijalaani bali nimeshataki kwa nia na matarajio yangu na Mungu anapokea shitaka la kila mtu miongoni mwetu kwa nia na matarajio yake usipokua Allah kwa ujuzi wake yeye mwenyewe ndio hujibu kwa kiasi aidha cha nia yako au vinginevyo kwa sababu hapangiwi cha kufanya

Haijalishi hata kama kila mmoja kamshitaki mwenzie ila mkosaji ndio ataadhibiwa kupitia mizani ya kupima nani kamkosea mwenziwe kupitia taratibu na miongozo iliyopo katika sheria au makubaliano ya KIMAMLAKA, KIMKATABA au KIKATIBA baina yenu. Ama hakika Allah ni mjuzi wa kila jambo na yeye pekee ndie ajuae yaliyo dhahiri na yaliyo sirini na hukumu yake haionei mtu

Hivyo basi Bw. AZIZ MUSSA usitie shaka nipo kwenye "RIGHT TRACK"

Zaidi ya yote nimeuelewa sana uzi wako umekaa kiungwana kabisa kongole kwa ustaraabu wa maandishi yaliyo elezea hali halisi

KARIBU SANA!!!
 
Back
Top Bottom